Zile dakika5 baada ya kuibiwa kitu cha thamani

Zile dakika5 baada ya kuibiwa kitu cha thamani

Nilimkaribisha gheto classmate wangu wa primary school ambae alifukuzwa kwa dada yake akaomba hifadhi kwangu kwa siku tatu akaishia kukaa miezi 3.

Jamaa nilikuwa nampa chakula na malazi kila kitu hataki kazi. Nilipomsihi afanye mpango wa kazi au kutafuta chumba akona isiwe tabu akasafisha gheto kila kitu kuanzia boxer, notebook(sio computer ni kitabu) hadi malapa ya kuogea.

Nilikuwa nalala kwenye biashara zangu, ile narudi gheto kubadili nguo nakuta kweupe kaacha fridge, kitanda na godoro tu. Mziki na vitu vingine muhimu vya ndani na vya biashara kasomba vyote.

Nilipiga magoti na kumuombea msamaha kwa Mungu. Tangu siku hiyo maisha yake kama nilimlaani bora ningemuombea mabaya.
Aisee laana itamtafuna milele hiyoo...!!
 
Uzuri wa JF hakuna anayekuona. Nitadanganya wapi na hapa mpo wa kuwadanganya.

Itaendelea.
 
Sio ungeninunulia nyingine we Putin wewe huna maana kabisa
Hahahaaa,ningekuwa na ww wasingeiba,maana wangeiba nikiwa na ww ningeonyesha udhaifu,na nisingekubali udhaifu,yaani ningenunua fasta
 
Niliwahi kuibiwa gari aina ya range rover mpya ya siku mbili toka ninunue,

Jamani nahisi roho inanisuta..jamani ni uongo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we fa.la umenifanya niangue kicheko usiku huu
 
Me nilikwapuliwa iphone x kwenye folen
Tulikaa muda mrefu kwenye folen tukaichoka ac ile kusema tufungue vioo tupate hewa safi
Sm ikaita nikaitoa ili nipokee wajanja wakapita nayo
 
Tulikua tunafanya Mitihani pale UDBS sasa nikampa mshikaji wangu aniwekee Tab yangu ya samsung 10.1 kwenye begi lake mi nikawa wa kwanza kumaliza mtihani na kisha nikatoka kuwahi kwenda cafe ili nipate breakfast kabla ya mtihani unaofuata ....sasa huku nyuma kumbe mshikaji nae alivyotoka akajua bag nimelichukua mimi hivyo nae akaenda zake bila kuangalia bag lake... wakati tunarudi kwenye paper inayofuata nilimwuliza tab iko wapi nipige brash kidogo maana nondo zangu zote zilikuaga softcopy....hapo kimbembe ndio kilianza...baada ya kugundua wote bag hatuna tulianza kulitafuta... Bag tulilipata ndani mlikua na tecno j8 tu ile Tab yangu sikuwahi kuiona tena toka ile siku, hakika sidanganyi ule mtihani unaofuata niliingia sielewi hata nnacho kifanya akili ilikua inawaza kwann yamenikuta.....huyu alieiba najua yupo Huku JF ile siku pale UDBS ungesearch vizuri mfuko unaofuata kulikua na tecno J8....ila siku yako ipo tu popote ulipo sasaivi!
 
Aisee mimi niliuziwa sabuni, nilijiona fala sana.
 
Back
Top Bottom