Ziara ya Mbunge wa Ukonga Machinjioni ya Mazizini Ukonga na mnada wa Pugu

JUkonga

Member
Dec 30, 2015
14
13
ZIARA YA MBUNGE WA UKONGA MH. WAITARA MWITA MACHINJIO YA UKONGA MAZIZINI NA PUGU MNADANI
Siku ya Jumanne tarehe 19.01.2016, Mbunge wa Ukonga alifanya Ziara ya kutembelea Machinjio ya Mazizini katika Kata ya Ukonga na Mnada wa Pugu ulioko kata ya Pugu Station jimbo la Ukonga.
Msingi wa Ziara ya Mbunge Mh. Waitara kwenda machinjio ya Mazizini Ukonga ni kama ni kutokana na malalamiko ya Wananchi na Wafanyabiasha wa Machinjio hayo: Baadhi ya Malamiko hayo ni pamoja na:
1. Wafanyabiashara wanalipa ushuru na unachakachuliwa, machinjio ya Mazizini wanachinja ng'ombe 400 hadi 500 kwa Siku, na kila moja ushuru ni Tsh. 2500. Ila taarifa iliyoko Manispaa ni ng'ombe 700 tu kwa wiki au wastani wa ng'ombe 100 kwa Siku, ukipiga hesabu ya chini, ushuru wa ng'ombe 400 kwa Siku ni 1milioni kwa wiki ni milioni 7 na kwa mwezi ni milioni 28. Taarifa iliyoko Manispaa ya Ilala ni kwamba, kwa siku ni 350,000, wiki ni 1.75mil na kwa mwezi ni 7mil, tofauti ya milioni 21. Huo ndiyo msingi wa kwenda Mazizini na sehemu pekee ya mbunge kupata taarifa ya kweli ni kwenda sehemu hisika na kuwasikiliza wadau wa pande zote mbili, wanaolipa na wanaopokea ushuru.
2. Kero ya pili ni mwekezaji wa Machinjio ya Mazizini anatiririsha Maji machafu kwa wananchi wananaozunguka eneo hilo, na malalamiko ya wananchi ni makubwa sana, tumekagua na imethibitika hivyo.
3. Huyu mwenye machinjio hana hata leseni yeyote ya biashara hiyo na wala halipi kodi yeyote serikalini na anachukua Tsh. 6300 kwa kila ng'ombe, ukipiga heasbu kwa idadi ya chini huyu mtu anapata 2.4mil kwa siku na 72mil kwa mwezi na halipi kodi yeyote na mazingira ni machafu sana.
4. Kulikuwa na malalamiko ya ushuru wa tsh. 500 hetini kwa wafanyabiashara ambao hauna stakabadhi na haijulikani nani anachukua pesa hizo.
ZIARA YA MNADA WA PUGU:
1. Kulikuwa na malalamiko ya wafanyabiashara, wanalipa ushuru wa Tsh. 6000 PUGU mnadani na wakifika Mazizini wanalipa ushuru wa Tsh. 2500, hoja ikaja kwanini ushuru ulipwe Mara mbili sehemu mbili tofauti ndani ya Manispaa moja? Kwanini usilipwe sehemu moja? Haya yote Mbunge ameyabaini na hakuwa mwenyewe alikuwa na madiwani wanne wa Jimbo la Ukonga.
2. Hoja nyingine ya wafanyabiashara wa Pugu kuna Tsh. 10000 wanalipwa askari wa mnadani na Daktari wa Mnada wa Pugu 10000 jumla ni Tsh 20000 bila risiti maana yake ni rushwa, tumepiga hesabu hawa watu wanachukua 400,000 kwa siku na 12mil kwa mwaka. Pesa zote hizo hazina stakabadhi na ni lazima ulipe. Sehemu pekee ya mbunge kupata ukweli wa malalamiko kama hayo ni kwenda sehemu husika na kuwasikiliza wadau wa pande zote mbili.
3. Kero nyingine ya wafanyabiashara ni kwamba ng'ombe wanaokufa hawachomwi, wanachunwa na kipelekwa sokoni maana yake watu wetu wanakula vibudu, hili nalo tumejiridhisha kwa sababu tumeona hakuna dalili ya majivu kwenye hiyo sehemu ya kuchomea ng'ombe waliokufa.
4. Kero nyingine mdiyo hiyo ya mazingira ya Mnada hakuna Maji, hakuna sehemu ya kunyweshea ng'ombe na vyoo hakuna vilivyoko ni vya kulipia kati ya Tsh 500 na 1000 kuoga. Pamoja na hasa watu kulipia ushuru, hata huo ushuru haufanyi kazi inayotakiwa.
MSINGI WA ZIARA YA MBUNGE NI KUSIKILIZA KERO ZA WAPIGA KURA WAKE NA KUBAINI UKWELI WAKE NA SASA ANAZIFANYIA KAZI.

Kwa taarifa Mbalimbali za jimbo la Ukonga tembelea Blog: MBUNGE WA UKONGA WAITARA M. MWIKWABE
 
Hapa si Mwigulu alistukiza usiku na tukaambiwa kuna Majipu yametumbuliwa???



Akaagiza ushuru ukusanye sehemu moja tena kwa EFD.....
 
Kwa sasa machinjio yanakusanya 80m kwa mweli badala ya 18m za awali.Duu kuna wamefaidi hii nchi balaa
 
kwanini mambo muhimu namna hii mnakaa nayo hadi yanapauka ? mmelenga kumhujumu mh mbunge ?


Mkuu hili jambo limechelewa kuja JF, ila lilishakuwa kwenye mitandao mengine ya jamii kama facebook na blogs.
Pia walikuwepo waandishi wa Habari na Redio mbalimbali.
 
Mkuu hili jambo limechelewa kuja JF, ila lilishakuwa kwenye mitandao mengine ya jamii kama facebook na blogs.
Pia walikuwepo waandishi wa Habari na Redio mbalimbali.
jf ni zaidi ya redio au tv mkuu , kila kizuri kiletwe kwanza jf ndio msambaze huko kwingine .
 
Back
Top Bottom