Zanzibari chonde chonde

Zanzibari chonde chonde

haya mtapewa talaka mnoitaka, mupumue vizuri.
 
na wewe uache andika sentensi za kipuuzi, dora ndo nini.
 
Wanaowashawishi Wazanzibar waichukie Bara na Viongozi mafisadi wanaojaribu kuvuruga mambo ili yao yasizungumzwe
 
sasa hayo si ndo matatizo ya kukaa pamoja mezani na kuyarekebisha, mbona mambo madogo tu.
 
ni mawazo ya mwarimu.
nani kakwambia (ukiondoa waislamu), wacha udini bwashee, bara kambarage anaheshimika na kila dini kila mtu, me muislamu yakhe
 
Mi nataka hata Leo muungano uvunjike hawa ma mwinyi waende zao!! Tuinjenge Tanganyika vzr
 
Ebu acha upumbavu wako msijitenge msijitenge ndo nini ? kWANI NYERERE kAMA NANI ? Tunataka zanzibar yenye mamlaka kamili, tutakutana EAC bado haitoshi ?? Kwani tukijitenga hivi siviwa tutaviondoa ? Vitababkia hapa hapa wala havitaenda popote kama udugu utakuwepo kama vile watanganika na wakenya, burundi, msumbiji, na kwengine, ujirani unatoshaa.
Msiijtinge msijitenge msijitenge nasema msijitenge.
1. Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu, hizi dosari ni za kukaa na viongozi na kuelekezana wapi parekebishwe sio kujitenga,

2. Dhambi ya ataetaka jitenga itamuandama siku zote alisema mwalimu.

3. scientifically proved kina cha maji kinazidi panda bcoz of kupanda kwa joto inosababisha melting ya mabarafu, zanzibar is amongst visiwa vyenye tishioa la kumezwa na maji, watu washapima pembezoni mwa fukwe zenu, zenji inazama mdo mdo, kama una bisha google, where will thy grandsons & daughters shelter themselves, hao wageni wanowahimiza mjitenge wana pa kukimbilia, nyinyi wabantu je?

4. Haya mnajitenga na bara mu watu wamoja now against an enemy tanganyika vidole vyote mnatu point sisi wabara ndo wabaya, mnasahau vitatu vinawapoint nyinyi, nani asiejua pemba na unguja hamuivi chungu kimoja, eti bara iliwagawa ikawatawala, kweli? haya tutaona.

5. Kidole kimoja hakiui chawa, wanowaambia mtakuwa better mkishajitenga wanawadanganya fungueni macho yenu na akili, umeme umeshaletwa, infrastructure inaboreshwa, tourists company zenu zinashirikiana vizuri sana na za kaskazini mkawaulize mambo yalivyo na yanavyozidi kuwa murua upande wao, uvuvi wanashirikiana vizuri sana na dar mtwara tanga hadi kigoma na mambo kibao, katiba hii hapa semeni dukuduku zote sio kujitenga,
siasa siasa siasa inawapoteza wandugu look at de other side of the coin, the future is looking good when we together, matatizo haya tujumuike tuya sought out pamoja, hata uswisi wana matatizo kila mahali kuna matatizo kuyakimbia is not a solution, eti hatuingiliani kiutamaduni that is bloody nonsense, dunia ya sasa inakuwa moja, ts all abt business, wanoungana wana nguvu sana angalia amerika, eu hiyo inakuja, nyie mwataka kimbia? come on fellas.

sijaoa huko sina ndugu wala sijawai kufika. ni mawazo yangu tu na mengine mengi sana ya kusema, muda tu hautoshi. Ila zenji honestly think twice mazee,
If u still insist kujitenga, obviously you will, go on wanasemaga mtoto akililia wembe mpatie.
 
Uko sahihi sana,lazima tuulinde na kuutetea muungano wetu,wanaotaka kutuvuruga sharti tuwapige
 
------- mwenyewe,
chapeni lapa hatutaki mbivu zenu
 
wacha udini bwashee, bara kambarage anaheshimika na kila dini kila mtu, me muislamu yakhe
Ndio maana tunawaambia kuwa mnaubudu nyerere! ni mtu gani duniani anayeheshimika na kila mtu na kila dini?!

Mimi ni Mtanganyika na nyerere hana sharafu yoyote kwangu mimi.

kweli kuna haja ya kuungana na watu wanaongozwa na mfu kaburini (si watanganyika wote)?
 
Wazanzibar wana haki ya kuamua hatma yao bila kuingiliwa wala kutishiwa na mtu awaye yote. Umefanya vyema kunukuu mawazo ya mmoja wa waanzilishi wa muungano Ndugu Julius Kambarage Nyerere. Unaonaje ukitoa nukuu kama hizo zinazoakisi mawazo ya muanzilishi mwenza wa muungano wa upande wa Zanzibar yaani Ndugu Abeid Aman Karume.
 
unayosema ni kweli.....ila swali la kujiuliza ni kwa nini zanzibar ilijiunga na ndani ya muungano huo kwa hiari na kwa nderemo ieweje leo....hawataki tena na wamechoka....ukipata jawabu kwa nini basi uta support movement yao hata kama ni mtanganyika....
lakini moja ya mambo yanayo udhi ni dharau
pili ....wanapo engea kuwa kuna mambo ambayo yanadhoofisha uchumi wao..basi tanganyika hawataki kuwasikiliza tena..ni kama vile umeshaingia ndani ya kitanzi basi utakoma...mpaka ufe
kuna mfano wa suala la gasi na petroli....haya masuala sio ya kugombana lakini upande wa tanganyika hauna nia nzuri na unaonesha umimi. zaidi na ubabe.....mathalan mafuta ya zanzibar tanganyika wangekubali yaliyopo zanzibar yachimbwe na zanzibar kuendesha uchumi wake.....na viyu kama hivo

so sio suala la utengano bali ...dharau...
hivo kama kuzama na vizame ila utu,uhuru na heshima ya nchi na watu wake ni bora hata kama nchi itakua masikini wa kutupwa.....
 
"huwezi kabisa kulinganisha muungano wa usa au eu na huu wetu hapa. Nakukubalia kwa vile hujawahi hatakuja huku, unaongozwa sanana hisia zako, mimi ninayeandika hapa ni muunguja 100%, na ni muumuni wa muungano wa "mkataba" ama na tuuvunje kabisa tukae kama majirani wema, ama ni baya hile, maana wenzetu mnaona kudai haki yetu imekuwa kama nongwa ..... Tuna kila sababu na ni haki yetu"
nenda mwana kwenda
 
Back
Top Bottom