Zipi sababu za msingi za kuhamishia TANAPA Serengeti?

FisadiKuu

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
8,167
13,443
Wasalaam Wanabodi...

Jana nilileta uzi wa malalamiko yangu juu ya kwanini Serikali yetu tukufu itake kuhamisha ofisi za TANAPA kutoka Arusha na kuzipeleka Serengeti sambamba na kujenga uwanja mkubwa wa ndege wilayani humo.

Je, kuna sababu gani ya kutaka kupeleka TANAPA Serengeti? Na kuna sababu gani ya kutaka kujenga awanja mwingine mkubwa wa ndege huko angali KIA ipo? Au tunataka tuiue KIA na kudhoofisha baadhi ya mikoa/maeneo/kanda flani flani hapa nchini?

Hivi huko Serengeti kuna Tours Company ngapi? Je, mbuga ya Serengeti inaleta watalii wengi kuliko Ngorongoro, Manyara, Tarangire na Mount Kilimanjaro kwa pamoja? Au tunafanya hivi kwa makusudi ili kila kitu kielekee kule tunakokupenda sie kwasababu labda kule tulikosa uungwaji mkono?

Naomba tujadili...
 
Kama waliweza kuwashusha madogo kwenye bus wakatembea kwa miguu watashindwaje kwenda serengeti.
Nchi haina ipango mara asubuhi mtu anahama kwenda dodoma pa kukaa hana anakimbilia chuoni, tusishangae ndio nchi ya vi-wonder na tuvumilie mpk 2025
 
Back
Top Bottom