Mbona UDP na TLP zilikufa?Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
Heshima,
Si lazima kwa mwanasiasa kubaki katika chama kilichomlea, hasa kwa siasa za Tanzania ambazo kwa namna fulani ni za masilahi zaidi kuliko utumishi wa watu. Wako waliohama toka CCM kwenda NCCR-Mageuzi kwenda TLP kisha CCM tena. Kutoka chama kimoja mpaka kingine ni jambo tulilolizoea.
Baada ya Zitto na wenzake kutimka CHADEMA na kwenda kuanzisha ACT-Wazalendo, walikuwa na matumaini ya kustawi. Kilivutia watu. Kilipata mbunge mmoja, Zitto mwenyewe na kuongoza Halmashauri ya Ujiji.
Mh. Rais alianza kuimong'onyoa ACT kwa kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Akaendelea kwa kumpa mgombea urais wa ACT mwaka 2015,mama Anna Mghwira u-RC wa Kilimanjaro.
Rais Magufuli hakuishia hapo, alimpa Juliana Shonza, aliyekuwa Viti Maalum CCM u-Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni na Michezo. Leo hii,mwanasheria Albert Msando ameula kwa kupata ajira Wizara ya Michezo, akiwa mjumbe kwa ajili ya kushughulikia hati miliki. Hii ni siku kadhaa baada ya kiongozi mwingine wa ACT, Samson Mwigamba, kutangaza kutimkia CCM akiwa na wenzake.
Hawa wote waliokimbia/walioteuliwa toka ACT kwenda CCM na Serikali, walikuwa 'wasaliti' toka CHADEMA.
ACT imekuwa shamba zuri la CCM. Ni kama CCM ilianzisha ACT ili kupokea makada waasi.
Sijui kama Zitto ataweza kujenga chama peke yake bila 'wataalamu'. Chama kinaweza kumfia. Ni bora arudi CHADEMA kuimarisha upinzani. Ni ngumu kupata tena ubunge na kuongoza Halmashauri. ACT inafuata njia ya UDP-Cheyo.
Mbona UDP na TLP zilikufa?
Hata Cheyo na Mrema walipitia njia hiyo hiyo.Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
Juliana Shonza ana uhusiano gani na ACT ??alimpa Juliana Shonza, aliyekuwa Viti Maalum CCM u-Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni na Michezo. Leo
Machali yupi unamzungumzia mkuu?? Huyu aliyekuwa mbunge wa kasulu kupitia NCCR-mageuzi??Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
Machali yupi unamzungumzia mkuu?? Huyu aliyekuwa mbunge wa kasulu kupitia NCCR-mageuzi??
Ana historia hii CHADEMANCCR-mageuziACT-wazalendoCCM now!
Mungu nisaidie uzao wangu usiwe na akili kama hiziKwani mkuu mmesahau kama huyu mnamwita ndumilakuwili baada ya kuutaka uwenyekiti, kama lengo la wanasiasa kushika madaraka waongoze wananchi kwa nini ukatae nafasi iyo ukipewa, wewe ukisusa hata mimi nakula uishie kulialia mitandaoni.