Zanzibar Yadai Uhuru 2017

Madafu

Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
14
Reaction score
22
Baada ya wiki mbili kutoka sasa, (tarehe 10 Disemba 2016) inafika siku ya Uhuru wa Zanzibar, siku ya Zanzibar kujigomboa na makucha ya ukoloni wa Kingereza mwaka 1963. Kwa muda ya miaka 53 tumesahaulishwa siku hii tukufu ambayo walishirikiana wazee wetu wa pande zote za siasa na makundi ya kabila zote na tabaka zote kupigania Uhuru na wakasherehekea pamoja tarehe 10 Disemba 1963. Leo siku hii tukufu haisherehekewi Zanzibar wala hapana kiongozi yeyote aneitaja siku hii, si CCM wala si CUF. Anakuja kijogoo cha Bara Tundu Lissu kuwafundisha vizazi vipya vya Zanzibar kwamba nchi yao ilipata Uhuru kutokana na utawala wa ukoloni wa Kingereza tarehe 10 Disemba 1963.

Baada ya kupita miezi minne kutoka siku ya Uhuru (26 Aprili 1964), Zanzibar ilipoteza Uharu wake kwa kuingia kwenye makucha ya mtawala mpya na kugeuka kuwa sehemu ndogo ya jamhuri mpya ya Tanzania. Tokea hapo 1964 mpaka hii leo nchi yetu ya Zanzibar haijasita kudai iwe na haki Zaidi katika huu utawala wa ukoloni mpya wa mabavu unaoitwa Muungano wa Tanzania. Mzee Rais Abeid Amani Karume kapoteza roho yake huku anajaribu kulivua koti la Muungano lililokua linaibana Zanzibar. Si siri kwamba Sheikh Karume alifika kuwa hasemi na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa sibabu karume anataka kutokana na Muungano. Nyerere akamuweka Alhajj Aboud Jumbe kushika pahala pa Sheikh Karume. Rais Alhajj Aboud Jumbe nae akataka kutokana na maonevu ya Muungano. Nyerere akawatumia vibaraka vyake kutoka Zanzibar kumfitini Rais Alhajj Aboud Jumbe akaishia kufukuzwa kwa adhara na kashfa.

Miaka michache iliyopita alisimama mwana halisi wa Zanzibar Sheikh Farid na Mashekhe wenziwe wa Uamsho wakadai Uhuru kamili wa Zanzibar. Leo Mashekhe hao wametupwa gerezani na kuadhibiwa na kunajisiwa kwa sibabu ya mapenzi yao ya Uhuru wa Zanzibar yao. Badili ya kudai Mashekhe wa Ukawa watolewe kifungoni, anasimama mwanasiasa anawakejeli kua “leo wako jela wanakunya kwenye ndoo”. Aibu gani Zanzibar kua na wanasiasa kama hawa?

Jitihada ya kudai Uhuru wa Zanzibar zimeendelea baina ya wananchi wa Zanzibar miaka yote iliopita. Wananchi wamechoka na utawala wa kikoloni wa Tanganyika. Kwa bahati mbaya viongozi wa Zanzibar hawakuthubutu kupeleka mbele matakwa ya wananchi. Badala yake wakawa wanababaisha wanachi kwa kudai serikali tatu au mengineo. Hapana kiongozi yeyote Zanzibar anaethubutu kuisemea nchi yake na kudai Uhuru wa Zanzibar kama anavyo isemea Zanzibar kijogoo cha Tanzania Bara Tundu Lissu.

Sasa imefika wakati wanasiasa wa Zanzibar washughlikie matakwa ya Wazanzibari kudai Uhuru wao kutokana na Muungano. Wananchi hatutaki Muungano. Wanasiasa wa CCM na CUF ama watuunge mkono kudai Uhuru wetu kamili mwaka 2017 au wawe tayari kutupwa na wananchi kwenye madebe ya taka ya historia.
 
Bado hamna uwezo wa kujitawala subirini mpaka mambo yatakapo kaa sawa
 
Ile kesi mliofungua kupinga muungano imeishia wapi?
Tulimabiwa na Sefu jini ameshapanda kichwani,karibu atataja jina,ndio hilo la kudai uhuru?
 
Mambo taratibu.

1. Ilikuwa siyo nchi, sasa ni nchi.
2. Rais wa JMT akienda zenji, anapokelewa kama rais mgeni.
3. Mna shirika lenu la hbr
4. Mna mamlaka yenu ya kodi.
5. Mmetunga sheria ya mafuta na gesi kuwa si mambo ya muungano, ni yenu pekee, hakuna aliyewakatalia.
6. Mna ligi yenu huko. Kazaneni muingie kwenye FA na CUF
7. Tanganyika ni kwenu lkn mtanganyika zenji sio kwao.
8. Bado vichache sana lkn hadi sasa hamna sababu ya kulalamika. Mmekamilka

Ushauri. Anzeni kuunda shirika lenu la umeme. Ipo siku tutawakatia umeme, hafu nasikia mmehongwa hamlipii chochote
 
Hamna haki ya kujitawala kama mnataka uhuru acheni kupiga poroja mitandaoni ingieni barabarani kudai uhuru tuwatengue miguu watu gani hamna shukrani mnabebwa hambebeki
 
Kila jambo lina mwanzo na mwisho...mie kwa maoni yangu....ipo siku hata nchi kubwa kama marekani zitagawanyika....seuze zanzibar...ni muda tu!
 
Hawa dawa yao ni kuwapelekea wakurya kule wakaishi halafu wawachokoze........maana wakurya si watu wa kuwaletea ujinga ujinga mbura.......
 
Kama
Mungesitisha kuwalipa IPTL kwanza ndio mupate ubavu wa kuwakatia Zanzibar umeme. Simply put it this way, ushawahi kuona mtu aliyejenga nyumba Kariakoo kwa ubia kulipishwa kodi, let alone kufukuzwa ndani ya jengo?
 
Naunga mkono hoja 100%

Sent from mTalk
 
Mi nahisi tatizo la muungano linasababishwa na usiri wa muungano wenyewe. Ni wachache sana wanaojua uhalisia wa makubaliano ya muungano na hawako tayari mwengine kujua.

Je ni nani hasa anamuhitaji mwenzake zaidi, kati ya Tanganyika na Zanzibar?

Kwa nini Zanzibar waone wanakaliwa kimabavu na Tanganyika?

Kwa mtazamo wangu hakuna lenye mwanzo lisilokua na mwishp kama watu wanaoana kwa ndoa halali na mapenzi mwishowe wanaachana. Iitishwe kura ya maoni kuuliza wanaotaka na wasiotaka muungano watu wafanye maamuzi wanayoyapenda.

Kusema Zanzibar hawajawa tayari sidhani kama Tanganyika tunamapenzi ya kiasi hicho kwa wazanzibari mpaka tuhofie ustawi wao wakitoka ktk muungano. Kwanza hizi ni nchi huru zilizoungana na sio nchi moja kuitawala nyengine kea kuiandaa baadae ije ijitawalr
 
Nataka kiwanja hapo Unguja mimi ni mnyamwezi nakuja wiki ijayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…