asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,041
Kuna habari zinazosema kuwa Che na Castrol walikosana. Castrol akataka Che aondoke Cuba. Hivyo alivyosafiri, Castrol akaandika barua kama vile ni CHE ameandika ili kuwaaga watu wa Cuba kuwa hatarudi tena Cuba.
Hiyo ilipelekea jamaa kuanza kutangatanga hapa na pale. Maada ya kutoka Tanganyika, kuna kila dalili kuwa mipango yake ilikuwa imekaa ovyo na kwa hali ya kawaida, angelitaka kurudi NYUMBANI ambako ilikuwa CUBA. Ila kutokana na barua hiyo, ikawa ameshafungiwa tayari milango. Akaondoka kichwakichwa kuelekea Bolivia ambako hawa Wajinga wakiwa wameshapewa habari kuwa yupo pale kijijini kwao hoi, wakaenda na kumuuwa. Nasikia baadaye walijilaani sana kugunduwa wametumika kumuuwa mtu kama huyo.
Kuna habari zinazosema kuwa Che na Castrol walikosana. Castrol akataka Che aondoke Cuba. Hivyo alivyosafiri, Castrol akaandika barua kama vile ni CHE ameandika ili kuwaaga watu wa Cuba kuwa hatarudi tena Cuba.
Hiyo ilipelekea jamaa kuanza kutangatanga hapa na pale. Maada ya kutoka Tanganyika, kuna kila dalili kuwa mipango yake ilikuwa imekaa ovyo na kwa hali ya kawaida, angelitaka kurudi NYUMBANI ambako ilikuwa CUBA. Ila kutokana na barua hiyo, ikawa ameshafungiwa tayari milango. Akaondoka kichwakichwa kuelekea Bolivia ambako hawa Wajinga wakiwa wameshapewa habari kuwa yupo pale kijijini kwao hoi, wakaenda na kumuuwa. Nasikia baadaye walijilaani sana kugunduwa wametumika kumuuwa mtu kama huyo.
aksante mkuu Sikonge ,ila niliwahi kuhudhuria kongomano la maadhimisho kama sikosei ya miaka 40 toka che guevara apite Tanzania lilifanyikia UDSM yalihudhuriwa na wanamapinduzi wengi sana na wanahistoria wengi mpaka balozi wa cuba aliyepigana na che wakati wa mapinduzi hayo na ushuhuda wa kitabu cha yule mwanamapinduzi wa zanzibara anaitwa Babu ila sikuwahi kusikia kitu kama hicho cha kugombana na Fidel.
mkuu zile zilikua propaganda za wamarekani tu, che na castro hawakukorofishana kama inavyodaiwa. kimsingi che alijiuzulu uwaziri nadhani mwaka 1964 kwa lengo la kuingia vitani kuikomboa latin america na maeneo mengine ya third world. aliondoka cuba kuja tz, then congo akawa haonekani wala hasikiki kule cuba, USA ikaanza kutangaza propaganda kua che ameuawa na castro coz alikua threat kwake kitu ambacho si kweli
ikumbukwe wakati che anaongea kwa mara ya mwisho(siku ile aliyouawa) na yule wakala wa CIA aliyefanikisha kumkamatwa kwake(wakala wa CIA Felix Rodriguez), che alieleza wazi kua ni castro aliyeshauri waanze harakati za ukombozi katika nchi ya Bolivia then waende argentina.
pia ni castro huyo huyo aliyefanikisha kuutafuta, kuupata na kuurudisha nyumbani mwili wa che na macomrade wengine, kazi iliyochukua miaka 30 coz kaburi la che lilikua unspecified
ni castro huyo huyo aliyeanzisha utaratibu kwa wanafunzi wa cuba kuimba nyimbo za kumsifu che kila siku wawapo mstarini(assemble), yeye mwenyewe wala hakuagiza aimbwe au kutukuzwa.
ni castro pia ambaye alivunja mahusiano na Bolivia na kutishia kuivamia kijeshi baada ya kuuawa kwa che.
haya yote yanathibitisha namna gani hawa macomrade walivyopendana
Sikuwahi kusikia kwamba alifika Tz ingawa alifika Kongo (Zaire) na kusaidia harakati za kivita.
Samahani Wakuu, labda nimeandika vibaya au nimeeleweka vibaya.
Kwenye uongozi kila mtu huwa na njia zake anazoona zinafaa kufuata. Baada ya Cuba kuwa chini ya hawa jamaa, Castro alianza kutimiza mipango yake na Che akawa na yake. Hapo ndipo ukatokea mpingano wa mawazo na kila mtu akiwa na wake. Che akaamua kuondoka Cuba na kuendelea kupigana.
Sasa hapa ndiyo habari zinapishana. Wengine wanasema aliandika barua hiyo kwa sababu alikuwa kashapishana na Castro na Castro hakutaka jamaa arudi tena Cuba. Kuna dalili nyingi zinazoonyesha kuwa baada ya kutoka Tanganyika, alitaka sana kurudi Cuba ambako angelijipanga vyema kabla ya kuondoka kwenda Bolivia. Ile safari ya Bolivia ni kweli kuwa alikuwa hajajiandaa vizuri.
Habari ya pili ni kuwa ile barua ya kuaga kuwa hatarudi Cuba, ilikuwa inalengo na kumuweka pembeni Castro na Cuba kama ikitokea kuwa Che amekamatwa. Yaani hata angelikamatwa basi hayo mapinduzi yake au kushindwa kwake kusimuhusishe Catro.
Sasa ukweli ni upi? Ni ngumu kwangu kusema kwa sababu kila sababu inaweza kusimama na kujitetea.
Hivyo Mkuu Voice of Mtwara, nafikiri hapa wala USA tusiingize kwa sababu tunaongelea BARUA ambayo ni kweli ipo. Swali tu hapa ni kuwa: Barua aliiandika kweli Che mwenyewe/alitoa idhini iandikwe au aliandika Castro ili amruke Che ikitokea amekamatwa akipindua nchi? Waligombana au hawakugombana si muhimu sana na hilo linatumika tu kutaka kujua nani aliandika ile BARUA ambayo ni kweli ipo.
Ohh, mwisho ni kuwa hata Castro ni Mwana Siasa tu ambaye kubadilikabadilika ni jambo la kawaida. Alijua sana kucheza karata zake na ndiyo maana hadi leo bado yupo hai pamoja na kuwindwa sana na USA. Ila mwisho wa siku, unagundua kuwa kati ya Che na Castro, kwenye mioyo ya watu, ni CHE bado yupo hai. Castro alilijua hilo na alilitumia sana kisiasa.
Khaa! Kumbe....kama hapo si mbali, nitapita!
nazidi kuikubali jamiiforums!Che Guevara[John the Baptist] alifika Kigoma with 100 Cuban Revolutinaries. Lakini alisikitika sana kuona kwamba Waaafrika hawana mwamko wa kisiasa,akaondoka. Alikuja kwa madhumuni ya Kwenda Kongo. Halafu akaenda Bolivia,akauawa,akakatwa kichwa. Alipokuwa Dar es Salaam,nasikia favourite restaurent yake ilikuwa ni Zahir Hotel. Hii Zahir Hotel sijui kama bado ipo. Nimewahi kwenda pale siku moja kula biriyani.
Maelezo yako yanaeza kua na ukweli kwa kiwango fulani, lakini familia ya Mandela sidhani kama imezuia kwenda kwa sababu unazotaka kutuaminisha. Mwaka jana nadhani Michelle alienda kumtembelea Madiba na hata picha zipo kuthibitisha haya. Na hata kitabu cha Mandela cha mwaka 2011 , Conversations with Myself foreword yake ameandika Hussein Onyango, nadhani si vema kuongelea vitu tusivo na uhakika navyo/Ni kweli Che alikuja Tz 1964 akitokea Congo, ni kweli pia wapiganaji wa Congo walimkatisha tamaa kwa sababu kila ikifika jioni ni lazima wapate pombe, muziki na ngono. Lakini wapiganaji hao wa Congo walimpenda sana kutokana na ujasiri na umahiri wake wa mapambano, wakati anawaaga kwenda kwenye mapambano ya Bolivia walimpa kifurushi cha Almasi ili zikamsaidie kwenye mapambano ya Bolivia, lakini alikataa akawaambia "SIKUJA KUFANYA BIASHARA, NIMEKUJA KUPIGANA!" Alipotoka huko alipitia Dar, alikaa siku chache kabla kuelekea Bolivia alikokwenda kuuawa kikatili na CIA ya Marekani. Manowari ya Kimarekani iliegeshwa katika bahari ya Hindi katika fukwe za Tz zikiwa na vifaa maalum vya kumfuatilia nyendo zake ili kumnasa na kumuua, lakini msimamo wa Nyerere ulikuwa pamoja na wapigania uhuru hivyo hakuwapa ushirikiano wamarekani kabisa katika suala hilo (alikuwa kwenye orodha ya magaidi pamoja na kina Nelson Mandela kwa mtazamo wa Marekani) Hivyo Comrade Che Guevara alijisikia nyumbani alipokuwa Dar, hivyo inawezekana kabisa alikwenda kula biriyani pale Zahir Restaurant.
Marekani haikuunga mkono mapambano ya ukombozi dhidi ya Wakoloni, na mpaka leo Marekani haiungi mkono mapambano yoyote ya kujikomboa kiuchumi, hasa kwa nchi ndogo zenye rasilimali nyingi ambazo wao wanazihitaji, watazidumaza kwa misaada na kuwahonga viongozi wake ili zisijitegemee ili zisiwe na maamuzi yake yenyewe juu ya rasilimali hizo, bali maamuzi yawe ni yao wamarekani, ndivyo ilivyo kwetu Tz, hatutakuwa na maamuzi juu ya Gesi wala Urani yetu, hata wananchi wakipinga nguvu za ziada za kijeshi zitatumika dhidi yao, lakini kule South Africa kwa Mzee Madiba hali ni tofauti, viongozi wa Marekani hawapati mapokezi mazuri kutoka kwa wananchi zaidi ya yale ya kiserikali, rasilmali zao wanazipangia wenyewe, hata Obama hawakumshobokea bali waliandamana kupinga ujio wake na walitaka akamatwe na kushtakiwa kwa kukiuka haki za binadamu kunakofanywa na utawala wake sehemu mbalimbali duniani, hata familia ya Mzee Mandela ilimkatalia kwenda kumjulia hali Mzee Mandela hospitalini.
Che Guevara angekuwa hai leo, au kama huko aliko anaweza kutuona tunavyowashobokea Wamerakani, hakika angetulaani na kutuchukia kuliko alivyowachukia wapiganaji wa Congo!
Zahir Hotel bado ipo.
Shariff Ritz,
Vipi na ile Al Kefak pale Mkunguni Str. nafikiri ilikua zamani ndo inashindana na hiyo Zahir kwa Mishikak,bokoboko/mandi na Sekela Tikka,Nan bread na vikorombwezo vinginevyo vingi mno...
wakti ule Nyerere alikua kafungia takriban kila kitu! Dah! yaani yule mtu alikua muhuni saana!ahaha!!
Nakumbuka sehemu ya Ice Cream ilikua moja tu mji mzima pale Snow Cream,wakti huo Bakhressa maskini hata mitambo ya Ice Cream hajawa nayo!?
Wenzetu Kenya walitutangulia kwa mengi...nakumbuka pale Nairobi zamani mno walikua na ile Malindi Dishes!
Yaani Wana-Mzizima tumetokea mbali mno!ahaha!!
Ahsanta.
Kuna habari zinazosema kuwa Che na Castrol walikosana. Castrol akataka Che aondoke Cuba. Hivyo alivyosafiri, Castrol akaandika barua kama vile ni CHE ameandika ili kuwaaga watu wa Cuba kuwa hatarudi tena Cuba.
Hiyo ilipelekea jamaa kuanza kutangatanga hapa na pale.
Maada ya kutoka Tanganyika, kuna kila dalili kuwa mipango yake ilikuwa imekaa ovyo na kwa hali ya kawaida, angelitaka kurudi NYUMBANI ambako ilikuwa CUBA. Ila kutokana na barua hiyo, ikawa ameshafungiwa tayari milango. Akaondoka kichwakichwa kuelekea Bolivia ambako hawa Wajinga wakiwa wameshapewa habari kuwa yupo pale kijijini kwao hoi, wakaenda na kumuuwa. Nasikia baadaye walijilaani sana kugunduwa wametumika kumuuwa
mtu kama huyo.
Al Habiby gombesugu,
Unanikumbusha mbali sana Al Kefak, hawapo siku hizi kuna Al Uruba, na wenyewe hatari kwa biriyani basmat, Mbuzi, Maziwa ya Ngamia, na Faluda.
Wewe mburula kaa kimya hujui kitu kama babayako; alifika Kigoma ,Tanganyika hakwenda Zenj!!!
Maelezo yako yanaeza kua na ukweli kwa kiwango fulani, lakini familia ya Mandela sidhani kama imezuia kwenda kwa sababu unazotaka kutuaminisha. Mwaka jana nadhani Michelle alienda kumtembelea Madiba na hata picha zipo kuthibitisha haya. Na hata kitabu cha Mandela cha mwaka 2011 , Conversations with Myself foreword yake ameandika Hussein Onyango, nadhani si vema kuongelea vitu tusivo na
uhakika navyo/
Maelezo yako yana walakin, kwanza Che kwao sio Cuba bali ni Argentina, alienda Cuba kuwasaidia kina Castro kuikomboa Cuba, baada kuikomboa Cuba alipewa uwaziri wa Viwanda na Biashara, wazo la kuwa Waziri wakati nchi nyingine bado zimo kwenye mapambano hakuliafiki, ndipo alipoondoka kwenda kupambana katika nchi nyingine duniani kama vile Vietnam, Cambodia, Congo nk hata kule ambako hakufika kama vile South Africa, Mozambique nk aliwafundisha wapiganaji wao mtindo wake maarufu wa
kupigana wa "Guerrila Warfare" ambao uliwasumbua sana watawala wa kikoloni na ulileta ushindi sehemu nyingi.
Yakhe Gombesugu una taabu kwelikweli weye,Wallahi,Shariff Ritz...tumetokea mbali mno!ahahaa!
Al Uruba napajua pale,napenda ile mikarangizo yao ya Hargeisa!ahahaa!!...nafikiri ipo Mkunguni Opp. na Chura!
Naikumbuka ile Ice Cream ya zamani tuko Primary ikiitwa "Chachamao"!ahahaa!
Mimi bakhti nzuri najua mpaka siku hiyo hapo Zahir, Che Guevara alipata Menu ipi!...na alikua na nani.
Ahsanta.
Hata Castro siyo M-Cuba ila ni M-Spain na ndugu zake wa Spain wanafahamika. Baba yake alizaliwa Spain na huko kuhamia tu kwenye mizunguko ya maisha.
Hapa bado tunaongelea ile barua kama ni kweli aliandika au hakuandika. Alikozaliwa au hakuzaliwa siyo muhimu.
Barua ni barua tu, inawezekana aliiandika au hakuiandika, lakini hakuna dalili kwamba walikosana na Castro kama ambavyo CIA walitaka kuuaminisha ulimwengu, kwani base yake ya operation ilikuwa ni Cuba, hata alipokuwa Tz alifikizia ubalozi wa Cuba, Hata wakati anaenda Bolivia, alifikia kwanza Cuba kisha ndio akaelekea Bolivia, kule alikuwa akitumia mawasiliano ya Radio call kuwasiliana na Cuba, CIA kwa kutumia mitambo yao waliintercept kisha kudisrupt mawasiliano hayo na kufanikisha kumkamata kwa kutumia vibaraka. Sasa huo ugomvi na Castro umetokea wapu?Hata Castro siyo M-Cuba ila ni M-Spain na ndugu zake wa Spain wanafahamika. Baba yake alizaliwa Spain na huko kuhamia tu kwenye mizunguko ya maisha.
Hapa bado tunaongelea ile barua kama ni kweli aliandika au hakuandika. Alikozaliwa au hakuzaliwa siyo muhimu.