Zindiko Yanga Na Simba; Watu Wazimi, Mmoja Afa

Zindiko Yanga Na Simba; Watu Wazimi, Mmoja Afa

Mashabiki wa Simba wakiwa wamembeba mwenzao baada ya kuzimia kisa Kiiza kushinda goli la 3 huku timu yao ikiwa haina kitu kipindi cha kwanza.
Na Mwandishi Wetu
Habari zilizotua mezani kwenye House of Media iliyopo maeneo ya Kawe kwenye Jengo la K-Net House floor ya 5 zinaema mzee mmoja maarufu nchini ambae ni shabiki wa timu ya Simba aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Mbande " Kindalindali" amefariki dunia jana maira ya saa kumi na moja na dakika 40 baada timu yake kufungwa magoli 3 bila kipindi cha kwanza.

Akiongea na Xdeejayz mmoja wa majirani wa mzee huyo mkazi wa Kigogo njiapanda ya Tabata Jijini Dar alisema mzee huyo alikuwa nyumbani akitizama mpira huyo pamoja na mwanae wa mwisho uliokuwa unarusha kupitia TBC1 kupitia Azam TV na baada ya mshambuliaji nyota Hamisi Kiiza Diego kuifungia timu yake magoli hayo mawili na kufanya kufikia idadi ya magoli matatu kwa mtungi hadi mapumnziko.
Chanzo cha Xdeejayz kiliendelea kusema kuwa baada ya goli la tatu mzee ghafra alidondoka na kupoteza fahamu na baadae alikimbizwa Hospitali ya Amana na huko ndiko umauti ulikomfika. Hata hivyo mwili marehemu utasafirishwa leo kuelekea kijijini kwao Mang'ura Mkoani Morogoro.

Hata hivyo wakati wa tukio hilo likiendelea timu ya Simba jana ilifuta uteja kwa Yanga baada ya timu hizo kukutana msimu wa mwaka jana na Yanga kubamiza Simba goli 2 kwa bila na jana pia Simba waliponea chupuchupu baada ya kurudisha kwa shida magoli matatu aliyokuwa ameshafungwa na Yanga.

ahhh haiwezekani labda kama alikuwa na matatizo yake binafsi
 
sidhani kama simba walipata shida kurudisha magoli maana timu yangu ya yanga baada ya kushinda tatu, waliondoka kabisa uwanjani wakifikria mipesa waliyoahidiwa, ningekuwa kiongozi ningewakata mishahara wote walioicheza, aibu sana kitendo cha jana

pole kumbe waliahidiwa mapesa?
 
Back
Top Bottom