Zitto, ACT itakufia rudi CHADEMA

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima,

Si lazima kwa mwanasiasa kubaki katika chama kilichomlea, hasa kwa siasa za Tanzania ambazo kwa namna fulani ni za masilahi zaidi kuliko utumishi wa watu. Wako waliohama toka CCM kwenda NCCR-Mageuzi kwenda TLP kisha CCM tena. Kutoka chama kimoja mpaka kingine ni jambo tulilolizoea.

Baada ya Zitto na wenzake kutimka CHADEMA na kwenda kuanzisha ACT-Wazalendo, walikuwa na matumaini ya kustawi. Kilivutia watu. Kilipata mbunge mmoja, Zitto mwenyewe na kuongoza Halmashauri ya Ujiji.

Mh. Rais alianza kuimong'onyoa ACT kwa kumteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Akaendelea kwa kumpa mgombea urais wa ACT mwaka 2015,mama Anna Mghwira u-RC wa Kilimanjaro.

Rais Magufuli hakuishia hapo, alimpa Juliana Shonza, aliyekuwa Viti Maalum CCM u-Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni na Michezo. Leo hii,mwanasheria Albert Msando ameula kwa kupata ajira Wizara ya Michezo, akiwa mjumbe kwa ajili ya kushughulikia hati miliki. Hii ni siku kadhaa baada ya kiongozi mwingine wa ACT, Samson Mwigamba, kutangaza kutimkia CCM akiwa na wenzake.

Hawa wote waliokimbia/walioteuliwa toka ACT kwenda CCM na Serikali, walikuwa 'wasaliti' toka CHADEMA.
ACT imekuwa shamba zuri la CCM. Ni kama CCM ilianzisha ACT ili kupokea makada waasi.

Sijui kama Zitto ataweza kujenga chama peke yake bila 'wataalamu'. Chama kinaweza kumfia. Ni bora arudi CHADEMA kuimarisha upinzani. Ni ngumu kupata tena ubunge na kuongoza Halmashauri. ACT inafuata njia ya UDP-Cheyo.
 
Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
 
Kwani mkuu mmesahau kama huyu mnamwita ndumilakuwili baada ya kuutaka uwenyekiti, kama lengo la wanasiasa kushika madaraka waongoze wananchi kwa nini ukatae nafasi iyo ukipewa, wewe ukisusa hata mimi nakula uishie kulialia mitandaoni.
 
Ndege mjanja huwa ananaswa na tundu bovu. Zitto ni opportunist. Aliamua kuanza kukimbia kabla ya kutembea sababu ya kubebwa mgongoni. Sasa anaishi kwa kutoa jasho lake.

Amebaki anapiga porojo mitandaoni...wala haeleweki anasema nini.Kuchanganyikiwa sio mchezo
 
Muacheni Zitto apambane na hali yake hata CHADEMA yenyewe haikujengwa siku moja.Ipo siku atatoboa ZZK komaa hadi kieleweke
 
Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
Hata Cheyo na Mrema walipitia njia hiyo hiyo.
 
Zzk kurudi cdm ni ngumu sana, Kwanza alifukuzwa,ingawa wana utaratibu tofauti akirudi ni Junior wa bint Sepeture,pili hatoaminika. Nadhani siasa siyo kitu chema sana kwa kijana,atafute ishu nyingine afanye wakati akisogeza umri atakaporudi kama itakuwa upande wake,amalizie hapo maisha.
 
Chama chenye mbunge chawezaje kufa? Tulia tu utaona mengi zaidi ya hayo. Atakuja jiunga Machali uone wakipata wabunge 2 utasema kinakufa? Chama kikipata mbunge 1 tu hakifi kamwe na hakuna wa kumtoa ZZK Kigoma upande wowote hata ccm wanalijua hili
Machali yupi unamzungumzia mkuu?? Huyu aliyekuwa mbunge wa kasulu kupitia NCCR-mageuzi??

Ana historia hii CHADEMA NCCR-mageuzi ACT-wazalendo CCM now!
 
Usijali hao ni wasaka tonge akiona hachaguliwi huko aliko aweza jiunga hapo ACT. Japo mkia ushakatwa watampokea tu labda awe ameshapata u dc
 
Nadhani umefika muda muafa sasa kwa zito kubwaga manyanga na kukabidhi uongozi wa ACT kwa mwanachama mwingine.

Kukimbiwa na vigogo wasiopungua watano ni kiashiria tosha kuwa kama kiongozi amepoteza uhalali wa kuendelea kukiongoza chama na ni dalili kwamba walioondoka wameona kuwa kiongozi wao hana vision hivyo kubaki hapo ni kupoteza future Yao kisiasa.

Ila kama anataka kukiua kabisa aendelee kungangania tu.
 
zitto na yeye anaona wivu kumuona cheyo na dovutwa wakialikwa ikulu na yeye amesubiri mwaliko akumbuke ikulu haiendi watu wanafiki ni sehemu takatifu
 
Kwani mkuu mmesahau kama huyu mnamwita ndumilakuwili baada ya kuutaka uwenyekiti, kama lengo la wanasiasa kushika madaraka waongoze wananchi kwa nini ukatae nafasi iyo ukipewa, wewe ukisusa hata mimi nakula uishie kulialia mitandaoni.
Mungu nisaidie uzao wangu usiwe na akili kama hizi
 
Back
Top Bottom