Elineema J Mosi
JF-Expert Member
- May 17, 2013
- 808
- 148
WAKATI utawala wa Rais Jakaya Kikwete ukiwa umebakiwa na takriban mwaka mmoja kamili kabla ya kumalizika, yayumkinika kuhitimisha kuwa moja ya kumbukumbu muhimu atakazotuachia ni wingi wa safari zake nje ya nchi, hususan huko Marekani.
Mfano rahisi ni wa hivi karibuni kwamba Rais Kikwete alizuru nchi hiyo Agosti ambapo pamoja na mambo mengine alihudhuria Mkutano wa Marekani na Afrika, kisha baadaye kwenda tena nchini humo kwa wiki mbili mwezi uliopita. Katika ziara hiyo (ya mwezi uliopita), Rais alipata fursa ya kuzuru hapa Uingereza kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership, kabla ya kurejea tena nchini Marekani.
Japo ni wazi kuwa baadhi ya ziara hizo haziepukiki, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba Rais wetu anasafiri mno kwenda nje ya nchi. Na licha ya ukweli kwamba Rais Kikwete ni muumini wa dhana ya ‘open government' inayohamasisha wananchi kufahamishwa masuala mbalimbali yanayoihusu serikali yao, mara nyingi hatufahamishwi waliomo kwenye misafara ya Rais kuja huku ughaibuni. Kwa hiyo ni vigumu hata kukadiria gharama za safari hizo kwani hatujui Rais kaambatana na watu wangapi.
Ziara yake ya mwezi uliopita nchini Marekani imeibua mambo makuu mawili. Kwanza, binafsi sikuwahi kufahamu kuwa tuna mabalozi kadhaa wa heshima nchini Marekani. Hilo nimelifahamu baada ya kuona picha ya Rais akiwa na baadhi ya mabalozi hao wa heshima. Suala hilo limenifanya nijiulize maswali kadhaa. Kwa mfano, pamoja na kutambua ukubwa wa nchi hiyo, lakini kwa nini tuhitaji mabalozi kadhaa wa heshima ilhali tuna balozi wetu kamili nchini humo? Na kama suala ni ukubwa na umuhimu wa nchi hiyo, vipi kuhusu kuwa na mabalozi kadhaa wa heshima China au hapa Uingereza?
Lakini katika hilo hilo, kama tuna wawakilishi kadhaa nchini Marekani, kwa nini basi kuna haja ya safari nyingi za Rais kwenda nchi hiyo? Kadhalika, tukirejea kwenye dhana ya ‘open government,' mabalozi hao wa heshima wanapatikanaje? Na pengine kubwa zaidi, gharama za ubalozi wao wa heshima ni kiasi gani? Na kwa nini nafasi hiyo isikabidhiwe kwa Watanzania wanaoishi huko au waliochukua uraia wa huko maana hawa wanaijua vyema nchi yetu na pengine wana uzalendo zaidi ya hao ‘wageni' tunaoowajiri kutuwakilisha.
Pili, mmoja wa mabalozi hao wa heshima, ametajwa kuwa ni mmiliki wa kampuni inayotarajiwa kuleta treni za kisasa kwa ajili ya usafiri kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na ‘katikati ya mji' (city centre) Dar es Salaam. Lakini kabla ya taarifa hizo, balozi huyo wa heshima alionekana katika picha moja akimkabidhi Rais Kikwete zawadi ya saa. Sasa katika mazingira ya kawaida tu, mtu aliyeonekana akimpa zawadi Rais, kisha akapatiwa fursa ya uwekezaji ‘chapuchapu,' yaweza kuzua tashwishwi ya aina fulani.
Kuna maswali mengi ya msingi kuhusu balozi huyo wa heshima na mradi huo kwa ujumla. Kwanza, taarifa za kuhusu kampuni itakayoleta treni hizo imezua utata mkubwa. Wakati baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa kampuni hiyo inaitwa Shumake Rails, taarifa nyingine zimeitaja kampuni hiyo kuwa ni ‘m/s shumoja.' Je, yawezekana kuwa kampuni hiyo ina majina mawili?
Lakini kinachotia wasiwasi zaidi ni ukweli kwamba wakati kuna tovuti ya shumoja.comExternal Links icon
ya kampuni inayojihusisha na masuala ya usafiri wa reli, hakuna tovuti yoyote ya kampuni ya Shumake Rails. Na hata ukiangalia tovuti ya ‘shumoja,' licha ya kutokuwa na taarifa zozote kuhusu, kwa mfano historia yake katika miradi ya usafiri wa reli, imesajiliwa mwezi uliopita tu, kitu kinachoweza kuzua maswali iwapo kampuni hiyo ni ‘kubwa' kumudu mradi huo unaotajwa kuwa na thamani ya mabilioni ya shilingi.
Utata mwingine ni jinsi mradi huo unavyoharakishwa. Katika maelezo yake, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ametaka wahusika waharakishe taratibu za mradi huo ili uweze kuanza mapema iwezekanavyo. Naye mmiliki wa kampuni huyo amedai kuwa ‘yupo tayari kuanza maradi huo hata leo.'
Uharaka huu ilhali kuna maswali kadhaa niliyokwishatanabaisha awali unaweza kuzua skandali kama ya Richmond. Kwa wenye uelewa wa masuala ya usalama wa taifa, kila uwanja wa ndege ni kitu kinachoitwa ‘kituo muhimu' (vital installation) na licha ya manufaa yanayotarajiwa, kuharakisha mradi huo kunaweza kutofanikisha uchunguzi wa kiusalama (vetting) kwa ufanisi.
Lakini kingine cha kushangaza ni ukweli kwamba mmiliki wa kampuni hiyo ameonyesha michoro ya jinsi mradi huo utakavyofanya kazi. Je, yawezekana maandalizi ya mradi huo yamekuwa yakiendelea kinyemela? Nauliza hivyo kwa sababu pamoja na maendeleo ya teknolojia, mwekezaji kutoka Marekani angelazimika kuwepo huko nyumbani kabla ya kuandaa michoro hiyo ‘iliyoonekana ghafla' siku ya utiaji mkataba wa awali.
Jingine, ninaomba wewe msomaji ulifanyie kazi. Nenda kwenye tovuti ya kutafuta habari (search engine) kama google.com kisha ingiza jina la balozi huyo wa heshima ushuhudie taarifa mbalimbali zinazotia wasiwasi sio tu katika uwekezaji katika mradi huo bali hata huo ubalozi wake wa heshima. Nisingependa kutoa hukumu bali nakuachia jukumu hilo wewe msomaji kisha ufikie hitimisho iwapo mwekezaji huyo ni anastahili au la.
Katika hafla ya kusanini ‘mkataba wa awali,' Waziri Mwakyembe amemshukuru Rais Kikwete kwa kusafisha njia ya kupata wawekezaji, ikiwa pamoja na huyo wa mradi wa treni ya kisasa. Lakini tukiweka kando picha inayomwonyesha Rais akikabidhiwa zawadi ya saa na mwekezaji huo, kuna picha mtandaoni zinazomwonyesha Waziri Mwakyembe na mwekezaji huyo wakati ya ziara ya waziri huyo nchini Marekani Septemba, mwaka jana. Pengine ili kuondoa wasiwasi unaoelekea kuligubika suala hili, ingekuwa vema iwapo serikali ikiweka bayana undani halisi wa mradi huo, kwa mfano wazo hilo la uwekezaji lilianza vipi hasa.
Naomba ieleweke kuwa sipingi uwekezaji huko nyumbani lakini ninaamini kuwa ‘tumeshaumwa na nyoka' mara kadhaa huko nyuma kutokana na ukosefu wa umakini wa baadhi ya watendaji wa serikali au pengine kutokana na ufisadi na ni muhimu kila mkataba unaosainiwa uambatane na uwazi wa kutosha.
Katika maelezo yanayohusiana na mradi huo sijaona sehemu yoyote inayotaja uwepo wa zabuni iliyopelekea mwekezaji huyo kukabidhiwa mradi husika. Kadhalika, sijaona sehemu yoyote inayoeleza uzoefu wa mwekezaji huyo katika mradi wa aina hiyo. Kadhalika, wasifu wake kwenye mtandao wa kijamii wa LinkedIn hautaji kuwa anamiliki kampuni ya ‘m/s shumoja.'
Nihitimishe makala hii kwa kutoa wito kwa wananchi kudai dhana ya ‘open government' anayehubiri Rais Kikwete itumike pia kutoa majibu kwa maswali mbalimbali yanayoleta wasiwasi kuhusu mradi huo wa usafiri wa kisasa sambamba na wasifu wa mwekezaji huyo. Tumeshafanya makosa mengi huko nyuma, lakini bado tuna fursa ya kujirekebisha kwa kuwa makini na kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
by
ELLY MOSI