Zawadi ya milioni 5 apewe Mabere Marando

Zawadi ya milioni 5 apewe Mabere Marando

hokani

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
102
Reaction score
77
Alipotekwa na kuteswa mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania Bwana Absalom Kibanda jeshi la polisi kupitia kwa kongozi wake IGP Saidi Mwema lilitangaza kwamba mtu yeyote atakayetoa taarifa kuhusu mtandao wa magaidi waliomteka na kumtesa Absalom Kibanda jeshi la polisi lingetoa shilingi milioni 5, na hakuna mtu alyewahi kujitokeza kutoa taarifa hizo; na kwa mara nyingine jeshi hilo hilo la polisi limeahidi tena kutoa zawadi ya shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zinazohusiana na mtandao uliofanya kitendo cha ugaidi kule kanisani Arusha.

Mimi napata wakati mgumu sana kuutafakari uwezo wa jeshi letu katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku (Profeshenolizimu); nasema napata taabu kwa vile polisi waliobobea katika kazi yao ya kiupolisi ya kunusa, kudadisi na kulinganisha tabia na vitendo vya uhalifu huwa hawapati taabu ya kuahidi mazawadi makubwa wakati wanajua kwamba wahusika wa matukio ya ugaidi wanajulikana, hata kama si wote lakini wale wachache wanaojulikana wakamatwe kwanza ili waisaidie polisi kuwapata wengine ambao bado majina yao hayajulikani.

Tukio la Kibanda na Dr. Ulimboka yanafana kama watoto mapacha, na kwa bahati nzuri au kama wahenga wanavyosema "Mungu si Athumani" baadhi ya watekaji na watesaji wa Dr. Ulimboka wanajulikana, na wanajulikana kulingana na taarifa zilizotolewa na muhanga mwenyewe ambaye ni Dr. Ulimboka katika nyakati tofauti! Sasa ni kwanini polisi isizihurumie pesa za walipa kodi kwa kutoa zawadi kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao kiukweli hawawezi kupatikana! Ni kwanini jeshi la polisi lichague watuhumiwa? Kitendo cha polisi kuahidi zawadi kinamaanisha kwamba watu watafute majina mengine lakini yasiwe yale yaliyotajwa na Mabere Marando au yasifanane na yake yaliyotajwa na Dr. Ulimboka mwenyewe! Ni kwanini jeshi la polisi wasiwakamate wale waliotuhumiwa na Dr. Ulimboka kwa makusudi ya kuwajua waliohusika na tukio la Kibanda?

Pia nashindwa kulielewa jeshi la polisi kwamba ni kwanini litangaze tena zawadi ya milioni 50 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kukamatwa kwa waliohusika na ugaidi wa kule kanisani Arusha wakati tayari tuna majina ya watu ambayo wamehusishwa na vitendo vya ugaidi! Naamini kama jeshi la polisi linafanya kazi kwa kuzingatia taaluma za kiupolisi na haki sawa kwa jamii watakuwa hawana budi kuwakamata mara moja watuhumiwa wa Dr. Ulimboka na wale watu 10 walituhumiwa na mwanasheria wa kujitegemea nchini Bwana Mabere Marando. Hawa wote wakikamatwa na kufanyiwa upelelezi wa kina naamini watakuwa wanawajua waliohusika na mlipuko wa bomu kule kanisani Arusha.

Hata hivyo nashangaa ni kwanini Mabere Marando asipewe zawadi yake ya milioni 55 kwa kuwataja watuhumiwa wa vitendo vya ugaidi hapa nchini!? Serikali itakuwa haijamtendea haki Mabere Marando kama watashindwa kumlipa zawadi yake hiyo ambayo mimi na watanzania wengi tunaamini kwamba anastahili kupewa haki yake. Au tungetegemea kwamba angeliwataja watu wengine mbali na hao ndipo awe amestahili kulipwa zawadi hiyo? Hata hivyo napendekeza kwamba Mabere Marando agawane zawadi hiyo na Dr. Ulimboka kwa vile naye amelisaidia jeshi la polisi pamoja na serikali kwa kuwataja baadhi ya watu waliomteka nyara na kumtesa, na majina aliyoyataja yanafanana ya yale yaliyotajwa na Mabere Marando.

Hata hivyo siamini kwamba jaji aliyemfutia Lwakatare mashitaka ya ugaidi alifanya hivyo kwa utashi wa maadili ya kazi yake au alilazimika kufanya hivyo kwa vile kesi imefika mahali ambapo itabidi lile tabaka la watawala ambalo lipo juu ya sheria na halistahili kufikishwa mahakani lilipohusishwa moja kwa moja na kesi hii; pia ikumbukwe Mabere Marando aliomba taarifa za mawasiliano za tabaka hilo zifikishwe mahakani kama vielelezo vya ushahidi wa kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Absalom Kibanda na kutengenezwa kwa video iliyomtia hatiani bwana Lwakatare kwa kesi ya ugaidi. Mimi na watanzania wengi tunaamini kwamba Lwakatare amenasuliwa na taarifa ya Mabere Marando ya kuwataja wahusika wa mtandao wa ugaidi ambao wapo juu ya sheria na kwa maana hiyo ikaonekana ni kheri kesi ya ugaidi ifutwe kuliko "Malikia" kufikishwa mahakani na kudhalilishwa mbele ya binadamu! Ndiyo maana nasema na naamini kwa vile majaji wetu tunawajua kulingana na kesi nyingi zilizowahi kufikishwa mahakani na zilizopo mahakamani, huwa hawana uhuru na lolote katika kutenda haki bali siku zote ni watu wa kusikiliza amri inayotoka kwenye lile kundi lililoko juu ya sheria.

Nimesoma kwenye magazeti rais Jakaya Kikwete akiahidi kwamba atawasaka magaidi popote walipo na atawakamata! Ni maneno mazuri sana na ya busara, lakini ni kwanini tupoteze muda na pesa za walipa kodi wa Tanzania kuhangaika kuwatafuta magaidi ambao hatuwajui na tuna uhakika kwamba hatutawapata wengine zaidi ya wale tunaowajua! Nasema hatutawapata kwa vile wale waliohusika na ugaidi wetu hapa nyumbani tulishatajiwa majina yao, na tunawajua, na wengine wanafanya kazi ofisi ya rais! Sasa inaleta hofu kwa jamii kama rais alishatajiwa kwamba baadhi ya wasaidizi wake wanahusika na vitendo vya ugaidi na hajawachukulia hatua yoyote, bali anaahidi kwamba atawatafuta magaidi popote walipo! Watanzania tunajiuliza magaidi wapi utakaowatafuta!? Je, rais anazungumzia magaidi wa matukio mengine mapya yatakayotokea au magaidi wa matukio yaliyopita!? Namuomba rais asiwaonee huruma wasaidizi wake wanaoshutumiwa na tuhuma za kigaidi; aiache sheria ichukuwe mkondo wake kwa vile wahenga wanasema "Mchelea Mwana Kulia Hilia Yeye Mwenyewe"; naiomba Serikali itumie taratibu za kasi ile ile wanayotumia kuwafikisha mbele ya sheria tabaka la watawaliwa kuwafikisha tabaka la watawala, kinyume na hivyo tunaendeleza chuki miongoni mwa jamii moja.

Mwisho napenda kuikumbusha Serikali kwamba zawadi za shilingi milioni 5 kwa atakayewataja watuhumiwa wa Kibanda apewe Mabere Marando na zawadi ya shilingi milioni 50 ya watuhumiwa wa mlipuka wa bomu kule kanisani Arusha pia apewe Mabere Marando kwa vile vitendo vya ugaidi ni vile vile na tunaamini wakitiwa nguvuni ukweli wote utapatikana kuliko kuanza kuwasingizia Al Qaida na Al Shabab mitandao ambayo haina maslahi yoyote ya ugaidi hapa nchini.

Dr. Noordin Jella
 
salaam kwa kitengo cha poli- ccm.
 
Serikali zezeta hujifanya hamnazo kwa kuziba masikio na macho inapopewa taarifa za kweli, kisha hujitangazia inatafuta ushahidi.

Hatuna serikali, Bunge la ovyo linalomilikiwa na vilaza wa ccm kila jambo - ndiyoooo, na hatuna polisi wala usalama wa taifa.

wote wameungana katika chama kimoja chama cha mafisadi - ccm, kama kawaida ya majambazi wote ukitofautiana nao wanakudhuru, ni aibu, aibu, aibu kuwa na serikali ya ovyo kama hii inayoongoza Tanzaania kwa sasa chini ya Kikwete na ccm yake.
 
Gaidi namba moja nchini ni Mwigulu Lameck Nchemba,yeye ndo anawajua wenzake wote.
 
Hata hivyo siamini kwamba jaji aliyemfutia Lwakatare mashitaka ya ugaidi alifanya hivyo kwa utashi wa maadili ya kazi yake au alilazimika kufanya hivyo kwa vile kesi imefika mahali ambapo itabidi lile tabaka la watawala ambalo lipo juu ya sheria na halistahili kufikishwa mahakani lilipohusishwa moja kwa moja na kesi hii; pia ikumbukwe Mabere Marando aliomba taarifa za mawasiliano za tabaka hilo zifikishwe mahakani kama vielelezo vya ushahidi wa kuhusiana na tukio la kutekwa kwa Absalom Kibanda na kutengenezwa kwa video iliyomtia hatiani bwana Lwakatare kwa kesi ya ugaidi.

Mimi na watanzania wengi tunaamini kwamba Lwakatare amenasuliwa na taarifa ya Mabere Marando ya kuwataja wahusika wa mtandao wa ugaidi ambao wapo juu ya sheria na kwa maana hiyo ikaonekana ni kheri kesi ya ugaidi ifutwe kuliko "Malikia" kufikishwa mahakani na kudhalilishwa mbele ya binadamu!

Ndiyo maana nasema na naamini kwa vile majaji wetu tunawajua kulingana na kesi nyingi zilizowahi kufikishwa mahakani na zilizopo mahakamani, huwa hawana uhuru na lolote katika kutenda haki bali siku zote ni watu wa kusikiliza amri inayotoka kwenye lile kundi lililoko juu ya sheria.
Dr. Noordin Jella


Mmmmmmh!... Malkia?!!!..... Nani huyu?!!!!!!!!!!!!
 
Katika mgao umemsahau Kubenea wa gazeti la Mwanahalisi!
 
Hapana mkuu, gaidi nambari moja nchini ni lwakatare ambaye ananyea debe

mahakama imemfutia Lwakatare mashitaka,MWIGULU anatakiwa Aburuzwe kortini kwa kulingana na Report ya Marando..huyu mdomo wake kila wakati Unatema Ubaguzi wa Kidini,KISIASA na Kikabila.
 
...yule mkenya wa Kovu nae katika huo mgao milio 50 wasimsau wampe angalau kifuta jasho...
 
Mkuu para ya mwisho inashabihiana na mawazo yangu... Matukio ya Kibanda, Kubenea, Dr Ulimboka, Daud Mwangosi, Igunga, Mbwambo, Padri Mushi na hili la kanisa Arusha yanalandana sana na ile kauli mbiu ya LIWALO NA LIWE kwa msaada wa watu wa marekani!!!
 
sasa mkuu mbona hao wanaotakiwa kutoa zawadi ndo wanao tuhumiwa? Yahani kitendo cha aijipii kumpa marando zawadi kinatafsiriwa kuwa polisi na usalama wa taifa wamejitangaza hadharani kuwa ndo watesaji!, (binafsi hadi sasa hiv naamini kuwa watajwa hapo juu ndo wahusika wa matukio yote ya kinyama hadi watakapo thibitisha vinginevyo) kwa kifupi hawawezi kujishtaki wala kujikamata!
 
mahakama imemfutia Lwakatare mashitaka,MWIGULU anatakiwa Aburuzwe kortini kwa kulingana na Report ya Marando..huyu mdomo wake kila wakati Unatema Ubaguzi wa Kidini,KISIASA na Kikabila.

Sio rahisi kwasasa kwani yupo juu ya sheria za nchi................kwanza ni mtanao mkubwa sana kama wafahamu mawaziri wawili wanahusika, rizi anahusika sasa itakuwaje hiyo? halafupia wakimwaga mboga yeye atamwaga ugali...........
 
Back
Top Bottom