Zarina Madabida alishukia gazeti la Nipashe

Zarina Madabida alishukia gazeti la Nipashe

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,633
Reaction score
7,021
Akichangia katika hotuba ya bajeti ya WAUJ,amewachana Tfda kutokana na hujuma zao zilizosababisha kuua viwanda vya dawa nchini.Kama vile haitoshi,amesema kuwa alihujumiwa na hao Tfda wakihusika kusema kuwa wamemkamata na sukari ya kutengenezea ARV iliyo expire.

Habari iliyoripotiwa na gazeti la Nipashe aliloliita la 'Kizandiki,waongo na washonganishi wakubwa'huku ukweli ikiwa ni kwamba hakuna ARVInayotengenezwa kwa sukari katika kiwanda cha dawa anachomiliki hisa huku serikali ikiwa na hisa nyingi zaidi ambazo ni 40%

My take;
Tfda inapaswa kuchunguzwa kutokana na kuwa na tuhuma nyingi nzito,ikiwa ni pamoja na kutoa vyeti vya kuhitimu ADDO kwa watu ambao hawakupitia mafunzo kwa rushwa ya hadi shilingi laki nane kupitia kwa baadhi ya wafamasia wa wilaya pamoja na kumiliki mafamasi huku wao wakiwa wakaguzi na wakiyaacha maduka yao yakivunja sheria wazi wazi.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Akitumia wasaa aliopewa na naibu spika mbunge wa kuteuliwa Mrs Zarina Madabida amelishutumu vikali gazeti la nipashe kwa kusema ni gazeti linaloleta uchochezi.

Huku akiwa amelishika gazeti hilo amelishutumu kuhusiana na habari yake juu ya matumizi ya sukari kutengeneza ARV. Amekanusha vikali kuwa hakuna ARV zinazotengenezwa kwa sukari.

Ameenda mbali na kusema kama nipashe ni gazeti linalosupport chama flani lijiweke wazi.

Kazi kwenu Nipashe.
 
amenishangaza zaidi aliposema haungi mkono hoja na akawa anawaponda wapinzani

haeleweki yuko upande upi zaidi haelezi bayana kwa kujenga hoja za kwa nini anaikataa hoja ya serikali
 
Vyakula vya watu tu hawana kitu ni midomo tu basi. kichwani hakuna kitu kabisa
 
Ukieleza ukweli bongo lazima uwe chama fulani....!
 
naona anasafisha jina la kiwanda chake na kuchafua jina la nipashe
 
Kama ni uongo kwanini Kiwanda chao ( TPI ) kimefungiwa ? Hawa viti maalum ni bora Wafutiliwe mbali kabisa , tena Mwambieni aishie hapohapo kabla hatujafumua Mauchafu mengine mubaki midomo wazi !
 
Kama ni uongo kwanini Kiwanda chao ( TPI ) kimefungiwa ? Hawa viti maalum ni bora Wafutiliwe mbali kabisa , tena Mwambieni aishie hapohapo kabla hatujafumua Mauchafu mengine mubaki midomo wazi !
kwa jinsi alivyoeleza leo ina maana TFDA wana chuki na kiwanda chake(serikali inamiliki 40%)
 
Makamba Sr aliwahi kunukuliwa akiwaambia wafanyabishara kuwa wakitaka mambo yao yafanikiwe lazima wajiunge CCM!... Sasa hawa wauaji waliotengeneza ARV feki nao wanatoa karipio kwa waliofichua hujma zao badala ya kuwaomba msamaha Watanzania...
Huu ujasiri wa kuwasababishia vifo raia wa nchi kisha kuwachimba mkwara mbuzi vyombo vya habari wanaitoa wapi? baada ya 2015 watakimbilia wapi?...
 
Conflict of interest- ana kiwanda cha madawa kinachotuhumiwa kufanya maovu

Mumewe ndio mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam,.Huyu mama ni tapeli mkubwa yeye na mumewe wamekopa pesa nyingi sana NSSF na PSPF kwa kutumia mgongo wa serikali na kiwanda cha dawa feki , hadi leo hawajalipa madeni hayo , wameamua kutumia siasa ndani ya CCM kama kinga ya madhambi yao, shame.
 
hajielewi huyo,hao ndo moja wabunge wanaochaguliwa kwa kigezo cha kujitoa uthamani
 
kwa jinsi alivyoeleza leo ina maana TFDA wana chuki na kiwanda chake(serikali inamiliki 40%)

Huyo mama si mtu wa kumuamini hata kidogo , inafahamika kwamba TFDA wana mapungufu , lakini kwanini Zarina ameamua kuyasema Leo , kauli yake ya Mwanzo haikuwa hii , hebu kumbuka ! Amefundishwa , ni mnafiki aliyehamasisha kuhamisha majukumu ya TFDA kwenda PHARMACY BOARD ( kwa Chuki tu ), hadi sasa wanashindwa kabisa kuyafuatilia waliyang'ang'ania ! Kumbe yeye ndiyo ana Bifu na TFDA tena bila sababu ya Msingi, yapo mengi sana kaka , kwa leo tuishie hapa , Angalizo , natamka kwamba sina upande wowote ninaofaidika nao katika hili , kwa hiyo isichukuliwe kama nina maslahi yoyote .
 
Mie sijaelewa maana inaweza ikawa hoja muhimu lakini haya majinga ya humu yanapenda kupotosha mpaka unashindwa kutoa mchango mzuri.
 
huyu mama ana shingo ngumu kama kinana badala ya kuomba msamaha na kujiuzuru ubunge anakuja na orodha ndefu ya fallacies
 
Makamba Sr aliwahi kunukuliwa akiwaambia wafanyabishara kuwa wakitaka mambo yao yafanikiwe lazima wajiunge CCM!... Sasa hawa wauaji waliotengeneza ARV feki nao wanatoa karipio kwa waliofichua hujma zao badala ya kuwaomba msamaha Watanzania...
Huu ujasiri wa kuwasababishia vifo raia wa nchi kisha kuwachimba mkwara mbuzi vyombo vya habari wanaitoa wapi? baada ya 2015 watakimbilia wapi?...

Hakuwa Makamba Sr...That was Fredrick Truway Sumaye
 
Akitumia wasaa aliopewa na naibu spika mbunge wa kuteuliwa Mrs Zarina Madabida amelishutumu vikali gazeti la nipashe kwa kusema ni gazeti linaloleta uchochezi.

Huku akiwa amelishika gazeti hilo amelishutumu kuhusiana na habari yake juu ya matumizi ya sukari kutengeneza ARV. Amekanusha vikali kuwa hakuna ARV zinazotengenezwa kwa sukari.

Ameenda mbali na kusema kama nipashe ni gazeti linalosupport chama flani lijiweke wazi.

Kazi kwenu Nipashe.
Chama na interest yake binafsi wapi na wapi. Labda ameingia bungeni kama mahakama kujitetea... Bungeni ni mahali pa kutetea maslahi ya wananchi, ukiona mbunge anajitetea bungeni ujue wananchi wamekosea kumchagua.
 
Mie sijaelewa maana inaweza ikawa hoja muhimu lakini haya majinga ya humu yanapenda kupotosha mpaka unashindwa kutoa mchango mzuri.
Haaaahahah..., majinga ya humu ni pamoja na wewe? Sasa tulia mkuu toa hoja yako basi, huku jf kila mtu anateleza tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom