Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
JACKA Resources Limited ni kampuni ya Australia ambayo imeandikishwa pia kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX: JKA) ikijihusisha na utafiti wa mafuta na gesi ikiwa imewekeza kwenye nchi za Australia, Tunisia, Nigeria, Tanzania na Somalia.
Kwa ujumla, kampuni hii imelenga uwekezaji katika Bara la Afrika na katika uwekezaji huo mpaka sasa inajivunia kusimamia rasilimali za mafuta zenye akiba ya mapipa takriban milioni 133 ambayo yamethibitishwa katika maeneo husika.
Nchini Tanzania, Jacka Resources inamiliki asilimia 100 katika kitalu cha Ruhuhu mkoani Ruvuma ambako inatafiti mafuta, lakini huko Tunisia inamilikia asilimia 15 katika Kitalu cha Bargou na nchini Nigeria inamiliki asilimia 5 katika Kitalu cha Aje Fields (OML113).
Kwa habari zaidi, soma hapa=> Zijue kampuni zilizowekeza katika mafuta na gesi Tanzania (15) – Jacka Resources Limited | Fikra Pevu