Ziraili wa gizani

Ziraili wa gizani

JamiiForums-288297360.gif
 
Asili ilipochagua usiku iwe ndio wakati wa kulala kuna siri kubwa ilifichwa huko
Kifo kinauma sana hasa anapoondoka mtu tumpendaye sana...nafuu ni kwamba unajua kwamba kafa na hutaweza kumuona tena.....
Kuna hili la kupotea watu
-kuna watu wanapotea kisha wakaonekana wakiwa hai hata kama wana majeraha
-kuna watu wanapotea kisha wakaonekana maiti zao.. Inauma sana
-kuna watu wanapotea kisha mabaki yao yakaja kuonekana baada ya muda fulani wakiwa wameoza kabisa ama imebakia mifupa tu
15a5cc703468e7d8d3a0ffd95ee22c5e.jpg
pamoja na maumivu yote hayo lakini unajua fika kwamba hatimaye kaonekana japo mabaki
Kimbembe kiko hapa!
Kuna watu walipotea halafu wakapotea kabisa kabisa, hawajawahi kuonekana tena wala maiti zao wala mabaki yao! Yani hawakuacha alama yoyote
Mwili wa binadamu una hulka moja. Haupotei kimoja lazima kitabaki chochote cha kukutambulisha iwe mabaki iwe maiti nk....lakini unaposoma habari za unsolved mysteries ama disapearances, kuna kitu kikubwa mno utakipata humo cha kutisha
Kiza kina meno! Kiza kina roho! Kiza kina mauti! Kiza kinameza na kupoteza kabisa.

Ulimwengu wa giza ni ulimwengu wa roho. Roho ya giza ikikukamata utapotea milele na hutakaa uonekane hata unyayo wako
Giza lenye roho hutengeneza maumbo ya ajabu na kuogofya, haya ndio maziraili yanayotowesha watu.

a9aa9c389a7f3ba1a7d1b6da85091cfb.jpg

Hii hutokeaje?
Scenarios ni tofauti... Mtu alikuwa karudi nyumbani salama lakini mara anaaga kuwa anatoka mara moja..hiyo ndio kwaheri.. Hutakaa umuone tena.

Tumewapoteza wengi kwa style hii...hata hapa tunaweza kuwa na mifano hai(sio wa Ben), ndege ya Malaysia ni mfano mwingine mzuri tu! Haijawahi kuonekana pamoja na technology ya kisasa mno ya kuitafuta!

Uhalisia ni UPI?
Kuna roho hulishwa/hula binadamu hai kama alivyo mzimamzima! Na hazikuvizii bali unaenda kwa wito unaaga kabisa watu uliokuwa nao.

-natoka kidogo
-kuna mtu namuona hapo jirani
-nimeitwa maramoja
-Mimi natangulia home nk nk
Ni wito ambao huja bila kutambua na sometimes wala hujui ni kwanini unaitwa unaitiwa nini na unaitwa nanani ama kwanini unawaacha wenzako na kuondoka mwenyewe! Cha kushangaza unaondoka ama unaenda bila hofu tena kwa kujiamini
Dunia halisi ni replica ya ulimwengu wa roho ukiona kuna fisi mla mizoga kuna roho ziko hivyo pia! Ukiona kuna simba na chui walao fresh kuna roho zipo hivyo
Ukiona kuna funza nk kuna roho zipo hivyo pia
34bdc63503c2d4d5e619d398fced26e6.jpg
technology ya camera kali zinazojiendesha automatically zimesadia kuweza kupiga picha kama hizi za viumbe vya ajabu usiku! Je hivi ndio hao ziraili wa kiza? Huku kwetu tungehitimisha kwa kusema kwamba kachukuliwa msukule!
Mganga mbona tunastishana usikuusiku?
 
This was caught on my in-home security camera . I'm the only one living here . Looks like someone watching me holding on to my bedpost . It's kind of creepy.
FB_IMG_1696441880830.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wa Dr.Dismas Chami aliyekua Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu, Tabora umeokotwa maeneo ya Malolo, Tabora asubuhi ya leo. Dr.Chami aliondoka nyumbani (Kaliua) jumatano ya September 4 na kumuaga mkewe kuwa anakwenda mjini Tabora kikazi na angerejea kesho yake. Hata hivyo hakurejea na simu zake hazikupatikana.

Familia ilimtafuta kwa wiki nzima bila kujua alipo, lakini ilipofika jumatano ya September 11 simu zake zilipatikana. Hata hivyo alipopigiwa hakupokea. Baadae alituma sms kwa mke wake iliyosomeka "Nisamehe sana, baada ya dakika chache sitakua nanyi duniani. Simamia kila kitu nilichokiacha. Pesa zote zipo CRDB bank, simamia watoto wasome. Kwaheri"

Baada ya kutuma sms hiyo simu yake ilizimwa na hakupatikana tena. Polisi kwa kushirikiana na familia waliendelea kumtafuta bila mafanikio. Hatimaye leo mwili wake umekutwa maeneo ya Malolo, ukiwa umechomwa sindano. Pembeni ya mwili huo kuna madawa mbalimbali ya hospitali ambayo inadaiwa yalitumika kujidunga/kudungwa.

Bado haieleweki kama amejiua mwenyewe kwa kujidunga madawa au ameuawa na watu waliomdunga madawa hayo. Haijafahamika pia kama sms aliyotuma kwa mkewe alituma kwa utashi wake au alikua chini ya shinikizo. Polisi wamesema wanachunguza chanzo cha kifo chake kujua kama kimetikana na migogoro ya kifamilia, Msongo wa mawazo, madeni, ugomvi binafsi au sababu nyinginezo. Rest easy Dr.Chami.!

HUYU HAPA
 
Back
Top Bottom