Zijue passports zenye nguvu duniani

Zijue passports zenye nguvu duniani

bendee

Senior Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
111
Reaction score
147
Habarini wakuu.
Niende mojakwamoja kwenye mada kama kinavyo eleza kichwa cha habari.
Pasi za kusafiria (PASSPORTS) inatambulika kama ufunguo wa kuingilia nchi yeyote duniani.
Na ili passport ihesabiwe kwamba inanguvu duniani lazima iwe na sifa tatu (3). Nazo nikamaifatavyo.

(1) VISA FREE SCORE ( hii ni ruhusa iliopo kati ya nchi na nchi kuruhusu raia wake kuingia baina ya nchi hizo bila ya haja ya kuomba viza (VISA). Mfano kutoka Tanzania bara kwenda Zanzibar, pale kuna viza free. Zamani watu kutoka Tanzania bara waliingia Zanzibar kwa viza( kwa sasa iliondolewa). Povu ruhsa kwa Hilo.

(2) sifa ya pili inayoifanya passport iwe na nguvu duniani ni VISA ON ARRIVAL. Yaani unagongewa viza pindi unapowasili nchi husika. Hii huhitaji kuomba viza ubalozini. Mfano tunaposafiri kwenda Kenya, Uganda Rwanda, Congo n.k, huwa hatuhitaji kwenda kwenye balozi zao kuomba viza. Bali tunapowasili mpakani au kwenye viwanja vya ndege tunagongewa viza pale pale na maafisa uhamiaji. Ila hii inauma sana hii kutokana na ubinafsi wa viongozi nchini mwetu kuwa wabinafsi utaona kuna nchi duniani wao kuja kwetu Tanzania wanagongewa VISA ON ARRIVAL lkn sisi kwenda kwao lazima tuombe viza halafu kupata sio lazima. Tujazishwe mifomu chungu nzima as if tunataka kwenda kufanya utapeli nchini mwa watu.
Zamani tulikuwa na VISA ON ARRIVAL ya kuingia Wingereza kwa malkia lkn viongozi wetu walipo ona vijana wanaondoka kwenda nakufanikisha maisha na hatimae kuishi kama malaika wakaiomba serekali ya malkia iwaondolee raia wa Tanzania VISA ON ARRIVAL, hapa lengo ilikuwa niwatu wasiweze kwenda wingereza lkn wabakie hapahapa Tanzania ili waishi kama mashetani!! (Povu ruhsa).

(3) sifa ya tatu ni kutoka United Nations Development Programme Human Development Index 2015 (UNDP HDI) is used as a tie breaker. The UNDP HDI is a significant measure on the country’s perception abroad. Yaani kwa mujibu wa taarifa zenu zinavyo tolewa na shirika hilo ndio na nyie munavyochukuliwa mulivyo. Na hapa ndio kuna haja kubwa kabisa ya serekali yangu tukufu ya SMZ kujitathmini sana katika kutoa vibali vya meli duniani. Kuna minchi inakuja kukata leseni za meli Zanzibar ili tuu waweze kuweka bendera ya Tanzania kwenye meli zao halafu kifatacho nikufanya madudu kibao wakiwa wameweka bendera ya Tanzania. Then nchi inapata sifa mbaya kwenye mashirika ya umoja wa mataifa. Wazungu wana msemo wao wansema what goes around comes around! Tujitafakari kwa Hilo.


Utagundua katika hizo sifa zinazoifanya PASSPORT itambuliwe kuwa strong duniani Electronic PASSPORT haimo!. Povu ruhsa.
Nchi zinazoongoza kuwa na strong PASSPORTS ni Singapore na south Korea.
Na nchi zenye weak PASSPORTS ni Afghanistan, yenye nchi 26 tuu ambazo ni viza free au VISA ON ARRIVAL.
Tanzania ipo nafasi ya 64.
81992aa55a4b90844a3941f7075759dd.jpg
1c8f502d2111ea2b40c6b9f1ae69b6f7.jpg
5df372427ce01d20df7efba585a25097.jpg
971818020a1baec5cbb49736a66649a0.jpg
c59b6093c2ea172a5e63ae83f63c0c63.jpg
8879f23f53bb65ea830c14c921d33d7e.jpg
 
Back
Top Bottom