zanzibar yatetea usajili wa meli ya iran

sabasita

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
1,501
392

amka2.gif
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema kuwa usajili uliofanywa kwa meli za mafuta hivi karibuni, umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa zile inazosajili nje ya nchi.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad, wakati akitoa taarifa rasmi katika Baraza la Wawakilishi huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Alisema kuwa alilazimika kutoa taarifa hiyo ili kutoa usahihi wa uvumi kwamba Zanzibar imesajili meli za Iran ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.
Hamad alisema kuwa Juni 27 mwaka huu, vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania, viliandika makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta.
Katika habari hizo ilidaiwa kuwa meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na kampuni ya serikali ya Iran.
“Taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yoyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu,” alisema waziri huyo.
Hamad aliongeza kuwa katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa.
Alisema kuwa usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) kupitia wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za abiria.

 
We subiri, likipigwa bomu moja tu atasema ukweli!...URAFI TU!
 
Back
Top Bottom