Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowasa amefuta ziara yake mikoani kwa ajili ya kujenga chama. Mtakumbuka kuwa siku kadhaa zilizopita, Lowasa alizindua mikutano ya ndani kwa lengo la kuwashukuru wafuasi wa CHADEMA waliompigia kura na kupeana mikakati ya jinsi ya kuimarisha chama hicho kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020 ambapo amejitangaza kuwa mgombea pekee kupitia CHADEMA.
Sababu za kufutwa kwa ziara hizo imeelezwa kuwa ni ukata unaomkabili mwanasiasa huyo uliotokana na kuwekeza fedha nyingi kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Inaelezwa kuwa mwanasiasa huyo alitumia fedha nyingi sana kwa ajili ya uchaguzi huo huku akiwa na madeni kibao aliyokopa kwa marafiki zake kwa madai kuwa atawalipa akishakuwa Rais. Kwa sasa hali ya mwanasiasa huyo kisiasa na kifedha inaelezwa kuwa mbaya sana na inasemekana kuwa hata nyumba yake ya Masaki imepigwa bei ingawa taarifa hizi bado hazijathibitishwa. Pia inadaiwa kuwa Lowasa yupo mbioni kuuza nyumba yake iliyopo London, Uingereza kwa lengo la kupata fedha za kuponya majeraha ya uchaguzi.
Pia imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema kuwa chama kwa sasa hakina fedha za kugharamia harakati za kujenga chama mikoani na kwamba ikiwa kuna ulazima wa kufanya hivyo, ni vema Lowasa akajigharamia kama alivyofanya kwenye mikutano ya kampeni.
Sababu nyingine iliyoelezwa ya Lowasa kusitisha ziara hizo ni mtafaruku uliopo ndani ya CHADEMA. Kitendo cha Lowasa kumteua Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu kwenye mikutano yake ya bara hakika ilizua maswali mengi sana. Inadaiwa kuwa Salum Mwalimu ndiye chaguo la Lowasa na anamuandaa awe Katibu Mkuu ifikapo 2017 ambapo inatarajiwa kuwa Lowasa atagombea na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kambi ya Katibu Mkuu ambaye anaungwa mkono na Mbowe inaonekana kukosa raha na uamuzi huo wa Lowasa hasa kutokana na kitendo cha Lowasa kushindwa hata kumpigia simu Katibu Mkuu, Vicent Mashinji katika jitihada zake za kujenga chama mikoani. Mashinji amesikika akihoji, inakuwaje Lowasa anafanya ziara mikoani bila hata ya kuwasiliana na Katibu Mkuu wa chama hicho?
Nilipohoji ikiwa uamuzi huo unatokana na kitendo cha jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, chanzo changu ndani ya CHADEMA kimetanabaisha kuwa kilichokatazwa ni mikutano ya hadhara na Lowasa alikuwa anafanya mikutano ya ndani kama alivyofanya kule Monduli. Hivyo si kweli kuwa kusitishwa kwa mikutano hiyo kunatokana na katazo hilo la serikali bali ni matatizo ya ndani ya CHADEMA.