Zifahamu aina za upendo

Zifahamu aina za upendo

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,873
[emoji2389] AGAPE ( unconditional love)

[emoji771] Ni Upendo usiokuwa na maharti, Upendo wa kujitolea usio na ubinafsi.
[emoji771]️Ni Aina ya upendo wa kiroho. Wakristo tunaamini kuwa Yesu alionyesha aina hii ya upendo kwa wandamu wote. Alijitoa mhanga yeye ili tuweze kupata ondoleo la dhambi zetu, aliteswa kwa ajili ya furaha yetu .
Soma ( Yohane 3:16)

[emoji2390].EROS (Romantic love)

Eros-. Ni jina la mungu wa kigiriki wa upendo na uzazi.
[emoji771]️Upendo huu huhusishwa na tamaa ya mapenzi ya kimwili. Ni aina Upendo wa shauku na hamu ya kingono.
Katika Biblia aina hii ya upendo ilionyeshwa na Amnoni alipofanya mapenzi na Dada yake Tamari. (Soma 2 Samweli 13) Aina hii ya upendo imeonyeshwa pia na Ibrahim, Yakobo, Daudi Pamoja na Suleman kwa idadi ya wanawake wengi waliokuwa nao tofauti na mpango wa MUNGU.

[emoji2391] PHILIA. (Affectionate love)

[emoji771]️ Ni aina ya upendo wa kirafiki. Wagiriki akiwemo Plato waliamini kuwa Aina hii ya upendo huwa haina mvutano wa shauku ya kimwili Kama ilivyo kwa Romantic love (eros).

[emoji771]️Aina hii ya upendo imeonyeshwa kupitia urafiki wa Yonathan na Daudi, Biblia Inasema Yonathan alimpenda Daudi Kama anavyoipenda Roho yake mwenyewe.
Soma kisa Cha urafiki wao (1 Samweli 18- 20) Natumai utajifunza mengi kupitia urafiki wao.

[emoji2392]Philautia. (Self-love)

[emoji771]️Ni aina ya upendo wa kujipenda . Katika jamii zetu siku hizi watu wengi wanashiriki Aina hii ya upendo Katika kujipenda na kuwa wabinafsi
[emoji771]️Kujipenda si vibaya lakini ni muhimu tujifunze kutoa na kupokea upendo Kutoka kwa watu wengine. Kile ambacho hatupendi kufanyiwa tujifunze kutowafanyia watu wengine pia.
[emoji771]️ Katika Biblia Aina hii ya upendo ilionyeshwa na Yakobo alipotaka haki ya uzaliwa wa kwanza Kutoka kwa kaka yake ili ampatie chakula, lakini pia alipochukua Baraka za kaka yake.
Soma (Mwanzo 25:27-34) pamoja na
(Mwanzo 27)

[emoji2393]. STORGE (Familiar love)

[emoji771]️Ni aina ya upendo wa kindugu au familia ambao huonekana ni upendo wa kawaida. Mfano upendo wa Mama kwa Mtoto. Aina hii ya upendo huwa ni Aina ya upendo wa kujuana baina ya mtu na watu.

Katika Biblia Aina hii ya upendo ilionyeshwa na Upendo wa Yusufu kwa ndugu zake.
( Soma Mwanzo 45: 1-13)

[emoji2394] PRAGMA (upendo wa kudumu)

[emoji771]️ Ni Aina ya upendo ambao msingi wake umejengwa Katika kuaminiana Tofauti na Eros (romantic love) ambao upendo wake huwa ni washauku ya kingono.
Pragma ni Aina ya upendo ambao umekomaa na kukuzwa kwa mda mrefu sana (Upendo wenye uvumilivu).
Katika Biblia Aina hii ya upendo ilionyeshwa na Yakobo alipomtumikia Laban miaka Saba ili ampate Raheli
(Soma Mwanzo 29: 15-30)
[emoji771]️Kwa bahati mbaya aina hii ya upendo ni nadra Sana kupatikana katika jamii kwa maisha ya leo..
[emoji771]️Siku hizi vijana hawana mpango wa uvumilivu wa kuutazama upendo Katika hali ya kukua bila kuwa na romantic Love....
[emoji771]️Ndoo Maana Neno la MUNGU likatukumbusha kwa kutuambia
"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, .. Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe"
( Wimbo ulio bora 2:7)

[emoji2395] MANIA (Upendo wa kuzingatia)

[emoji771]️Ni Aina ya upendo wa kimapenzi ambao unaweza sababisha mtu kuwa na wazimu,
msongo wa mawazo, wivu, au hata hasira.
[emoji771]️Upendo huu hutokea baada kukosekana kwa usawa kati ya romantic love na pragma love.
[emoji771]️Watu wengi wanaopata aina hii ya upendo wa kimapenzi huwa wanakabiliwa na hali ya wazimu, wivu na hata hasira ya kuhisi kusalitiwa na wapendwa wao.
[emoji771]️Wanaogopa kupoteza kile ambacho wamekipenda. Hofu hii ya kupoteza huwafanya wafanye maamuzi magumu na yenye Hatari zaidi kwa kile kinachoitwa wivu wa mapenzi.

Aina hii ya upendo katika Biblia ilionyeshwa na Amnoni kwa dada yake Tamari alivyompenda kiasi Cha kuugua
( soma 1 Samweli 13).
 
Back
Top Bottom