Zingatia haya akilini mwako

Zingatia haya akilini mwako

Bei Rahisi Electronics

Senior Member
Joined
Apr 4, 2025
Posts
197
Reaction score
583
Jambo la kwanza naombeni tumpe sana Mungu nafasi katika maisha yetu ikiwa tunayahitaji sana amani,,Tusiache kumwamini Mungu hata kama nafsi zetu zimebeba majuto , Maana kumwamini Mungu kunaleta roho ya kujiamini na ujasiri wa kuendelea na utafutaji wa siku zote....

images (7).jpeg


ENDELEA NA (KUSOMA ) đź§µ.

Mambo Yafuatayo ni Yakuzingatia Katika Maisha.

👉 KISASI KIZURI NI KUPAMBANA ZAIDI YA MWANZO.

Hasira zimewapelekea watu majuto ya kudumu maishani mwao; Kuingia jela, kufilisiwa mali, Kupotezwa. Mawe unayorushiwa yaokote kutengeneza ukuta, Huwezi kupambana na aliyekuzidi. kuwa kimya haimanishi wewe mjinga la hasha bali unajua safari yako ni ndefu, Utalipa kisasi kwa wangapi? Waliokukosea ni wengi. Haki kwa ajili ya matajiri tu, Tafuta na wewe za kwako uwanyanyase, Sahau maskini kutendewa wema.

images (4).jpeg


👉ADUI HATOKI MBALI.

Anguko lako linasababishwa na unaowamini, Ndio maana kwenye death crime investigation wahisiwa wa kwanza ni watu wa karibu.

Kuwa msiri kuficha neema zako, Wezako wanazitamani. Kumbuka waliomtumbukiza Yusuph kisimani ni ndugu zake.

images (3).jpeg


👉 NYAKATI.
Mungu huwaleta watu kwa maksudi maalum Katika maisha yako kwa kipindi Fulani, Baadae huwaondosha Hivyo usin'gan'ganie mtu jua wakati wake umefika wa kuondoka.

images (6).jpeg


👉 ALIYEKUZIDI MAFANIKIO AMEKUZIDI NA DHAMBI PIA.

Kwenye utafutaji kumkosea Mungu hakuepukiki, Msikitni na kanisani ni sehemu ya kutubu dhambi na sio kufaata mafanikio, Hakuna mafanikio kwenye democracy, Ujanani ni utafutaji uzeeni kutubu.

250px-Le_Grand_Saint_Michel,_by_Raffaello_Sanzio,_from_C2RMF_retouched.jpg


👉 ANGALIA HURUMA YAKO.

Watu wengi wabeba mizigo sio ya kwao , Mara nyingi matatizo tuliyonayo yanatokana na Mwenendo mbaya wa tabia zetu, Mungu hutufunza kwa kutuadhibu kulipia ujinga tuliofanya, wewe unaenda kumtua, Shauri yako!.
📌Simanishi usisaidie watu.

Beggars_in_the_street_2.jpeg


USITIGEMEE SUPPORT KWA WATU WANAOKUJUA.

Never ever, Anayekufahamu ni mshindani wako anataka uwe vilevile, Zaidi atakukopa na kukusema udhaifu wako, vizuri usitumie show off kwenye Utafutaji wako Hakikisha Uweleweki ikiwezekana Nenda mbali katafute.

images (9).jpeg


👉KAMA ULIMFANYIA MTU UBAYA HASAU KAMWEE!.

Ulimnyanyasa wakati hana kitu, Ulijua hatofika kokote? sasa amafanikiwa unarudi kwake... unajichekesha kama halijatokea jambo_ kumbuka maumivu ya manyanyaso yako ndo yamemfanya kuwa hapo.
Kwa iyo kaa mbali!.

images (2).jpeg

Mwisho.
Kama Kuna chochote unaweza kuongezea, Usisahu Kunifollow, Kulikes ,Kukoment na ku share.
 

Attachments

  • images (7).jpeg
    images (7).jpeg
    18.6 KB · Views: 18
ambo la kwanza naombeni tumpe sana Mungu nafasi katika maisha yetu ikiwa tunayahitaji sana amani,,Tusiache kumwamini Mungu hata kama nafsi zetu zimebeba majuto , Maana kumwamini Mungu kunaleta roho ya kujiamini na ujasiri wa kuendelea na utafutaji wa siku zote....



Tumtafute Mungu yupi ? Kuna Mungu wengi sna kila mmoja anadai yeye ni .sahihi kuliko mwingine 🤔
 
ambo la kwanza naombeni tumpe sana Mungu nafasi katika maisha yetu ikiwa tunayahitaji sana amani,,Tusiache kumwamini Mungu hata kama nafsi zetu zimebeba majuto , Maana kumwamini Mungu kunaleta roho ya kujiamini na ujasiri wa kuendelea na utafutaji wa siku zote....



Tumtafute Mungu yupi ? Kuna Mungu wengibna kila mmoja anadai yeye ni sahihi kuliko mwingine 🤔
Haijalishi utofauti wa Imani ila Mungu ni mmoja
 
Back
Top Bottom