Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Miongoni mwa mambo ambayo raia wengi huogopa kuyazungumzia kiundani ni mfumo wa saisa yetu.
Wengi wao hudhani siasa ni kwa ajili ya watu fulani walio maalumu na inawahusu hao tu.
Ndio maana ukizungumzia jambo lolote kiyakinifu au kupinga hoja ya jambo fulani kwa fikra za kina watu watakwambia unaleta siasa.
Kwamba ni kutoelewa mantiki ya siasa, ndio maana watu huogopa na kutotaka kujihusisha nayo?.
Hapana hata walio na elimu na taaluma nao bado wanaogopa kuzungumza chochote kuhusu mifumo ya siasa nao wakiamini kuwa siasa ni jambo hatari.
Kwa mujibu wa kamusi ya Oxford ya Lugha ya Kiingereza inaeleza maana ya siasa kuwa ni mfumo jumuishi wa kiserikali au Kikundi Cha watu unao husisha maamuzi na nguvu ya Madaraka.
Kwa mantiki hii siasa imebeba maamuzi, watu na madaraka hivyo hakuna siasa pasipo watu na hakuna maamuzi pasipo watu na hakuna madaraka pasipo siasa.
Dhana inayohusisha neno siasa hupotoshwa kwa maksudi au kwa kutokukusudia na kufanya watu wahofie kujihusisha nayo ndani ya jamii.
Hali hii imepelekea watu wachache kujihusisha na siasa na kuthubutu kuwa Sehemu ya siasa na kupewa fursa mbalimbali ndani ya mfumo wa siasa hasa uongozi.
Kundi liliosalia hulazimika kuwa kundi linalopokea maagizo, matamko na amri kwakua halina nguvu ya kufanya maamuzi na limekosa madaraka.
Kwenye jamii inayoelewa mantiki ya siasa, watu hujihusisha katika siasa pasipo woga wala hofu kwakua wanajua faida na hasara zake.
Jamii iliyoshiba maarifa huiona siasa kama njia sahihi ya kutatua matatizo mbalimbali katika jamii.
Jamii iliyokosa muamko wa kisiasa hukosa dira na mtazamo chanya katika maendeleo kwakua maamuzi ya umma hushikiliwa na Watu wachache ambao muda mwingine huweza kufanya watakavyo kwa maslahi yao binafsi.
Hayati Julius Nyerere aliwahi kusema "Wanasiasa Wana tabia ya kimalaya Malaya" kauli hii ililenga kuwafahamisha raia kuwa wanasiasa wengi wa wakati huo walikuwa na tabia ya kuwa wasaka fursa na wadanganyifu ambao muda mwingine hawaeleweki.
Kuwaachia watu wachache washike madaraka na wao ndio wafanye maamuzi ni kuendekeza uozo katika jamii kama alivyosema Nyerere.
Peter Mwaihola ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na Jamii.