Zinduka: Siasa inanunua watu, Polepole naye kanunuliwa

Wadau, kama channel 10, itaendelea kuleta wachambuzi ambao ni bias , kama Humphrey polepole, ni lazima tuikache hii TV kama tulivyo ikataa TBC na star TV , huyu jamaa kutumwa ila amekula vidonge vyake humu jamii forum na walio mpigia simu wamemchana, huyu jamaa siyo mchambuzi huwezi kumshambulia MTU eti ni fisadi , kwamba mwaka 1995 Mwalimu nyerere alimkataa, kama alikuwa fisadi kwanini alipewa uwazili Mbele ya macho ya nyerere, Polepole anasema eti kama CCM ingepitisha mgombea mwenye tuhuma angetembea tanzania nzima kuzungumza ukweli , kapigiwa simu akaulizwa kuwa Maghufuli ni msafi? Tuhuma za kuuza nyumba za taifa ? Repoti ya CAG ? Hakujibu anabaki kusema Lowasa ni fisadi? Nafikili watanzania kwa umoja wetu watu kama hawa akina polepole tuwakatae na kuwapuuza ikiwezekana kuwazomea kabisaa , na Television zinazo leta watu wa namna hii tuzichukie na tusifuatilie vipindi vyao, Tunataka mabadiliko kama ukawa siyo wasafi waache wachukue nchi pengine itakuja kuzaliwa kitu kingine Mbele ya safali siyo ccm ituaminishe kuwa ndio wako safi wakati ni mbwa mwitu na fisi wakubwa eti taiga kubwa kama hili liongozwe na mawazo ya Nape , magufuli na kinana watanzania tunamatatizo mengi ccm mnataka mtuaminishe na tuyasahau matatizo yetu wakati Wa uchaguzi, hamtatuweza hii ni mwendo mdundo mpaka kieleweke, kama Prof.Lipumba amezingua , na Dr.Slaa bado analegalega lakini watanzania bado wanaamini katk mabadiliko ndio kwanza watu wanaongezeka itakuwa Humphrey polepole mchumia tumbo alie tumwa na CCM hamtamzuia Lowasa kuiona ikulu hii ni safari ya mabadiliko nje ya CCM , mwendo mdundo mpaka Ikulu, UKAWA PAMOJA TUTASHINDA.

MKUU sikusikia uchambuzi wake. kama ndivyo kuna haja WARYOBA kumtimua kwenye timu take ya katiba nimeamini sasa watanzania sasa hawa watu wametufanya wapumbavu vya kutosha wanazidi kunipa hasira nikalale kituoni trh 25! Yaani makongamano yote aliofanya na anayoendelea kufanya no kufisadi pesa ya mfuko wa marehemu Nyerere? kwa uelewa wangu makongamano hayo nikuelimisha wtz wakatae rasimu iliyochakachuliwa na mafisadi wa ccm Leo hao hao anawataka warudi iliwaipigie kura ya ndio. Inamaana polepole kweli hats wewe msomi mzima hujui mchi hii nini kinatusumbua unakuwa ndumilakuwili? Hakuna bamadiliko ndani ya ccm hata yesu akirudi! Mgombea yeyote was chama chochote ananadiwa na ilani iliyoandaliwa na chama husika na ilani ya ccm imesha andaliwa na akina wasira (Tyson) walewale ambao wapo toka ukoloni raising anatakiwa aitekeleze. jiulize makongamano ninayofanya ni ya nini kama sitaki chamambadala kikamate usukani? kura za maoni umeziona ccm hakuna wabunge wapya ni walewale waliokuwa wakisemabungeni ndiooo ndio wamerudi kwasababu walikuwa na fedha ya kutosha waliolipwa kwenye bunge la katiba ambalo kila siku unatembea kila mkoa kutudanganya kuwa halikutundea haki liliondoa maoni yetu kwenye rasimu. tukuaminije? Ukawa ni rasimu ya WARYOBA ndio mpango mzima baada ya uchaguzi! Ccm no kurudisha gharama walizonunua kura na watakazo endelea kununua kura ndio mpango mzima baada ya uchaguzi! Ukowapi polepole au umeshapata mgao wa escrow!!!!?
 
Hivi tumejiuliza kile kipindi nani amekilipia nakufanya Polepole aongee yake?
 
Kaongea ukweli kuhusu Ukawa. Mbana tunataka kusikia mazuri tu ya ukawa lakini mabaya hatutaki?
 
Ila tukiacha ushabiki wa kisiasa ukweli unabaki pale pale Edward Ngoyai Lowassa ni FISADI Papa,ananuka rushwa hafai kabisaaaa
 
Mwandishi wa Jana nampongeza maaana hata yy alishtuka kumwona polepole tofauti....
 
Na ndicho kinachoendelea jf siku hizi. Lowassa alikuwa shetani, ilikuwa ukijaribu kumtetea humu, utabebeshwa matusi mpaka basi, muulize Pasco.

Akaja Dr Slaa aliyepewa nickname ya rais wa mioyo ya watu. Alipojaribu kukosoa ubakwaji demokrasia matusi kedekede yamemhusu.

Vipi shujaa Lipumba? Mwenyekiti mwenza UKAWA. Alioga sifa tele toka jf. Sasa anapokea matusi ya kuzidi toka hao hao waliompongeza.

Jf imegeuka kijiwe cha wahuni tu, hakuna la maana

Mkuu Nyenyere uko sawa kabisa. JF kwa kipindi hiki kuelekea uchaguzi baadhi ya members wanashangaza sana. Huwa hata mimi najiuliza,"na hawa members pia wamenunuliwa??"

Ni ajabu sana kuona ukweli unapozungumzwa basi unaonekana hufai. Usizungumze jambo ovu hata kama lipo wazi. Ama kweli ukipenda sana unakuwa kipofu. Na kweli Humphrey Polepole ameongea mambo yasiyo mepesi na hili la 'uchafu' wa viongozi aliweka wazi msimamo wake wiki kadhaa zilizopita pale Kumbukumbu ya Mwl Nyerere akiwa na Mzee Butiku na Mzee Warioba kabla hata CCM haijampitisha mgombea urais wa chama chao.
 
Last edited by a moderator:
Pesa mwana halamu Kama Renatus Mkinga kanyamazishwa sishangai kwa Humphrey Polepole kunyamazishwa ,amewasaliti watz kwa vipande vya fedha.
 
Last edited by a moderator:
Watu wanafiki sana humu JF, hasa jukwaa la siasa! Huyu jamaa alikuwa anafagiliwa sana kabla ya kusema yeye ni sisiemu damu, ila baada ya kujitangaza, wengi wanamuona hafai HATA akiongea UKWELI.
Kama haupendi anachoongea, kwa nini unakuwa na kiherehere cha kutuliza makalio yako kwenye kiti na kumsikiliza? Si u-tune clouds tuu uangalie?
Mi NAMFAGILIA sana Polepole, huwa anadunga watu masindano ya ukweli, HAOGOPI.
Watanzania LAZIMA tujifunze kusikia na kuelewa mambo ambayo hatuyapendi pia!
 
Back
Top Bottom