Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,
Kwanza naunga mkono marekebisho ya sheria hizi kufanyika, kwa sababu yanafanyika kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na maslahi ya Watanzania badala ya maslahi ya wawekezaji, japo siungi mkono miswada hii kuletwa kwa hati ya dharura kwa sababu tayari kuna mikataba mingi iliyopo kabla ya sheria hii mpya inayoletwa ambayo itaathiriwa na mabadiliko haya, hivyo ni busara kutoa fursa kwa ushirikishwaji, ili kulinda interests za both parties kwenye mikataba iliyopo na pia kujipa muda kutafakari the consequences kitu ambacho hakiwezi kufanyika bila ushirikishwaji. Udharura huu hautoi room ya ushirikishwaji, japo najua unafanyika kwa maslahi ya taifa ila unapofanyika kwa udharura as if kuibiwa ndio tumeanza kuibiwa leo, unaacha maswali mengi bila majibu kuwa kwani waliosababisha hadi tuibiwe hivi ni kina nani, wako wapi na wamefanywa nini?!.

Tayari pongezi zimeishaanza kumiminika kwa Rais Magufuli na Waziri wa Sheria Prof. Kabudi, huu sio uzi wa pongezi, bali ni uzi wa angalizo la kisheria, kwa vile jambo kama hili liliwahi kufanyika hapa nchini kwetu siku za nyuma, na mahakama kuu ikalifumua, leo linarudiwa tena huku watu wakishangilia kwa mbwembwe, hivyo hapa natoa tafakuri angalizo kuwa baadhi ya vipengele vya sheria hii ni illegal, havitekelezeki, na soon sheria hii itarudishwa bungeni kurekebishwa, unless kama ni kweli sasa nchi yetu inaendeshwa kidikiteta!. Kupitishwa kwa sheria hii fasta fasta, kumenisababishia kujiuliza maswali ya kujiuliza, Kwa vile tunaibiwa kupitia mikataba mibovu, ili sheria hii ilete unafuu ni kama tuu itaanza kutumika mara moja baada ya kusainiwa, swali ni... je, sheria hizi mpya zita act retroactively?.

Kama jibu ni ndio/yes, then Tanzania tutakuwa tunatengeneza tena bad laws ambazo tutakuwa tumevunja mikataba yote iliyopo ambayo baadhi ni ya kinyonyaji kuhusu rasilimali zetu, hivyo kukata mirija ya wanyonyaji hawa, na hawatakuwa na uwezo tena wa kututisha tisha kutushitaki popote zaidi ya Tanzania, kitu ambacho kiukweli ni hakiwezekani, it is illegal.

Angalizo Muhimu la Kisheria.
Kuna baadhi ya watu wakiwemo viongozi wetu wenyewe wanafanya mambo ya ajabu ikiwemo kutunga sheria za kiajabu ajabu na mara baada ya sheria hizi za ajabu ajabu zikiishwa tungwa, watu wanashangilia na kupongeza bila kujua wanashangilia nini na wanapongeza nini!. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Kiingereza, common laws of England ambao unatamka retroactive laws ni repressive na illegal!. Sasa leo tunatunga illegal law, halafu tunashangilia, wakati wanasheria wanajua wazi baadhi ya vipengele, havitekelezeki!. Huku ni kumdanganya rais Magufuli!.

Swali kuu la msingi ni jee Tanzania, can we stand by mabadiliko haya ya sheria zetu kwa kukata mirija ya wanyonyaji?. Jee do we have the guts to stand by the laws kwa mabadiliko haya?. Isije ikawa tunashangilia sasa, kisha tunakuja kugeuziwa kibao kwenye mengine yote ili kushikishwa adabu na mabeberu hawa na mwisho wake tunakuja kujutishwa na mabeberu kwa vilio na kusaga meno?. Nani anakijua kilichomkuta Patrice Lumumba wa Congo kwasababu ya utajiri wa Almasi?. Nani anakumbuka kuhusu blood Diamonds za Angola?. Nani anakijua kilicho muondoa Saddam Hussein Iraq, au Muammar Gaddafi Libya?. Linapokuja suala la mabeberu kulinda interests zao, mabeberu sio watu kabisa ni ma beasts kabisa, hivyo tusipojiangalia, tutakuja kushangaa, mtu wetu anaondoshwa mzima mzima na tunabaki tukishangaa na tusiamini!.

Nakiri kupandisha uzi huu baada ya kumsoma mwana jf huyu
Kipengele cha Tanzania Kutoshitakiwa Nje ya Tanzania.jpg

Mkuu Msemakweli, asante kwa hii. Kwanza naunga mkono hoja ila sio kwa haraka na udharura huu wa Bunge letu, bila kupata muda wa kutafakari na kupima the consequences. Kipengele hiki kikitumika retroactively ni illegal!. Hatuwezi kutunga illegal law na kuishangilia, halafu kesho ndipo tunagundua ni illegal na kupeleka bungeni mabadiliko na kuifuta hii ilegality!. Bunge linalotunga illegal law ni Bunge la mazuzu!. Tuna AG mule, tuna wanasheria kibao wabobezi mule, ambao wanajua fika, Tanzania haiwezi kutunga retroactively law na tukabaki salama!.

Declaration of Interest.
Kwa vile hoja ya bandiko hili ni hoja za kisheria, hivyo naomba ku declare interest kuwa mimi Pascal Mayalla, japo ni mwandishi wa habari tuu, tena wa kujitegemea, ila pia nilisomea sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, USDM na kuhitimu shahada ya sheria, LL.B, tena sio LL.B plain, LL.B yangu ni hons!.. Wakati nikiwa mwanafunzi chuoni hapo, Jaji Mkuu wa sasa wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma ndio alikuwa Dean wangu, Waziri wetu wa Sheria na Katiba wa sasa, Prof. Palamagamba Kabudi ndie alikuwa supervisor wangu wa LL.B dissertation yangu, hivyo naombeni ikitokea nika wa blast walimu wangu, msidhanie ni kwa hasira za vibano vya mwalimu na mwanafunzi, bali hapa ni hoja tuu za kisheria, haitegemei nani ni nani, kutunga sheria ya ku act resroactivey ni bad law!.

Miswada hii ikipita hivi hivi ilivyo, na kama itakuwa applicable retroactively kwa mikataba hii ya kinyonyaji iliyopo sasa, then Tanzania tutakuwa automatically tumevunja mikataba yote ya uwekezaji kwenye maliasili zetu!, hakuna tena kutishiwa kushitakiwa popote nje ya Tanzania, hakuna cha IICD wala cha MIGA, mambo yote sasa ni kwa sheria zetu za JMT. Huu ndio uzalendo, huu ndio uanamume, na kama hawataki kufuata sisi wenye mali tunachotaka, bora wafungashe, virago vyao na wakwende zao!, but hapa naomba tuambiane ukweli, jee sisi Tanzania, tunao uwezo huo?, can we stand?. Do we have the guts and the capacity to challenge them?. Nyerere alijaribu kwenye nationalization na matokeo tunayajua, jee Magufuli atasimama na hii Magufulification na Magufulinaization yenye kila dalili za pseudo dictatorship into full dictatorship, ambazo the rule of law sio issue sana kivile?, ikibidi kuzibadili sheria zetu ili zitufaidie sisi, then tunazibadili bila kujadiliana na yeyote na hata kama kuna atakayeathirika na mabadiliko haya, potelea pote, kwanza tubadili ndio tuje tukae mezani kutafuta a win win situation kwa kutumia sheria mpya!. Hili litawezekana?.

Kwavile wengi humu ni vijana wadago, kwa sisi wazee wa umri wangu, tunakumbuka vita ya uhujumu uchumi ya Edward Sokoine, kwanza wahujumu uchumi walikamatwa wakatiwa ndani, kisha Bunge letu likatunga sheria ya uhujumu, kisha sasa tukaitumia sheria hiyo mpya kuwahukumu wahujumu hao, kuna watu wanajua what happened to Sokoine?. Kwa umasikini wetu huu, with a very poor intelligence, Tanzania do we have the ability and the capacity kum protect Magufuli ili ayatekeleze haya?. Mtu asije akatafutiwa sababu akaondoshwa watu tukabaki tumeduwaa!.

Baada ya Sokoine kuondoshwa, wanamume walitinga mahakamani, Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi zote, serikali ikashindwa vibaya, na kudaiwa fidia ya mabilioni na ikatamkwa wazi kuwa sheria hiyo ni batili!. Sasa tumetunga tena sheria nyingine batili!, Mtunga sheria mkuu wa sheria hii ni mwalimu wangu Prof. Kabudi aliyetufundisha kuhusu retroactive laws ni bad laws!.

Tanzania tunafuata mtindo wa sheria wa nchi za Jumuiya ya Madola ambayo unataka sheria iwepo kwanza ndipo ukiivunja unakuwa umetenda kosa, ili kosa lifanyike, lakini kwanza sheria iwepo kutamka jambo fulani ni kosa. Lakini kama jambo fulani wakati linafanyika halikuwa kosa, lakini huwezi kutunga sheria na kutekekezwa retroactively. Naomba kuwaandaa kisaikolojia kuwa baadhi ya vipengele vya sheria hii mpya ya madini ni vipengele batili, ama soon itarudishwa Bungeni kufumuliwa, na krekebishwa ama ikilazimishwa kutekelezwa kwa lazima, Tanzania tunakwenda kupigwa mwereka mahamani mapema asubuhi!.

Lakini kama sheria hizi mpya, zitaanza kutumika kwa mikataba mipya itakayoingiwa kuanzia sasa, baada ya kuwepo kwa vipengele hivi, then Watanzania wenzangu, wala tusishangilie saana kivile, kwa sababu, tutaendelea kuibiwa kupitia mikataba mibovu iliyopo mpaka ama imalizike, ama tukae mezani ku renegotiate na wawekezaji hawa ambao baadhi yao ni wanyonyaji, wanaweza kabisa wakagoma ili kuhakikisha kuwa wame extract madini yetu yote, na gesi yote na Tanzania tukaachiwa tuu mashimo!.

Ili sheria hii iwe na maana ni lazima ianze kutumika kuanzia sasa ilipopitishwa, ila kwa vile sheria huwa hazi act retroactively, kwa mikataba iliyofungwa kabla ya sheria hii, inakuwa haifungwi na mabadiliko haya, wanasheria mliopo humu tusaidieni, jee vipengele hivi vipya, havivunji mikataba iliyopo inayotaka usuluhishi kwanye vyombo vya kimataifa?.

Jee nini hatma ya Tanzania kwenye mikataba ya kimataifa tulioridhia ikiwemo MIGA?.

Nini hatima ya Tanzania katika uwekezaji kupitia FDI?, wenye fedha zao kweli watakuwa tayari to take such risks?.

Jee tushangilie tuu, au pia tujiulize na the consequences, jee Tanzania tuna guts to stand the international pressures za mabeberu hawa, ama tunapitisha tuu sheria hizi kwa mbwembwe, lakini hatuna uwezo wala jeuri ya kuzitekeleza na ama soon kibano kikitufika, tutaufyata kwa kuzirejesha Bungeni kufumuliwa na kurekebishwa ili kuheshimu mikataba ya kinyonyaji iliyopo!, na amini usiamini, hakuna mwekezaji yoyote wa kimataifa atakubali kuja kuwekeza kwenye nchi yenye sheria za ajabu kama hizi!.

Ushauri wa The Best Way Forward ni Renegotiation to Reach A Win Win Situation
Kupitisha sheria mpya kwa hati ya dharura bila ushirikishwa ni kosa, maadam tumeisha fanya kosa, kufanya kosa sii kosa, kosa kurudia kosa!. Hivyo huu ni ushauri wangu wa the best way forward kwa situation iliyopo ni kukaa mezani na wawekezaji wote tuliosaini nao mikataba kabla ya sheria hii mpya kupitishwa, kuwapigia magoti, kuwaomba wakubali kupitia upya mikataba yao katika win win situation, sisi tupate na wao wapate, hii ya kulazimishana, nawaombeni sana msishangilie na kumvimbishwa kichwa rais Magufuli kuwa tunaweza kila kitu, tuwalazimishe lazime wafuate, asiyetaka na afungashe, aondoke!, jee tunaweza?, tunayo jeuri hii?. Kuna watu kama Billy Gates au Dangote, akikohoa tuu, nchi zinatetemeka!, can we stand?.

Kitakacho Tokea
Kitakacho tokea ni ama baadhi ya vipengele vya sheria hii mpya vitapuuzwa, ama ili kuepuka aibu ya kupitisha sheria mbovu kwa mbwembwe, serikali itapeleka kimya kimya, marekebisho ya baadhi ya vipengele vya sheria hii, kikiwepo hicho kipengele cha arbitration, kitaondolewa ili kurejesha confidence kwa wawekezaji. Kwenye hili, time will tell, kama Nyerere na Sokoine walikuwa ni wakali ukweli ukweli, lakini walishindwa, hivyo kwenye hili la sheria kutekelezwa kwa retroactively, naowaomba mimi niwe mkweli bayana wa nafsi yangu, Mwalimu wangu Prof. Kabudi na wanasheria wake, waliotunga sheria hii kwa mtindo wa zimamoto, wamemdanganya rais Magufuli kwa kumtungia sheria yenye vipengele vya ajabu, halafu rais aka accent, then sheria hii itashindwa kutekelezwa, hivyo soon watapeleka marekebisho Bungeni na kumrudia rais a accent marekebisho hayo, na hili likitokea, naombeni hoja za bandiko hili zizingatiwe, Tanzania tutaonekana ni nchi ya ajabu, tunatunga sheria za ajabu kwa mbwembwe, tunazipitisha kwa mbwembwe, rais wetu ana zi accent kwa mbwembwe, lakini katika utekelezaji ndipo tunajikuta kumbe Bunge letu, na serikali yetu, iliyosheheni wanasheria manguli tena wengine ni waalimu wetu wa sheria wa chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam ambao sisi tulipokuwa wanafunzi tukisomea sheria, waalimu hawa ndio waliotufundisha kuwa sheria yoyote inayotungwa kama ita act retroactively is a bad law, it's illegal, lakini leo, waalimu hawa hawa ndio wamegeuka wanasiasa na wao sasa ndio hawa wametunga illegal law, wakaipitisha, wakampelekea rais akaisaini ianze kutumika, huku wanajua fika retroactively law is illegal law kwenye jumuiya ya Madola, lakini bado wamepitisha, sasa siku ya kurejea Bungeni kuyarekebisha haya madudu yao ya kisheria, hizi sura zao wataziweka wapi?.

Paskali
 
wewe ulitakaje haswa?
Kama mwana sheria unashauri nini?

[HASHTAG]#Achawoga[/HASHTAG]

Mbona mnapenda kuwadanganya na kuwatisha wananchi waliopigika na the so called international preassures na treaties...??

Hivi kuna raha gani wananchi wanayoipata kwa kuendelea kuogopa hizo MIGA and the likes?

Toa ushauri kama msomi sio kututishia na hadithi za kuliwa na Simba kama bibi zetu walivyofanya.
 
Sijui nguvu gani aliyonayo huyu mama jenista mhagama! Jana nimeona mnyika amesimama kuomba hiyo mikataba isipitishwa kwa hati ya dharula ila huyo mwanamke akasimana kupinga!

Na ukiangalia hoja yake dhaifu sana, na kama kawaida Wabunge wa ccm wakampigia makofi.......
Bado tuna safari ndefu
 
Sijui nguvu gani aliyonayo huyu mama jenista mhagama! Jana nimeona mnyika amesimama kuomba hiyo mikataba isipitishwa kwa hati ya dharula ila huyo mwanamke akasimana kupinga!

Na ukiangalia hoja yake dhaifu sana, na kama kawaida Wabunge wa ccm wakampigia makofi.......
Bado tuna safari ndefu

Wabunge wa CCM nilishawatoa akilini kama ni wapigania RASLIMALI zetu.Hawa watu wa ndiyoooooooooooooooooooooooooooooooooo bila kufanya tafakari zaidi.Miswada hii ilitakiwa wanasheria waidadavue vizuri ili iwe inanguvu zaidi.

Kwenye Katiba yetu inaweka wazi kabisa haki ya raslimali zetu lakini Majambazi ya CCM yakatengeneza ya kwao wakaipeleka kwa HATI ya dharula leo tunapigw akama wendawazimu tu.

Miswada ya sheria ilitakiwa iwe inapewa muda wa kujadiliwa hasa na wanataaluma bila kujali itikadi zao.Kwetu tumeweka chama kwanza Taifa baadaye.Usimshangaye Jenista Mhagama hawana tofauti na Musukuma na Kibajaji
 
Kuna option ya kupitia mikataba upya na kuisajili kwa sheria mpya.

Kumbuka suala la makinikia limewaleta mezani na kutupa nafasi ya kubadili kabisa mikataba hiyo kwa sheria mpya ( haraka ya hati ya dharura kuwahi majadiliano)
 
Ni jambo la kufikiria sana. Wengine wanataka iwe ya dharula, maana hata wakipewa mwaka mzima wa kupitia sheria hii hawawezi kuisoma, na hata wakisoma hawataelewa. Ndio maana kwao dharula haina shida. Hao ni akina Msukuma, Kibajaj na Goodluck.

Mimi ni mwana CCM, hatua iliyochukuliwa ni nzuri saaana, ila isiwe ya dharula.
 
Pascal Mayalla,

My brother, hapa bwana panataka akili kubwa wala sio majority participation hii inayoendelea sasa nchini juu ya masuala haya, kwa sisi watu wazima tuliopata neema ya kuuona utendaji wa serikali za awamu zote tano tunahofia historia isije ikajirudia kama ilivyokuwa wakati wa Mwl Nyerere na sera zake za Nationalization ya njia kuu za uchumi toka kwa wawekezaji hasa wa kigeni ambao wakati huo tuliwaita wanyonyaji na miradi ya uwekezaji wao tuliiita mirija,

Kwa kila aina ya mbwembwe tulifanikiwa ku-forfeit the so called mirija yote ya kiuchumi toka kwa makupe hao na kuifanya kuwa mali ya umma, baada ya zoezi hilo hao MABEBERU waliji-organize duniani kote na matokeo yake cha moto tulikiona hawa jamaa walitu-drill accordinglly mpaka uchumi wa nchi uka-paralyse na hivi ndivyo wanavyoipiga sindano za ganzi serikali ya Nicholas Madullo wa Venezuela tokana na sera za Marehemu Hugo Chaves. Hofu,

Tahadhari na maswali yako vina maantiki pana sana ktk mjadala huu tete isipokuwa inahitajika electromagnetic telescope kupambanua logic hiyo.
 
Tukiamua tunaweza tatizo mabashite ni wengi

Labda kaka, ila wajuzi na wasomi wa kweli tunao, tatizo liko pale pale na tunatumaini halitakuwepo, ni tabia, ubinafsi, uroho, kutokuwa wazalendo, kutokuangalia mbali na kufikiri ya karibu...

Tunaweza kwa hili kama wananchi wote kwa pamoja 110%, bila kujali tofauti za vyama au itikadi..

NARUDIA, TUNAWEZA...
 
Pascal Mayalla,
mkuu, kwenye awamu hii reasoning ya wasomi wa Kitanzania waliomo serekalini na chamani imekuwa paralysed na JPM intimidation.
utadhani wamerogwa vile.
misukule.
hakuna wa kusema fyoko hata kama wanajua kinachofanywa na kusemwa si sahihi!
 
"Isije ikiwa tunashangilia sasa kisha tunakuja kushikishwa adabu na mabeberu hawa na kujutishwa"

Hilo ndilo linatusubiri Paskal wazungu wanatusubiri turukeruke kama mahindi ya bisi kwenye moto then watuonyeshe upumbavu tuliosani kuwapa madini kisheria
 
jingalao,


Wananchi unaowazungumzia hapa hawakuifikia hali hiyo kwa sababu ya bandiko hili la Paskal,wamefikishwa hapa na sera na sheria mbovu za uwekezaji zilizopitishwa na wale tuliowapa dhamana.Wawekezaji ni sawa na mgeni afikaye nyumbani kwako,usipomkaribisha hawezi kulazimisha kuingia sebuleni kwako,tuliwakaribisha wenyewe tena kwa "karibu za dharura" zilizotamkwa kwa mbwembwe huku tukitumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kwenda kusaini "karibu za dharura" Hotelini London.

Tusigeuze shingo kwa hasira kushambulia watu wanaoleta mijadala juu ya Rasilimali zetu,Rasilimali zetu tulizigawa wenyewe tena kwa kuwapigia magoti wawekezaji huku tukitumia nguvu kuzima kila sauti iliyopazwa kupinga ugawajwi wa Rasilimali zetu.

Wakati viongozi wetu wakituhoji swali la kizushi eti "tumerogwa na nani," aliyetuuliza swali hilo alikuwa ni sehemu ya wabeba tunguli katika ibada za kishirikina za kuliroga Taifa letu,alikuwa sehemu ya baraza la mawaziri lililojadili na kuridhia uwekezaji,na alikuwa sehemu ya bunge lililojadili na kupitisha kifungu kwa kifungu sheria mbovu zilizowapa haki wawekezaji kubeba hadi vumbi(makinikia)na kulisafirisha ulaya.

Hasira zako juu ya mleta hoja ulipaswa uzielekeze kwa wale waliotufikisha hapa,ccm na serikali yake bila unafiki wowote ndiyo waliotufikisha hapa tulipo kwa fikra zao za dharura,mawazo yao ya dharura na sheria zao za dharura.Masuala nyeti ya Rasilimali zetu hayakupaswa kujadiliwa kwa dharura,lakini kwa sababu account za viongozi wetu zilizopo huko ng'ambo zilikuwa zimejazwa mapesa,waliamua kutoa kila kitu kwa dharura bila kuwafikiria hao unaowaita wananchi masikini ambao leo mnajaribu kuwafanya ngao ya uharibifu wenu.
 
Back
Top Bottom