J.K.Rayhope
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 316
- 31
Wakuu wa jamvi,habari!Natumai wote hamjambo.Nimekuwa na maswali mengi kichwani kuhusu Zanzibar na muungano kwa ujumla.Kwa wale wenye kumbukumbu chokochoko za muungano zinazidi kuongezeka kila mwaka na kila awamu ya urais inapoingia,ni wazi kwamba yapo mambo ya msingi ambayo Wazanzibari wanahitaji.Inawezekana serikali zote 2 zinayapuuza na kuyaona ni ya "kitoto" lakini kwa ulimwengu tulionao kiongozi hapaswi kuziba masikio.Kwa maoni yangu,siyo kuanza kuuunda tume za kiintelijensia,kiongozi mwenyewe,toka ofisini,kaulize kunani huko.Chonde MwanaJF kama unafahamu hata kiduchu kwamba wazanzibar wanataka nini hasa,tujuze tupate kujua.Mungu tusamehe Tanzania,tumeanza kuchoma hata madhabahu yako.Tusamehe na utupe roho wa kutuongoza tuishi kwa amani.Aaamen.
Acha unafiki huo,hakuna wenye asili ya kiarabu wala kichina hapa zanzibar,wanao dai nchi huru ni wazanzibari wenye asili zote,alimuradi ni mzanzibari. mnafiki mkubwa.Ni kweli kuna kero za Muungano zinazofahamika na ilidhaniwa kuwa kupatikana kwa Serekali ya Umoja wa Kitaifa Kungekuwa Mwanzo wa kuanza kuzishughulikia Rasmi, kwani kabla ya mwafaka huo Viongozi wakisiasa na wafuasi wao Walikuwa hawaaminiani na kulikuwa na uadui wa wazi kati yao.
Kilichozuka sasa ni Wimbi la Tamaa likiongozwa na Wazanzibari wenye Asili ya Kiarabu kua Wana visima 72 vya Mafuta ya Petroli yaani Utajiri mkubwa Mno Utakaomkomboa kila Mzanzibari lakini Uko HATARINI kuporwa na Watanganyika. Hivyo UAMSHO wanawataarisha Wananchi wenzao kwa mapambano hivyo wawe tayari kufa kupigania Mafuta yao. Kwa hiyo mkuu kinachohitajika na Wazanzibariiii ni UTAJIRI WA MAFUTA. na kiongozi wao amewahakikishi VISIMA 72. Watapeta au vipi?
Acha unafiki huo,hakuna wenye asili ya kiarabu wala kichina hapa zanzibar,wanao dai nchi huru ni wazanzibari wenye asili zote,alimuradi ni mzanzibari. mnafiki mkubwa.
Ukweli wananchi wameshaonesha hisia zao za vitendo kuwa muungano hawaitaki,muungano tulio nao ni wa Tanu na ASP= CCM.mkuu kama kuna kitu unakifahamu si ufunguke ili watu tuweze kujua?? Kuliko kubweta,kulalama na kutokwa na povu kwenye coment za watu??
Hembu tumegee ukweli halisi basi
Acha unafiki huo,hakuna wenye asili ya kiarabu wala kichina hapa zanzibar,wanao dai nchi huru ni wazanzibari wenye asili zote,alimuradi ni mzanzibari. mnafiki mkubwa.
Ukweli wananchi wameshaonesha hisia zao za vitendo kuwa muungano hawaitaki,muungano tulio nao ni wa Tanu na ASP= CCM.
Huo ndio ukweli,viongozi ndio wenye muungano,lakini wananchi ndani ya nyoyo zao hawana muungano,sio zanzibar hata huko tanganyika.