Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,423
Mh Rais, kwanza kabisa naomba nikusalimie SHIKAMOO...Mh rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili naomba utambue Mh Rais mimi Yericko Nyerere mkulima wa Bamia Mbutu Kigamboni ninavichukia vitu viwili tu duniani, cha kwanza ni Shetani yule afahamikae na wakristu na waislamu, na cha pili naichukia CCM yani hicho chama ambacho kimekupa dhamana ya urais na ambacho wewe ni mwenyekiti wake. Hili nakuomba utambue wazi misimamo yangu kwa kuwa ni haki yangu inayolindwa kwa katiba ya nchi yangu na katiba ya ulimwengu.
Leo jumapili kama ilivyo ada yangu kukupa zawadi za weekend nataka nikupe zawadi yangu maalumu kwako Mh rais wangu kipenzi, ninatumia mitandao ya kijamii kama ukurasa wangu wa facebook, JamiiForums na twita kufikisha zawadi yangu ya jumapili kwako kwakuwa naamini wewe ni mmoja ya wasomaji wazuri wa habari za mitandaoni na ninahakika wewe ni mmoja ya "mashabiki wangu" katika kurasa zangu za mitandao kama JamiiForums, Instagram na Twita
Leo ninaiangazia serikali yako na wewe kujua na kuwajulisha wasomaji kama ni serikali ya KIDIKTETA au wewe ni DIKTETA..
Kwamjibu wa Plato, katikakitabu chake cha Jamhuri ya Plato anasema, "Serikali kwa asili ni chombo cha mabavu", yaani ni dubwashwa flani la hatari sana. Hili nakubalia nae kabisa, kwamba hata sasa ukiambiwa "kopo hili la chooni ni serikali", basi chunga sana mdomo wako, liogope hilo kopo kama ukoma.
Serikali ni neno linalotoka katika lugha ya Kiajemi "serkari", likiwa na maana ya mamlaka.
Serikali ni watu na taasisi ndani ya jamii hasa dola vyenye mamlaka ya kutawala na kufanya maazimio kwa wote katika eneo fulani. Serikali inatunza na kutekeleza sheria, kanuni na miongozo na kuendesha shughuli muhimu za umma. Shabaha kuu ya serikali ni kutunza "amani" na "usalama" wa raia katika jamii.
Kuna serikali za ngazi mbalimbali kwa mfano kwenye taifa, jimbo, mji na kijiji. Taratibu hutofautiana kati ya nchi na nchi. Katika mfumo wa shirikisho mamlaka ya serikali hugawiwa kwa kusudi kwenye ngazi mbalimbali hasa za taifa na jimbo.
Kinyume chake ni itikadi ya serikali kuu inayoweka mamlaka yote katika ngazi ya serikali kuu inayoweza kuamua kukabidhi sehemu ya madaraka yake kwa maeneo na vitengo vya kiutawala.
Kuna Serikali ya mtu mmoja au ya watu wengi, Kati ya tofauti za kwanza katika mifumo ya serikali ni swali kama mtawala wa juu awe na madaraka yote au kama anapaswa kupewa mamlaka kwa muda tu tena kwa pamoja na watu wengine.
Kuna serikali ya .Udikteta na Ufalme mwenye mamlaka yote ni mifano ya serikali ya mtu mmoja asiyebanwa na mamlaka mengine.
Katika dunia mpya Mahali pengi mfumo wa demokrasia umefaulu zaidi unaounda utawala juu ya uchaguzi wa raia wengi au wote na kukabidhi mamlaka kwa muda tu.
Hata hapa kuna tofauti kama katiba inampa mkuu wa serikali mamlaka mengi sana (kwa mfano mfumo wa Serikali ya kiraisi) au kama inagawa mamlaka zaidi kati ya watendaji na bunge (Serikali ya kibunge).
Tofauti kati ya jamhuri na serikali ya kifalme siku hizi si kubwa sana kwa sababu karibu wafalme wote hukubali Ufalme wa Kikatiba wakifuata katiba ya nchi.
Kuna Serikali katika mfumo wa mihimili ya utawala. Zamani serikali ilikuwa jina kwa mamlaka yote ya dola. Siku hizi nadharia ya mgawanyo wa madaraka inaangaliwa zaidi.
Katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka mamlaka hugawiwa kati ya mihimili mitatu ya utawala:
1. Serikali au mamlaka ya utendaji inayotekeleza sheria.
2. Bunge au mamlaka ya kutunga sheria.
3. Mahakama au mamlaka ya kuamulia sheria.
Muitaliano Niccolò di Bernardo dei Machiavelli katika kitabu chake kiitwacho The Prince anasema madaraka hudumishwa kwa damu ikibidi, hii ni dhana pana akiitazama na kuirejelea serikali ya kilatini kwa nyakati hizo alikuwa sahihi kwamba mamlaka hulindwa kwa damu. Serikali ya kilatini zama hizo ilikuwa katika tafasiri ya kwanza ya serikali niliyoieleza hapo juu, hapo ndipo uhalali wa Niccolò di Bernardo dei Machiavelli ulipo na unasimama hivyo.
Lakini kuonyesha nyakati za Machiavelli zimegota, Jean-Jacques Rousseau ananukuliwa akisema, "Maandamano ambayo matukio yake ni kumung’oa mfalme madarakani na kumnyonga ni kitendo ambacho ni cha kisheria kama kile kilichokuwa kikimleta yeye atoe hukumu la kifo au la kunyang’anya mali ya wengine"
Hii ni katika zama mpya ndipo tunapotua kwenye aina ya mwisho ya miundo ya serikali ambayo kwa namna moja ama nyingine ndio inayohudumu katika Tanzania ambapo tunakuta Serikali kuu, Bunge na Mahakama.
Miundo hii yote ili ihudumu kwa mafaa ya taifa na sio watawala inategemea sana miundo ya idara au mashirika ya kijasusi ambayo ndio injini ya tawala zote ulimwenguni, mwelekeo wa ujasusi wa taifa lolote ndio mwelekeo wa serikali yoyote.
Katika ujasusi napo hapa kumegawanyika sehemu kuu mbili muhimu, ambapo taifa likikosea au likichagua aina fulani ya ujasusi basi matokeo yake yatategemea msingi wa ujasusi huo na kuathiri jamii husika kwa ujumla.
Kuna ujasusi wa Kijeshi (Military Intelligence), huu ni mkongwe, na kuna ujasusi wa kiraia (Intelligence Agencies) , huu ni katika zama mpya za dunia mpya.
Ujasusi wa kijeshi kwa dunia ya leo umefanyiwa marekebisho ambapo hushughulika pia na mambo ya kirai sio kijeshi tu, yani hawa tunauguana nao mitaani kama walivyo wale wa ujsusi wa kirai (TISS). Tofauti yao ni kuwa uchakataji wa taarifa zao na mwisho wa maamuzi huwa katika msingi wa asili wa kijeshi (amri).
Ujasusi wa kiraia huu tangy karne ya 19 baada ya mageuzi ya dunia kuwa ya usasa, ulifanywa kuwa ndio ujasusi unaotumika kufanya maamuzi ya mwelekeo wa nchi, taarifa za hawa zilizochakatwa ndizo zilikuwa za kimaamuzi ndani ya jeshi, serikali na uchumi. Lakini kubwa kabisa ni kwamba msingi wa ujasusi huu ni utu,diplomasia, demokrasia na kinga zingine za kikatiba.
Hapo naamini sasa mwangaza tunaupata juu ya matokeo ya serikali yoyote inayoamini katika msingi wa ujasusi mpya...
Nchini China Ujasusi wa kiraia ndio unaoamua mwelekeo wa taifa hilo chini ya shirika la ujasusi la MSS, ripoti ya MSS iliyochakatwa ndio huamua mwelekeo wa Jeshi la China, Uchumi wa China na Siasa ya China. Lakini haina maana kwamba ujasusi wa kijeshi haupo au haufanyiwid kazi, bali maamuzi
ya mwelekeo wa taifa hutegemea ripoti ya MSS.
Nchini Urusi, Israel, Uingereza na Marekani maamuzi ya nchini hizo yapo chini ya mashirika ya kijasusi ambayo ni FSB, Mossad, M16 na CIA haya ni mashirika ambayo majeshi ya nchi hizo hutegemea maamuzi yake na sio majeshi yaamue mwelekeo ww mashirika hayo. Mwelekeo wa mashirika hayo ndio mwelekeo wa mataifa hayo.
Nchini Kenya maamuzi ya nchi hutegemea ripoti ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo iitwayo National Security Intelligence Service (NSIS) inayoongozwa na Maja Jenerali Philip Wachira Kameru kwa nguvu ya Apti Parati Fideles
Nchini Rwanda maamuzi ya mwelekeo hufanywa chini ya ujasusi wa kijeshi chini Directorate of Military Intelligence (DMI). Hali hiyo inaifanya idara ya ujasusi ya Rwanda ya National Intelligence and Security Services ( NISS) kufanya kazi chini muongozo wa DMI.
Namna ya kuchagua mifumo hii ni aina tu ya mtawala anayeongoza serikali katika wakati huo ndio huamua, hii inatokana na namna anavyopenda kuiongozia serikali yake hakuna tatizo kwakuwa vyombo vyote katika nchi ni vya ujasusi vinavyofanya kazi kwaajili ya taifa husika.
Utatambua kwamba ni ujasusi wa kijeshi unaoongoza nchi kwakuangalia mambo makuu mawili 1. Amri za kiutawala na 2. Nafasi za uteuzi (kirais). Haya yanamaana sana katika kutazama mambo haya. Faida na hasara zake nimeshaziainisha hapo mwanzo. Kimsingi ujasusi wa kijeshi unapingana na demokrasia, siasa za wengi wape, uhuru wa kumwambia mfalme upo uchi, wala kuhoji chochote, kwanamna moja ni utawala unaozingatia sauti ya sponsor tu.
Nchini Tanzania vivyo hivyo kuna ujasusi wa kijeshi na ujasusi wa kiraia. Ni wajibu wako kutambua ni ujasusi upi unaoongoza taifa, faida na hasara zake...
Nakutakia jumapili njema mheshimiwa rais John Pombe Magufuli udumu katika fikra zako.
Adui yako ni yule umuaminiye ama hata kumvisha na kumlisha...
Na Yericko Nyerere