Zifahamu sheria zako za msingi ukikutana polisi

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,685
ZIFAHAM SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI

IMEANDALIWA NA MAWAKILI.
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAM HAKI ZAO.
 
Ahsante kwa kutushirikisha elimu muhimu mkuu. Tatizo askari wengi hayo mambo waliyaacha walipomaliza mafunzo chuo.
Sasa hivi wanafanya kazi kwa maagizo na kiburi, utapigwa, utabambikwa kesi, utadhalilishwa hata kama hauna kosa. Kinachokuokoa inakua ni ile kusoma mazingira na kuongea nao ili kujinusuru, wengi hawafuati taratibu na sheria.
 
Hii heading haijakaa poa. Ilitakiwa iwe "ZIFAHAM SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI WA UK". UK ina maana United Kingdom, sio Ukonga!

Kwa huku Africa labda polisi wa South Africa ambako wanaitwa SAPS -South African Police Service na huko kuna taasisi ya kuchunguza makosa yanayofanywa na polisi(Independent Police Investigative Directorate-IPID). Kwa taarifa tu, polisi wetu wanaitwa 'Tanzania Police Force', ndiyo maana wanasema tii sheria bila shuruti. Hapo wanamaanisha tii amri bila shuruti.
 
Hizi haki zangu mbele ya Jeshi la Polisi nitaziweka kwenye friji ili kuzitunza mpaka pale watakapoacha kuvaa magwanda na kuanza kuvaa shati na tai, kwa sasa nitatii sheria bila shuruti.:D
 
Hii heading haijakaa poa. Ilitakiwa iwe "ZIFAHAM SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI WA UK". UK ina maana United Kingdom, sio Ukonga!

Kwa huku Africa labda polisi wa South Africa ambako wanaitwa SAPS -South African Police Service na huko kuna taasisi ya kuchunguza makosa yanayofanywa na polisi(Independent Police Investigative Directorate-IPID). Kwa taarifa tu, polisi wetu wanaitwa 'Tanzania Police Force', ndiyo maana wanasema tii sheria bila shuruti. Hapo wanamaanisha tii amri bila shuruti.
Ni kweli mkuu, hiyo tii sheria inamhusu raia tu, mbona wasiseme "tutii sheria" na wao iwahusu
 
Vitu vingine hivi havina maana ,wale raia waliopigwa juzi Geita na Polisi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ,haya uliyoandika hapa walikuwa hawajui ?
 
Jeshi la Polisi litabadilika ikiwa sisi watanzania kama jamii tutastaarabika. Imagine askari anampiga virungu vya hatari raia na mwandishi anayetaka kumsikiliza Lowassa kama ilivyotokea Geita. Mambo ambayo raia wanamwambia Lowassa hata polisi yanawagusa maana bado wapo wengi wanaishi nyumba full suti ya bati au mbao, lakin unashangaa wanapata wapi ujasiri wa kuwapiga wananchi virungu wakati hawafanyi fujo yoyote.

Lowassa sio wa kukamatwa na vijana wadogo. Kwa kura milioni 6, anastahili kupigiwa simu na OCD au RPC na kuambiwa aende kituoni bila ambush za polisi. Lakini kwasababu bado tupo stone age kiustaarabu, wacha tupigane virungu tu.
 
Back
Top Bottom