ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Hata ukifanya jambo zuri ,wao wananikashifu...wengine wamezoea kusema eh ehh mwisho watachoka...DDC MLIMANI ORCHESTRA-duniani kuna mambo.
 
natafuta huu wimbo

[Sara(Wacha Majivuno) - Urafiki Jazz band ]



Heeee Sara wacha majivuno ee

Usiwe kama Mwanaisha

Kanikataa sababu mimi ni Mshona Viatu eee


Kampata aaa Mshkaji mwingine ehehe hee hee

Mwenye gari kubwa sana mtumba

Kavunja uchumba mwanaisha sababu mimi ni Mshona Viatu ee



(Chorus)



[Wote]

Tamaa yako Mwanaisha, itakuponza,
Kwa kumfuata yule bwana mwenye mtumba,

Mwanaisha ,Mwanaisha, ogopa sana mamaaaa
kazi ni kazi Mwanaisha , bora mkono uende kinywani eeeh

aliye na huu wimbo aniibox tafadhali nimeshautafuta sana
 
osa osa mimi ni nduguyo, usinibague kaka sababu ya pesa, pesa ni matokeo, undugu ni pale pale,
 
Wakuu kuna ule wimbo wa "VIJANA WA SIKU HIZI MARIDADI SANA, CHENI SHINGONI SIGARA MKONONI" mweye nao anirushie au anipe link.
 
Huu wimbo unaitwa "Kuoana." Patrick alimuimbia dada yake baada ya kuolewa. Patrick ni marehem kwa sasa. Muziki wa Tanzania ni mzuri sana ila radio zetu za kijinga ndizo zinajitahidi kuua muziki wetu lakini hawawezi kwani wapenzi tuko wengi.
mkuu siku hizi hakuna watangazaji bali kuna ma dj
 
Mimi sielewi nifanye nini
Ooh mama pili eeh
Mapenzi ya safari yamenichosha
Leo mimi kesho yule sitaweza
Pili eeeh pili mtoto wa Tanzania
Pili we mswahili ujanja mingi
Usiku na muchana mi nakutafuta
Ninauliza upo wapi? magomeni mapipa mapipa(chang'ombe)
Unieleze mama yoooh
Pili eeh mbona mi sikuelewi
Pili sema ukweli wako amua wewe
Pili muswahili
Usiku na muchana nakutafuta sikuoni
Pili sema ukweli wako amua wewe
Pili nasema mpenzi nielewe unieleze nipate kujua
Mapenzi gani imekuwa kampuni
Unieleze wapenda wangapi waleta aibu kwa wazazi wako
Umenitoa thamani ya kukupenda aaah.
Hiyo ilikuwa moja one na mzee mzima morenoooo
 
Oooh matilda tulia mama hebu nisikie
Mama matilda sasa hebu tulia umlee mtoto wako
Matilda mama
Mama matilda nakuomba nisikie punguza nyendo za usiku na mchana mamaaa
Kumuacha mwana peke yake anatafuta wapi ***** hayupo
Na siku nyingine ukalale huko huko huna imani matilda utauwa
Matilda mtunze mwanao mama uhuni kwako hauna faida matilda utauwa
Furaha hazina mwisho matilda utauwa.
 
Wadau ebu nikumbusheni huu wimbo kaimba nani ingawa chorus yake siikumbuki vizuri ila unavoanza kuna mwanamama anaimba anasema "Nimeshitushwa na ujumbe ulionitumiaa................ Umesema kwamba hama zako hama zangu............" halafu kuna jamaa nae anaitikia kat kat ya wimbo anasema "Shogaa eeeeh jeuri hiyo mimi sinaaa........................ Ukiniudhi utanionea" Siukumbi vizuri ila izo sehemu nilizozitaja zimeimbwa kwenye huo wimbo! Waloimba wanaitwaje au kama kuna mtu anao atupie link hapa.
 
Wadau ebu nikumbusheni huu wimbo kaimba nani ingawa chorus yake siikumbuki vizuri ila unavoanza kuna mwanamama anaimba anasema "Nimeshitushwa na ujumbe ulionitumiaa................ Umesema kwamba hama zako hama zangu............" halafu kuna jamaa nae anaitikia kat kat ya wimbo anasema "Shogaa eeeeh jeuri hiyo mimi sinaaa........................ Ukiniudhi utanionea" Siukumbi vizuri ila izo sehemu nilizozitaja zimeimbwa kwenye huo wimbo! Waloimba wanaitwaje au kama kuna mtu anao atupie link hapa.
Ni shoga wa Fina Mango kama sijakosea
 
Kijogoro sina nyumba ee, ntajenga ndani kwa ndani, ntajenga nyumba ya mawe ee, ghorofa ndani kwa ndani, sijaona manowari ee. Ikipita barabarani
 
Kuna kitu kinaitwa, "Kisa cha foto albam"
Kisa ni picha iliyopigwa zamani eeh katikati ya Dar es alaam eeh
Kisa ni picha iliyopigwa zamani ee
Katikati ya mji wa mwanza ee
Sheli Zinuna nakupa pole Zinuna ee.
2. Kupatwa kwa mwezi sio kiama- mwenge jazz.
3. Kata ya maji ukweni- sinahakika na bend ila nadhini bima Lee, muimba Maxmilian Bushoke.
Makumbele- maguezi du Zaire
Kaweke zege mbinguni- Bima lee
5. Ayoyo mie- Sammangwana.
6. Machawi na mulozi- Rwambo Mackiady & Sammangwana.
Ukatiri, ndoa ya mateso, namsaka mbaya wangu- Marjani Rajabu.
7. Tucheze ngoma za kwetu, masafa marefu, mapenzi gani haya, Mama- Tancurt Almas.
Nyabasi, Nimesimama kwenye kona, Asha mwana Seph, Huwezi kula muwa bila kukuta vundo, kulithi ndoa ya kaka- Juwata.
Nishike mkono, kibela acha chuki, sema ukweli wako- Mk group.
Nyimbo ziko nyingi. Ila leo niishie hapa, zamani watu walikula uhondo sana. Kipindi hicho nilikua napenda kufuatilia mziki sana ila uwezo wa kupata pesa ya kiingilio sikuwa nao nilijiunga nawenzangu kuchenza nje ya ukumbi, mpaka fungulia mbwa ndopo tunaingia ndani. Pale 82 hoteli sasa hivi San siro, pamoja bend zingine kupiga pale, ulikuwa ukumbi wa nyumbani wa washirika Tanzania stars. UFI Clabu, ulikuwa ukumbi wa nyumbani wa Bima Lee, Lion Hoteli, ulikua ukumbi wa nyumbani wa Mk beets, bend ndugu na MK group, watoto wa magorofani ukumbi wa nyumbani ni Africa hotel ghorofa la saba.
Sikinde wakati wanaitwa mrimani park, ukumbi wa nyumbani ulikua kule mlimani chuo kikuu, baada ya kumilikiwa na shirika la maendelea Dar es allam wakaitwa DDC mlimani park ukumbi wa nyumani ikawa DDC Kariakoo. JUWATA ukumbi wa nyumbani ulikua CCM Mwimjuma Mwananyala, ulikua unanunua gazeti la mfanyakazi unapata ratiba za bend, sinema kulikua na kumbi nane za sinema Dar. Ila kwenye mziki ukisikia saxs phone zikipigwa chama chetu za mapinduzi cha jenga nchi, jua mziki umefungwa. Ila kwa haya niliyoaandika kama kuna mwenye kumbukumbu sahihi anaweza weka sawa.
 
mwenye wimbo wa UDA JAZZ unaitwa "TULELE TUBOWE" Umetungwa na kuimbwa na Mikidadi Seif kwa lugha ya Kimwera anisaidie
 
mwenye wimbo wa UDA JAZZ unaitwa "TULELE TUBOWE" Umetungwa na kuimbwa na Mikidadi Seif kwa lugha ya Kimwera anisaidie
Huyu muimbaji wa wimbo huu nilionyeshwa, yupo kule Nachingwea, maisha yake ya sasa hayaenda na maisha mwanamuziki alikua bend maarufu kama ufafiki. Ila hata mzee Juma Mrisho nilimuona kipindi urafiki imekufa yeye akabaki kama meneja wa jumba la maendeleo urafiki, ukweli ni shida.
 
Back
Top Bottom