Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Kilio cha Wanawake na Wanaharakati wa kutetea haki za wanawake kuhusu dhamana ya gharama za fedha za uchukuaji wa fomu, kugombea nafasi ya urais,uwakilishi na udiwani katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kimepatiwa ufumbuzi baada ya ZEC kupunguza asilimia 50 ya gharama hizo kwa wagombea wanawake.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji George Joseph Kazi, ametangaza punguzo hilo kwa wagombea wanawake pekee watakaosimamishwa na vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mwenyekiti huyo aliyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa pamoja na wadau wa uchaguzi wakati wa utoaji wa tathmini ya uandikishaji wapiga kura wapya awamu ya pili uliofanyika leo Mjini Zanzibar.
Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo punguzo hilo halitahusisha nafasi ya viti maalum kwa nafasi ya uwakilishi na Udiwani bali ni kwa wagombea wanawake majimboni na urais wa Zanzibar.
Naye Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo Thabit Idarous Faina amesema tume hiyo imetoa punguzo hiyo baada ya malalamiko ya wanawake kuhusu kiwango cha fedha kilichoweka kwa ajili ya uchukuaji wa fomu nafasi ya urais,uwakilishi na udiwani.
Amesema tume ilipokea malalamiko na ushauri uliokuwa ukitolewa na wanaharakati wa kutetea haki za wanawake na hivyo ZEC kupitia kanuni yake ya uchaguzi ya mwaka huu imetoa punguzo hiyo ikiwa chama kitasimamisha mgombea mwanamke.
Hatu hiyo ya ZEC itawahamasisha Wanawake wengi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambapo gharama za awali kabla ya punguzo ilikuwa shilingi milioni mbili kwa nafasi ya urais wa Zanzibar, shilingi laki mbili kwa uwakilishi na shilingi elfu thelasini kwa udiwani.
Gharama hizo za dharama kwa wagombea wakipata kura zaidi ya asilimia kumi, au kushinda nafasi aliyogombea au mgombea akifariki kabla ya siku ya uchaguzi fedha hizo wanarejeshewa wenyewe wagombea lakini vyenginevyo ya hivyo fedha hizo zinaingia serikalini.