Zijue namba za magari ya Tanzania! Pamoja na namba maalum za magari ya viongozi, Serikali na Taasisi za Umma kwa ujumla

Kuna uzi humu utafute lakini kukusaidia
SU=Shirika la Umma a.k.a Soma ule.
STL=Serikali ya Tanzania mwendelezo wa STK
SM=Serikali za Mitaa.
MT=Magereza Tanzania.

SLS - Shirika la serikali(Zanzibar)
PT - Polisi Tanzania
JW - Jeshi la wananchi
RAB - Shirika la reli
 
ST # A ni magari ya Ikulu
PT ni Police Tanzania na si TP kama ulivyoainisha
DFP ni Donor Funded Project hii ni badala ya TX
SU ni Shirika la Umma
STA,...STG,STH,STK, STJ,...,STZ ni magari ya Idara nyingine za serikali pamoja na wizara
WN (abc) ni waziri wa nchi
W (abc) ni waziri
S ni Spika
NS ni Naibu Spika
JM ni Jaji mkuu
CAG ni Chief Auditor General

Ongeza na hii CS- chief secretary
 
Lakini mbona naona STJ nyingi zinatumika na polisi, na STK zinatumika na wengine (especially wizara)?

Pia Sijawahi kuona wala kusikia STB wala STC. Ila ST zipo....na STA sio STA, mara nyingi huwa ST halafu namba, halafu mishwo ndio A.

Naweza kuelewa kuwa ST = Serikali Tanzania ila hizo herufi bado. Naomba mawazo zaidi, kwa wanaofahamu zaidi.

ST... A ni namba ya Serikali ya Tanzania mahsusi kwa State House.
 
Back
Top Bottom