Zari anaposema tatizo ni Diamond, hii ndio maana yake

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Watu wengi wanashindwa kumuelewa Zari anaposema tatizo ni Chibu yani Diamond.

Ali Kiba akitoa wimbo mashabiki wake wanakimbilia kwenye page za Diamond au watu wa karibu yake kulazimisha wausapoti uwezi kuwaona kwa wasio mhusu.

Diamond akipata dili ya tangazo wanaibuka watetezi feki wa haki za wanawake na kulia kwa uchungu kwa nini apewe tangazo ilihali anadhalilisha wanawake! Ukiuliza kamdhalilisha nani? Watakwambia Wema. Kivipi? Hakuna majibu ya msingi.

Tuzo zikitangazwa duniani kote lisipokuwepo jina la Diamond zinapita kimya kimya.. Likiwepo jina lake inaanzishwa kampeni kumpigia kura mnaijeria yoyote ili kumpa upinzani Chibu.

Diamond akisaidia wasanii wachanga kwao sio habari nzuri. Diamond akijenga msikiti kwao sio habari nzuri. Diamond akisaidia mashuleni kwao sio habari nzuri.. Diamond akifanya wimbo na mnaijeria na akitolea video south Africa.. Utasikia sioni kwa nini wasanii wanakimbilia kufanya video nje, mara muziki wetu unakuwa wa kinaijeria.. Kesho nao unasikia wamepanda ndege kufanyia video South Africa au wanafurahi wamepata collabo na mnaijeria.. Kwa Diamond muziki unakufa, wao wakivuka boda muziki unakuwa.

Lazima tukubali Diamond kwa sasa ndio daraja letu la kuivusha bongo fleva.. Wapo wasanii wamefanya makubwa kuufikisha huu muziki hapa kina Prof J, AY, Sugu nk lakini kiukweli Diamond amekuja kufanya mapinduzi makubwa mno. Kuna watu walifanya harakati nyingi kuubadili muziki umlipe zaidi msanii wengine waliishia kutukana matusi na ubabe ila Diamond katumia njia za kisayansi kuibadili game yetu na kiukweli game kaibadili mno ata km atupendi kukubali hili. Vitu wanavyofanya na njia wanazopita sasa yeye ametoka huko miaka 4 iliyopita.

Wakati Kiba anafurahi kusainiwa label ya kimataifa. Diamond anapambana kuipeleka label yake kuwa ya kimataifa, baada ya miaka mitatu wengi ndio mtaelewa tofauti ya Chibu na wengine.

Mtamchukia Tiffa, Zari, Babu Tale, Sallam, Fella, Kifesi lakini awa ni kafara tu ishu hapa ni Diamond. Awa wangekuwa mtaani huko awausiki na mafanikio ya Diamond wasingekuwa tatizo.

Ata ugomvi wa kifamilia kati ya Esma, mama Diamond na Zari ishu sio Zari anajisikia ishu ni Diamond kashindwa kubalansi upendo, upendo umeelemea kwa Zari na Tiffa.. Mama na dada wanaona ule umiliki wa imaya unapungua siunajua tena mambo yetu waswahili kukaba ata kama mtu kashaanza maisha ya familia . Kwa hiyo jamani kelele zooote tatizo ni Chibu.
 
diamond kakuta tayari mziki wa bongo unajulikana kimataifa hajaitangaza tz kiivyo kama unavyodhania!!sema tuko kwenye wakati mzuri wa youtube,WhatsApp,fb nk sasa kuwa known kimataifa ni wakati kidogo tu
 
Muziki wetu ulikuwa unajulikana kupitia msanii gani? Na ulipenya nchi gani?
 
Mkuu unaongea ukweli mtupu naishi apa sauzi eastern cap yani mademu waki xhosa wanapenda mziki wa Diamond sana
 
QUOTE="mr gentleman, post: 16267187, member: 95717"]Muziki wetu ulikuwa unajulikana kupitia msanii gani? Na ulipenya nchi gani?[/QUOTE]
ay,saida,jayd walikuwa nominated tuzo za kora wakati huo
 
Kwa mtizamo wangu c kwamba watu hawaoni alichokifanya chibu na anachiendelea kufanya au alichokifanya kiba na wasanii wengine kuufikisha muziki wa bongo hapa,shida kuu inayotafuna ni mambo ya utimu utimu haya.
Mtu atazungumzia vibaya flan kwa sababu yeye ni timu flan,mi nadhan muziki wa bongo ni wa bongo wote so kuko na kila haja ya kutokuwa na haya makundi.
 
huyo diamond wako sio wa kwanza kufanya collabo na mnigeria, wala si wa kwanza kushoot sa hata usa hakuanza yeye, huyu diamond kashawapa limbwata wengi akina nyie
 
huyo diamond wako sio wa kwanza kufanya collabo na mnigeria, wala si wa kwanza kushoot sa hata usa hakuanza yeye, huyu diamond kashawapa limbwata wengi akina nyie
Members wa JF hatuongei hivi,tunaongea hoja si msuto, sasa ngoja nikuongoze jinsi ilivyotakiwa uongee. 1.Kama DIAMOND si msanii wa kwanza kufanya colabo na wanaija leta wewe huyo wa kwanza na nyimbo yake ilifika katika levo vipi za ubora kimataifa ............... 2. Lete huyo msanii wa kwanza kushoot S.A na US na nyimbo yake/zao zilikuwa zinachezwa kwenye tv zipi za kimataifa na zilikuwa zinashika nafasi zipi za juu ............... Kwahiyo unatuambia kuwa ukinusulika na "limbwata" la DIAMOND ndio unakuwa na chuki za kijinga na kipumbavu zilizokosa hoja kama hizi zako si ndio ???????
 
wewe waangalia levo za kimataifa, hushawahi kuhudhuria kwenye hayo mataifa au unanidhihishia kuwa nawe ndo wale wale?
watazama vituo vya tv kuliko kutazama kaimba nini na hayo mataifa yanamuelewa ama la. hivi diamond anazifkia levo hata za akina fa, ay, na jide mbona ay na jide walishafanya hizo mambo kitambo. TATIZO MNAMFUATILIA MOND KULIKO BONGO FL
 
sijasema namchukia diamond, ila uzembe wenu wa kumuona diamond mkubwa na kumtukuza ndo vitu vinaniboa mimi ninaeujua mziki huu kabla ya diamond, kama unaujua na kuufatilia mzk huu hutabishana na mimi, kuna watu wame cross border na kuitangaza tz zaid ya huyu jamaa labda kipind hcho hamkuwa na hata radio,
 
Nonsense...
Zari aliweka picha akisema "tatizo sio Tee mbaya,tatizo ni chibu"
Haya maelezo yote nilifikiri utaongelea hilo,pumba tupu.
Kama huna huna cha kupost kaa kimya.
 
wewe waangalia levo za kimataifa, hushawahi kuhudhuria kwenye hayo mataifa au unanidhihishia kuwa nawe ndo wale wale?
watazama vituo vya tv kuliko kutazama kaimba nini na hayo mataifa yanamuelewa ama la. hivi diamond anazifkia levo hata za akina fa, ay, na jide mbona ay na jide walishafanya hizo mambo kitambo. TATIZO MNAMFUATILIA MOND KULIKO BONGO FL
Mkuu nakufagilia sana umeongea pointi, sasa mwalimu wangu mimi nina swali dogo tu, hao uliowataja hapo kwenye red umewapima kwa vigezo vipi yaani uniambia wamefanya hiki na kile na kile na kile ....................... ( unitajie vigezo vinavyotumika kimataifa vya kupima wasanii "MSANII ALIYE JUU YA MWENGINE/ WENGINE" na kwa vile umesema unaujua sana huu muziki bila shaka hata vipimo vya kimataifa unavijua. ) Maana kama ni kusema tu hata mimi naweza kusema kuwa Harmonize yuko juu ya Kiba, ila ukiniuliza kwa vigezo gani ndio natakiwa niviainishe sasa wewe mkufunzi wangu hebu nisaidie kwa hili.
 
Back
Top Bottom