Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mchungaji Paul Sanyangore kutoka Victory World International Ministers amezua gumzo baada ya picha zake akiwa mbele ya umati wa waumini akidai kuwa ana namba ya simu ya mbinguni kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika picha hizo iliyowashangaza wengi mchungaji huyo anaonekana akimuombea mwanamke mmoja na ghafla anaanza kuongea na simu kwa kile alichodai kwamba anapokea maagizo kutoka mbinguni.
"Hello, hapo ni mbinguni? kuna mwanamke hapa, una nini cha kusema kuhusu yeye? Oh.. nimuulize Sibo ni nani ", anaonekana mchungaji huyo akizungumza kwenye simu.
Mchungaji huyo aliendelea mbele zaidi na kile anachodai ni kuzungumza na Mungu na kumueleza mwanamke huyo maagizo aliyopewa na anayodai kuwa ni Mungu.
Mwanzoni mwa mwezi huu mchungaji huyo aliahidi kuziweka hadharani namba hizo za simu anazotumia. Lakini hadi sasa bado hajafanya hivyo. Licha ya kuwa picha hii ilirekodiwa mwezi mwaka huu. Lakini siku ya leo ndio imekuwa ikijadiliwa zaidi mitandaoni nchini Zimbabwe na Afrika Kusini.