Zindiko la samaki Mbenga.

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
2,111
Reaction score
3,975
Kuna huyu samaki hatari anayepatikana Afrika. Kwa kiswahili anaitwa Mbenga. Kwa kiingereza Tiger Fish hasa anapatikana kwenye Mto Congo na matawi yake. Hadi ziwa Tanganyika anapatikana sababu ni sehemu ya system ya mto Congo.

Ni samaki lakini ana meno kama ya mamba au wanyama wengine wakali. Pia ana magamba magumu ya kuweza hata kuhimili kuumwa na mamba.


Inadaiwa hakuna zindiko kali kama la samaki huyu. Watu humtumia kufanya mazindiko mawili. Moja la kujilinda, hili hutumia magamba yake magumu. Na lingine la kushambulia, hili hutumia meno yake.

Meno au magamba ya samaki huyu huchomwa kwenye moto. Kisha husagwa na mtu hunywa majivu yake yakiwa yamechanganywa na dawa za mitishamba pamoja na damu.


Wakongo wengi hutumia kinga hii. Inadaiwa mtu aliyetumia meno ya samaki huyu akianza kukushambulia ni ngumu sana kumzuia. Labda uwe ulitumia kinga ya kujilinda ya magamba mengi sana, au ya samaki mkubwa kuliko yule aliyetumia adui anayekushambulia.

Pia magamba hayo huwekwa juu ya milango ya kuingilia ndani. Wachawi na nyoka huwa hawagusi nyumba hizo. Watu wengine huwa wanavaa hirizi zenye vipande vya meno na magamba ya samaki huyu.

Wakazi wengi wanaozunguka ziwa Tanganyika wanafahamu zindiko hili. Mtu huko akimpata Mzenga anakuwa kama amepata dhahabu. Meno na magamba yake yanasoko zuri sana .

 

Attachments

  • Tigerfish-teeth.png
    417.3 KB · Views: 11
Dawa kwa ajili ya maugomvi ya kushambuliana ama kupigana!

Wewe katika maisha yako uliwahi kupigana na wangapi?

Kama ushavuka age ya utoto, mtu mzima kupigana ni nadra sana.

Najiuliza, au kuna cha naana chenye faida zaidi ya kupigana na kumshinda mgomvi wako?
 
Huko Congo waasi wanatumia sana. Na hata raia. Muda wowote unaweza jikuta unatakiwa ujitetee. Pia inasaidia kwa nyoka na wachawi.
 
Huko Congo waasi wanatumia sana. Na hata raia. Muda wowote unaweza jikuta unatakiwa ujitetee. Pia inasaidia kwa nyoka na wachawi.
Hazisaidii kitu ni psychological tu so inakupa confidence ya kupambana. Kuna waasi wanajiita Mai Mai bakata Katanga hawa walikua wanajifukiza matambiko na kwamba risasi haziwapati ila mbona walikua wanadunguliwa tu na walikua wanakufa.

Nadhani ni kumtisha adui na kukupa confidence kupambana ila sio kwamba zinasaidia otherwise kina Mobutu wasingepinduliwa.
 
Niende zangu kigoma sasa nikawahi zindiko, haha.
 
Mazindiko yana miiko yake Sasa usipo fuata miiko linaisha nguvuuuuuuuu

Mfano.. kunawa maji ya moto, kukalia kinu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…