Ziara ya RC Gambo chuo kikuu cha Arusha

Jim007 2

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
395
247
Leo tarehe 27/01/2017 Mh mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amefanya ziara katika chuo kikuu cha Arusha. Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa amezungumza na uongozi wa chuo,watumishi pamoja na wanafunzi.
Pia alipata fursa ya kutembelea miundo mbinu mbali mbali ya chuo hicho ambacho kinamilikiwa na kanisa la Waadventista Wasabato.

Alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi na kusikiliza kero zao na changamoto zinazowakabili ikiwemo kutokuridhishwa na huduma zinazotolewa na mfuko wa Bima ya Afya katika utoaji wa kadi za Bima ya Afya hivyo kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa utoaji wa huduma hiyo chuoni hapo.
Masuala mengine ni kama tatizo la kukatika umeme mara kwa mara, tatizo la maji, ulinzi na usalama chuoni hapo, sehemu kubwa ya wenye sifa ya kukopeshwa na bodi ya mikopo kutokuipata mikopo hiyo, pia wamemweleza hofu yao ya kumaliza masomo na kukosa ajira.

Katika kujibu changamoto hizo mkuu wa mkoa ameuagiza uongozi wa NHIF (bima ya Afya) mkoa wa Arusha kufika chuoni hapo mara moja ili kuweza kulitatua tatizo hilo ndani ya wiki moja toka leo.
Mkuu wa mkoa ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndg. Alexander Mnyeti na Mhandisi wa maji wilaya ya Arumeru kufika chuoni hapo siku ya Jumatano tarehe 01/02/2017 na kukaa na uongozi wa chuo kuona namna wanaitatua kero hiyo ya maji ya muda mrefu.

Kuhusiana na suala la ulinzi chuoni hapo na maeneo ya jirani Mh. Mkuu wa mkoa ameihamasisha jamii nzima ya Arumeru bila kuwasahau wanachuo wenyewe kuona namna gani wanaweza kujenga kituo cha polisi ili kuimarisha usalama chuoni hapo na maeneo ya jirani, kwa kuanzia Mh. Gambo ametoa mabati 100 ili kuamsha ari ya wananchi na jamii nzima ya Arusha University kuanza ujenzi huo mara moja.

Mh. Gambo ameichukua hoja ya wanafunzi walio na sifa za kukosa mkopo na kuagiza uongozi wa chuo kumpa majina ya wanafunzi husika na ofisi yake kuyawasilisha bodi ya mikopo ili yashughulikiwe, pia ametoa changamoto kwa vyuo kutoa kozi kulingana na mahitaji ya serikali kwa wakati husika ili kuepusha mgogoro wa kuwa na wahitimu wengi wasio na ajira.
Vile vile katika kujibu baadhi ya changamoto Mh Gambo aliwapongeza wanafunzi kwa ujasiri wa kutoa kero zao bila woga na ameahidi ataweka utaratibu wa kutembelea vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha ili kujua mazingira halisi na matatizo yanayokabili vyuo husika.

847c6268013f4a7b6718e9546a5de342.jpg


Picha Mh Gambo akivalishwa skafu na wanafunzi wa TAPS walio katika eneo hili la chuo kikuu Arusha , akisaini kitabu cha wageni na akifanyiwa utambulisho na makamu mkuu wa chuo.

8be33a3c9f736f93ed4df6dbeab01aa7.jpg

49f53199d318dd34e576938e48f9b63c.jpg
e67a66199e51dd5aab4cb465686fd907.jpg
121e49efa5d167d56a5c37295b3239ab.jpg
92b614effbb4fcbde9258f6f076502d1.jpg
def88833ee84c06274b110d4b5c5efbe.jpg
 
Nawaona Chadema mnavyochungulia na roho inavyowauma
Hili sio swala la U-chadema wala U-ccm, Huyu Jamaa tangu aingie Arusha sijaona la maana alilofanya, sana sana kuharibu utulivu uliokuwepo na kuchonganisha wananchi na viongozi wao waliowachagua.
 
Hiyo picha inamuonesha alivyo na uchu wa madaraka kuliko utu, kajivimbisha na kujitutumua wakati hata hajai kiganjani, looh1 kweli kazi imepata mtu wa kuipindisha badala ya kuifanya.
 
Hili sio swala la U-chadema wala U-ccm, Huyu Jamaa tangu aingie Arusha sijaona la maana alilofanya, sana sana kuharibu utulivu uliokuwepo na kuchonganisha wananchi na viongozi wao waliowachagua.
Hivi mkuu ni kwamba huoni kweli ama umeamua kujitoa ufahamu??..kushughulika suala la maji kwa wanfunzi wa chuo cha Arusha huoni kama ni jambo la mmana kwako??...kutatua changamoto ya usafiri kwa wanafunzi hawa kwako hilo si jambo la maana, kushauri uongozi wa chuo kutowazuia wanafunzi ambao hawajakamilisha ada kufanya mitihani hilo sio la maana??...hebu wakati mwingine muweke mapenzi ya uvyama pembeni muongee hoja.
 
Hili sio swala la U-chadema wala U-ccm, Huyu Jamaa tangu aingie Arusha sijaona la maana alilofanya, sana sana kuharibu utulivu uliokuwepo na kuchonganisha wananchi na viongozi wao waliowachagua.
Tulieni dawa iingie hii ni awamu ya Magufuli na vijana wake
 
Back
Top Bottom