Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

ZILLAHENDER MPEMA,
Nime kuelewa mkuu. Asiye kuelewa basi atakuwa ana matatizo makubwa ya ki saikolojiya.

Hivi kwa nini huyu bwana hakujiuzulu kama haku yahafiki yaliyo kuwa yakitendeka? Mbona tunaona wenye kujiuzulu wasio hafikiana na fikra zake? Ka nini yeye hakufanya hivo?

Mbona hajasema mchango wake katika uharibifu uliofanyika? Na kama na yeye alikuwa mmoja wa waharibifu anao wakashifu kila siku, basi ajiuzulu kama anaipenda nchi anavyodai.
Manaake hana sifa ya kuwepo alipo.

As for the main topic, asipo washirikisha wasomi(toka vyuo vikuu), Bunge kujadili mwelekeo wa nchi, matokeo hayangoji mganga wa jadi kutabiri.
Ni HASARA kubwa nchi na vizazi vijavyo.
 
Hakimu Mfawidhi,
Mkuu Hakimu Mfawidhi,
Kwanza usiwe na wasiwasi wowote, hivi ni vitisho tuu, hawa jamaa hawawezi kutufanya chochote wala hawawezi kutushitaki popote kwasababu tumeisha badili sheria zetu za uwekezaji kwenye sheria mpya ya madini, kwenye extractive industries tumeweka kipengele hiki


Hivyo hawa jamaa kama wana malalamiko yoyote, waende mahakama zetu za kizalendo.

Ila ile siku tulipo badili sheria, niliuliuliza swali hili humu
Sasa haya ni matokeo!.
P
 
Pascal Mayalla,
Spot on !! Hii thread yako ya mwaka 2017 naiona kama "Prize Winning Article". Ulichokiandika ndiyo kinatokea vile vile. Uliichambua ile Sheria mpya, ukaonyesha mapungufu, ukaonya na mwishowe ukatoa ushauri lakini wenye mamlaka wakapuuza.

Mchango wako kiukweli ni bora kuliko MPs wote wa CCM na Spika wao kuacha mswaada huo upite na kuwa Sheria.

Hongera sana, you are really a brain and a patriot
 
Mkuu Stuxnet, kwenye nchi zenye udikiteta na freedom of expression ikiwa kwenye mizani, its very risk to be right when wenye mamlaka are wrong, huchelewi kunyooshewa kidole kuwa wewe ni msaliti!, na kuelezwa kuwa hapa tuko vitani kwenye vita vya kiuchumi, na vita vya kiuchumi ni mbaya kuliko vita vya kawaida, na huwa inafahamika wasaliti vitani huwa wana fanya nini!.

Hivyo kazi yetu wengine ni kuobserve tuu, kusema, na yakianza kutokea, tunakumbushana tulisema nini!.

Kwenye hili la vita vya rasilimali zetu, kuna viongozi wetu, kwa kujua Rais Magufuli anataka kusikia nini, wao wanaamua kumsikilizisha tuu kile kile anachotaka kusikia, huku baadhi yao wakijua waz kuwa vitu vingine wanamdanganya.
Sasa tunasubiri mkataba mpya na Barrik usainiwe, tusikie Watanzania tutaelezwa lile deni letu la dola bilioni 190, limeyeyukia wapi?!.

Wakati hao viongozi wakimdanyanga rais, akina sisi huku tunaonya kuwa rais anadanganywa!, because we are no bodies, no body listens, wenyewe kwa wenyewe huko ndani kwa ndani wakagundua lile deni ni la uongo, wakakubali kulifuta kimya kimya, bila kuwaeleza Watanzania sababu, lakini mkataba utakapo sainiwa deni halipo, Watanzania ni lazima tuelezwe, deni letu limekwenda wapi?.

P.
 
Paskali,
Kuna mambo serikali inafanya maamuzi sio ya JPM hata zilizopita unabaki na maswali mengi sana.
Mathalani, wakati wa JK mkataba wa Oil na gas Mtwara ulipita kwa hati ya dharura. Niko tayari kukosolewa kama nakosea, kulikuwa na uharaka gani??

Wakati wa Ben Mkapa, kuna shauri lilikuwa mahakamani kati ya Watanzania wa Bulyanhulu Kahama vs investor alikuwa tayari anataka kuanza kazi. RC wa Shinyanga wakati huo a Rt man in uniform Gen. Kiwelu akatoa amri watu wavunjiwe nyumba hata kabla mahakama kuu kanda ya Tabora hajatoa haki.

Watawala mara kwa mara sijui wakiwa ofisini huwa wanaona nini na sijui nini huwa kinalazimu hati za dharura.

Ni nchi hii hii achilia mbali sheria kuwa mbaya dhidi ya investors. Kuna wakati sheria ilipitishwa hata ukichimba choo ukapata almasi sheria haikutambua kama huna leseni. Na sheria akaja na kitu cha ajabu sana kuwa inawezekana wewe ni mwenye ardhi ila kilicho chini ya ardhi sio chako. Wakati huo wala hakuwa ananyongwa Dangote au ACACIA walikuwa wanaminnywa Watanzania. Cha kufurahisha/kusikitisha, the financial times hawakuona hiyo kama habari.

Suala la maslahi ya Taifa Tanzania, linahitaji mjadala mpana sana na wa wazi. Maana kila mmoja kutegemea na angle aliyopo anaona yuko sawa.







Naomba nikiri, pamoja na ubobevu wa wanasheria wetu na wasomi wetu; perception ina matter sana wakati wa kufanya maamuzi. Nini mtu anaona na kama hataki kumsikiza mwingine, hapo inakuwa ni tabu tabu.

Mchana mwema wakubwa
 
Pascal Mayalla,
Mkuu Paskali mimi nawe tumesoma biblia hata kama hatujasoma sana theojia ua divinity.

Kuna hadithi ya Yusuf alikuwa mfanyakazi kwenye nyumba ya Mkuu wa Walinzi wa Farao wa Misri hapa kwetu ni kama vile Boss wa Walinzi wa Rais (PSU) kwa Marekani inaitwa Secret Service. Enzi za Nyerere alikuwa Peter Bwimbo kwa sasa wanamjua walio kazini; sisi raia hatumjui.

Mke wa mkuu yule wa walinzi alimsingizia (alimshtaki) Yusuf kwa mumewe kuwa Yusuf alitaka kum.... sasa. Mume mtu bila hata kufanya uchunguzi (Investigation) akamchukua Yusuf akamtia kororoni. Kuna nyakati wakubwa wakishauriwa na watu wanaowaamini; huwa hawa-dig deep enough na huo ndiyo ubinadamu.

Rais Mkapa amekiri kwenye kitabu chake kuwa Gavana Balali alimwingiza chaka. Amekiri tena PSRC kwenye ubinafsishaji hawakuwa na good strategy ya namna gani viwanda vinavyobinafsishwa, wahusika wanafanya kile juhudi za kuendeleza shughuli za viwanda.

JPM pia alitabainisha wakati mmoja kuwa "vijana wake wa vetting" wali-recommend kuwa Mtaka hafai hata kuwa DC. Ina maana hata wale waliopendekeza JK ampe u-DC wa Mvomero walikosea. Yet; JPM alikiri Mtaka ni RC namba moja kwake.

Kwa facts hizi, bila shaka watu wa karibu maana ndo mzee yuko nao kila siku ndo anawaamini, sitashangaa in the course of 5 years wasimwingize chaka kwa kukusudia au kwa bahati mbaya. Maana kama vile Mke wa Potifa alipika ushahidi kwa boss wa Usalama kuwa jamaa lilitaka kum.... boss nae kwa hasira bila kufanya further investigation nae akaingia kingi... asomae na afahamu
 
Si kweli kwamba anadanganywa, ni kwamba anajidanganya ili kutimiza malengo yake binafsi, na waliomzunguka nao wanatimiza wajibu wao wa kumsaidia kujidanganya, ili nao wafaidishe matumbo, na ndio maana anateua wale watu wa ndio tu,

Huyo mtu amekuwa kwenye sysyem zaidi ya miaka ishirini, hivyo sio mgeni kujua nini kinaendelea, haya ni matokeo ya pale ajenda binafsi na za chama zinapopewa kipaumbele zaidi kuliko ajenda za nchi, ndio unaona rais na chama tiss, jwtz, police na NEC wote wanabariki wizi wa fedha za wananchi, uaaji , kuteka na uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi, bado naendelea kusubiria contents za hii mikataba tuliosaini juzi na Barrick, sasa kwa sababu kwenye bandiko hili nilisema kuna vipengele vya ajabu, na kwa vile mikataba hiyo imesainiwa wakati tayari tunayo sheria hii mpya ya madini, kama mikataba hii mipya imeingiwa bila kuzingatia kipengele hiki,


then mikataba hiyo ni illegal!. Kama sheria inasema hivi, lazima mikataba yote ifuate sheria!, kisheria huwezi kusaini kitu ambacho ni illegal. Juhudi za kupata details ya kilicho sainiwa zinaendelea,ila kama ni kweli kipengele hiki kimepuuzwa, then hiki ndicho kitu nilichouliza humu, jee Tanzania tunaweza?, tunao uwezo huo?, tuna guts?.
Majibu ni hiki kinachofanyika sasa kwenye mikataba hii.
P
 
Mkuu hizi sheria japo zilipitishwa kwa hati ya dharula lakini zina maslahi makubwa kwa taifa letu. Kwamba zitatumika retrospective sidhani kama itakuwa hivyo. Issue kubwa kwenye mikataba ya madini ni voidable contracts. M Mkuu hizi sheria japo zilipitishwa kwa hati ya dharura lakini zina manufaa kwa taifa letu. Kwamba zitafanya kazi retrospective si kweli kwa sababu kwenye sekta ya madini ishu sio hizi sheria, ishu kubwa ni mikataba iliyojaa udanganyifu kwa hiyo ni voidable contracts. Tanzania inaweza ikaivunja hii mikataba sababu kampuni nyingi zilisaini kwa udanganyifu. Mfano sisi wananchi wengi tulikuwa tunajua ule mchanga uliokuwa unasafirishwa ulikuwa na copper tu kumbe kuna madini mengi ikiwemo na dhahabu iliyobaki, huu ni udanganyifu na mkataba kama huu unavunjika kisheria. Kwa hiyo ishu hapa sio hizi sheria bali ni mikataba mibovu iliyosainiwa huko nyuma. Na hizi sheria zitasaidia kuepukana na mikataba mibovu
 
Mkuu Chagu, waati tunabadili sheria na kuleta sheria mpya, tayari tulikuwa na mikataba mingi kwa sheria za zamani, sasa ili tufaidike na hii sheria mpya, inabidi i act retrospectively, sasa ili hili lifanyike, lazima hao wenye migodi wawe cnsulted na wakubali, vinginevyo tunazidi kuibiwa!.

Hii mikataba ya juzi imesainiwa chini ya sheria mpya, kwenye eneo moja tuu la mikataba sheria yetu mpya inasema hivi


Sasa tafuta kilichosainiwa ni hiki?.
Unatunga sheria ya kujimwambafy, lakini unapofika muda wa utekelezaji hiyo sheria inayohitaji umwamba kweli, kumbe wewe huna umwamba huo!, kama hivi ndivyo sheria yetu mpya inavyosema, juzi mkataba umesainiwa bila kipengele hiki kufuatwa na hivi tunavyozungumza kimeisha nyofolewa kimya kimya!.

Sheria ilisema hatutasafirisha mchanga!, tumesaini mchanga unasafirishwa!. What is the use kusaini sheria na vipengele kibao vya kimwamba, halafu unapojikuta huu umwamba hatuna, tunapeleka marekebisho kimya kimya!.

P
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…