Zijue Tips za kubaki salama ili usiibiwe pale unapo nunua bidhaa mtandaoni

mwanajamii26

Member
Dec 16, 2014
58
13
Wengi wetu tumekuwa tukinunua bidhaa kupitia mitandao bila kujua kuwa tunaweza kuingia kwenye hatari ya kuibiwa.kuna mitandao mingi sana inayotoa huduma ya kuuza na kununua bidhaa mtandaoni mfano kwa hapa Tanzania tuna Kaymu na jumia. .
Sasa hapa nimekuwekea tips za kuweza kutambua kama mtandao unaotaka kuutumia kununua bidhaa ni salama au la.
=======

Bila shaka wewe si mgeni wa kusikia neno kununua bidhaa kupitia mtandaoni. katika karne ya sasa kumekuwa na mitandao mingi sana inayojihusisha na kuuza bidhaa. mfano wa mitandao hiyo ni AMAZON,KAYMU na JUMIA. Lakini swali linalokuja hapa ni je kuna usalama kiasi gani kupitia hiyo mitandao kwa wateja wanao nunua hizo bidhaa.
kiukweli hakuna anayejua juu ya hili. sasa hapa nitakupa Tips ambazo zitakuwezesha kubaki salama pale unapo nunua bidhaa kupitia mtandao na pia kuweza kutambua mitanado ambayo ni salama kwa kununua bidhaa mtandaoni
Mambo haya ni haya yafuatayo.

ANGALIA KAMA MALIPO YANAFANYIKA KWA NJIA SALAMA
hakikisha mtandao unaotumia kununua bidhaa unakupa option ya wewe kuwa na account, lakini pia wakati unafanya manunuzi ukifika katika kipengele cha kuingiza user ID/ password, social security number au credit card details basi hakikisha link yako inaanza na “https” badala ya “http”
kumbuka http ni kifupisho cha Hypertext Transfer Protocol wakati ile s husimama kama secure.hivyo wakati wa kujaza taarifa zako za user ID/ password, social security number au credit card details link inatakiwa ianze na https hii hufanya taarifa zako kuwa katika hali ya usalama hivyo endapo link itaanza na http inamaanisha taarifa zako hazipo kwenye usalama na hivyo wezi wa mitandao wanaweza kuzipata.
hii ina maanisha kuwa mtandao huo unaotumia kununua bidhaa sio salama na achana nao

ANGALIA KAMA MTANDAO UNATOA OPTION YA CASH DELIVERY
Hakikisha mtandao unaotumia kununua bidhaa unatoa option ya Cash on Delivery hii itakusaidia wewe kuamua kulipia bidhaa kupitia Cash on Delivery badala ya kulipa kwa kupitia online. sasa endapo mtandao unaotumia hauna option hii basi kuwa na mashaka nao

ANGALIA MAONI YA WATEJA WENZIO HASA JUU YA BIDHAA UNAYOTAKA KUNUNUA
Hakikisha kabla hujafanya manunuzi na kufanya malipo unaangalia maoni ya wateja ambao tayari walishafanya manunuzi juu ya bidhaa husika, hii itakusaidia kupata uhakika juu ya mtandao kuwa ni salama na pia itakusaidia kujua uimara wa bidhaa unayotaka kununua.

ANGALIA WARRANT, GUARANTEE NA RETURN POLICIES
Unatakiwa kuhakikisha mtandao unaotoa huduma ya kuuza bidhaa una warranty, guarantee and return policies. na unatakiwa uzisome na kuzielewa hizi read the websites return policy, their guarantee / warranty terms.. hii ni kwasababu kuna uwezekano mkubwa wakati unaagiza bidhaaukaletewa bidhaa ambayo ni mbovu au sio sao. sasa kama website haina return policy ina maana huna uwezo wa kurudisha hiyo bidhaa na hivyo mtandao huo si salama.

Chanzo: Mwanajamii
 
Back
Top Bottom