Ziara ya Trump China, Boeing yaula

ze kokuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
7,476
Reaction score
9,654
China imetoa oda ya kununua ndege za Boeing zaidi ya 300,hayo yamejiri baada ya Trump kuzuru nchi hiyo katika ziara yake ya bara la Asia.

Nchi hiyo na Marekani zilitiliana sahihi kwenye mikataba yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 250($250bn),ikijumuisha ununuzi ndege za abiria(Boeing), injini za ndege, magari,chip za kwenye simu zinazotengenezwa Marekani ikiwa ni oda toka kwa kampuni ya Xiaomi na nyinginezo, nk.

Dili hilo kwa Boeing lina thamani ya zaidi ya dola bilioni 37($37bn).
Trump ameonekana kuonyesha uwezo wake katika mazungumzo ya kibiashara na kupata mikataba yenye thamani kubwa kwa kampuni za Marekani. Mwezi uliopita shirika la ndege la Singapore airlines Ltd walitiliana sahihi na kampuni ya Boeing mkataba wa dola bilioni 13.8 ($13.8bn) tukio lililoshuhudiwa na Trump pamoja na waziri mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong.

Mashirika ya ndege ya China yamekua ni mnunuzi mkubwa wa ndege kutoka Boeing na Airbus, ikiwa ni matarajio ya nchi hiyo kuipiku Marekani kama kinara wa soko la usafiri wa anga baada ya miaka mitano. Boeing imesema kwamba baada ya miaka 20 inatarajia kwamba China itahitaji ndege 7,240 zenye thamani ya dola zaidi ya Trilioni 1.1($1.1 trillion).

Mpaka sasa mashirika makubwa ya ndege ya China Air China Ltd, China Eastern Airline Corp, China Southern co yanatarajia kuongeza ndege 600 mpaka kufikia mwaka 2020.
 
China wanaitumia hiyo nafsi ili Trump asifunge uhusiano wao hapo China itaendelea kupata nafasi kimataifa.
 
Reactions: SDG
Sawa ni kweli mkuu nakubali ila tuache mbwe mbwe basi wakati bado tupo mchicha, tusubiri hata tusogee tuwe kama mpapai ndio tuanze makelele
Mkuu huo ni uchochezi ujue [emoji23]
 
China wanaitumia hiyo nafsi ili Trump asifunge uhusiano wao hapo China itaendelea kupata nafasi kimataifa.
Fuatilia ziara zote Trump kuanzia ile ya Saudia, Poland, South Korea, Japan na China. Kote huko anapata madili tu

•Saudia -Silaha dola bilioni 350 kwa ujumla

•Poland - Gesi
•South Korea - Silaha
•Japan -Silaha
•China -Biashara kama hvyo ndege, uchimbaji gas, nk

Naomba siku na Tanzania tupate Rais mfanyabiashara kama Trump
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…