Zesco United Football Club special Thread

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,692
Ni klabu ya soka yenye makazi yake katika mji Ndola na inashiriki katika ligi kuu nchini humo Zambian premier league.

Klabu ilianzishwa mnamo January 1, 1974 na klabu hii imetumia mda mwingi kuwa juu toka toka ianzishwe. Uwanja wao wa nyumbani wa Levy Mwanawasa Stadium uliopo Ndola kusini mwa Zambia, una uwezo wa kubeba mashabiki 49,800 na ulizinduliwa mwaka 2012.

Sijui Kama unajua ila nahisi hujui Zesco FC ni kifupisho cha Zambia electricity Supply Corporation United Football.
Kwa majina ya utani wanaitwa Team Ya Ziko, Zegalacticos, Zega Mambo, Team Zega.

klabu hii inamilikiwa na na kampuni ya umeme ya ZESCO.
Klabu ya ZESCO United ilipata mafanikio yake ya kwanza mwaka 1980, waliposhinda taji la Zambian Division One. Baadae mwanzoni mwa miaka ya 2000 waliposhinda taji lingine la Zambian Division One mwaka 2003, FAZ Premier League mwaka 2007, 2008, 2010, 2014 na 2019, the Barclays Cup mwaka 2007, 2008, 2010 na 2014, ABSA Cup mwaka 2019, Zambian Charity Shield mwaka 2007 na 2011 the 2006 Mosi Cup, na mwaka 2007 wakashinda Zambian Coca Cola Cup.

Zesco ndiyo klabu ya kwanza kutoka Zambia kufuzu hatua ya makundi CAF African Champions League mwaka 2009. ZESCO ni klabu moja Kati ya klabu tatu kubwa kule Zambia ikiwemo Nkana na Green Buffaloes ambazo zina rekodi ya kutofungwa katika uwanja wa nyumbani na klabu za kigeni.

ZESCO United pia ni klabu ya kwanza Zambia katika karne hii kucheza na klabu kutoka ulaya pale waliocheza na Zenit Saint Petersburg nchini Abu Dhabi mwaka 2008.
Walifika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa afrika kwa mara yao ya kwanza na ya mwisho baada ya kutoa sare ya 2-2 kule misri kwa mabingwa wa nchi hiyo Al Ahly.

Waliendeleza rekodi yao kutofungwa na klabu kutoka nje ya Zambia na ilikua mechi ya 26 bila kufungwa siku ya jumamosi September 17, 2016 baada ya kuitandika 2–1 klabu Mamelodi Sundowns FC in the CAF African Champions League.

Zesco United ndiyo timu yenye wachezaji wengi wakigeni nchini Zambia. Msimu wa 2015 wachezaji kutoka Kenya, Nigeria na Tanzania waliongeza ladha kwenye klabu hiyo wakiwemo Ayo Oluwafemi na Christopher Chigozie (wote kutoka Nigeria), pia alikuepo David Owino kutoka Kenya na Juma Luzio kutoka Tanzania na msimu uliopita aliingia mchezaji kutoka Togo Emmanuel Mathias.

Hii ndiyo klabu itakayo pambana na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania.
IMG-20190903-WA0068.jpeg
 
Yaani hadi zesco inaanzishiwa jukwaa lake maalumu huku ikiwa ni timu ndogo tu isiyo na tija yoyote ile kwa ukanda wetu huu wa cecafa! Au kwa sababu itakutana na timu ya wananchi siku chache zijazo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom