Zijue dalili 4 za mpenzi mkorofi

Zijue dalili 4 za mpenzi mkorofi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
HATABIRIKI
Siyo watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu ana furaha na kuonesha mapenzi, mara ghafla anakasirika na kutaka kuadhibu mtu.

MKATILI
Ni wenye tabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatajali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.

LAWAMA
Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayo yapata, Mfano anapo kosa kazi, anapo-shindwa shuleni. Kila kitu ni kosa la mtu mwingine na siyo yeye.

WIVU
Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa siyo kwamba anataka muda huo awe na wewe.
 
Sifa yangu ni ya kwanza... Na imenisaidia sana
 
Asee demu wangu nmemuacha jana kwa the same reasons. Mtoto mzur kichiz lakini furaha ndani hakuna. Imebidi nipige moyo konde tu nimpige chini.
 
SITABIRIKI hiyo ndiyo sifa yangu ya ulazima
 
Mi sina izo sifa ila nimekuja kugundua ukiwa huna izo sofa mapenzi huyawezi,... Watakuchapia wenye izo sifa, ao ndo wanawake
 
Back
Top Bottom