Zingatia ninayokwambia Mwanangu

Zingatia ninayokwambia Mwanangu

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
Kwenye haya maisha usipokua Mbishi na ukaishi kibishibishi popote unapoenda ukakaa ukakubari tu watu wakuoneeonee kibwegebwege, mwanangu unakubari tu kila mpuuzi anachukua maamuzi ya kukuoneaonea tu kirahisi rahisi tu unamuacha mjinga mmoja anakuoneaonea na wewe umekaa tu unamwangalia.

Sawa Mwanangu umeshindwa kurusha ngumi eeh sababu yule anakuzidi nguvu mwili mkubwa wewe ulingani nae ila umeshindwa kweli kujitetea hata kwa kurusha vitofa Mwanangu hujafanikiwa hata kuokota Maandazi ya Mungu kweli Mwanangu ukajitetea mwenyewe?

Jipambanie mwenyewe Mwanangu dunia hii haipo fair hata kidogo watu hawa-play fair kila angle ya hii dunia kuna wapuuzi wao wanacheza rafu kila mchezo hata kwenye gemu fair. Usikubari wakunyong'onyeze Mwanangu. Pambana. Ukiweza na wewe cheza rafu tu ila cheza kwa umakini maana marefa wa mchezo wana wachezaji wao ndani ya uwanja hawachelewi kukupa kadi nyekundu Mwanangu.

Mwanangu kama wewe ni msomaji mzuri wa Biblia utakumbuka Bwana Yesu alisema kwamba ukipigwa Shavu la kulia basi mgeuzie na la kushoto ila cha ajabu Petro alimkata mtu sikio la kulia Yesu hakumwambia yule mtu ageuze na la kushoto ili Petro alimalizie na lile sikio la kushoto yule mtu ayapoteze masikio yote mawili. Mwanangu unajua Bwana Yesu alimaanisha nini kutengua kauli yake aliyoisema mwenyewe na kumponya yule mtu aliekatwa sikio badala ya kumwambia Petro maliza na sikio la pili?

Mwanangu nakukumbusha usiishi kinyonge tena usikubari kuonewa popote unapoenda pambana kwa jasho na damu, asitokee kima yoyote mchovu mchovu wa kukuambia chochote kwenye kujipambania kwako, kaza Mwanangu tena kaza sana.

Na huu ni wosia wa Babu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom