Zanzibar wadai mgawo wa madini

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
SUALA la mgawanyo wa rasilimali zinazohesabika kuwa ni za Muungano, linazidi kuchukua sura mpya kila siku na sasa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) wanataka Zanzibar ipatiwe mgawo kutokana na mapato ya madini kabla ya kuanza kuchimbwa kwa mafuta ya Zanzibar.

Waliyaeleza hayo jana wakati wakichangia bajeti ya Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, Mansour Yussuf Himid.

Waziri kivuli wa wizara hiyo, Hamad Masoud, alisema kwamba ni jambo la kushangaza kuwa Zanzibar haikushirikishwa wakati Tanzania Bara inafanya utafiti wa rasilimali ya mafuta na gesi.

Alisema kwamba Serikali ya Muungano ilipaswa kutafuta mshauri wa kuweka utaratibu wa mgawo wa maliasili za madini, lakini jambo hilo halikufanyika na badala yake linafanyika katika kutafuta mafuta ya Zanzibar.

“Leo hii kwa kuwa kuna uvumi wa dalili ya kuwepo mafuta Zanzibar, ndiyo Serikali ya Muungano imetanabahi na kutushirikisha,” alisema.
Masoud alisema kwamba ni vyema Waziri Kiongozi akatoa hoja kwa Waziri Mkuu katika vikao vyao kuwa, Zanzibar nayo ipate mgawo kutokana na mapato yanayotokana na madini yanayochimbwa Tanzania Bara, tangu uchimbaji ulipoanza.

“Hili litawathibitishia Wazanzibari kwamba wenzetu walighafilika na walipotanabahishwa walitenda haki kwa kuwapa Wazanzibari fungu lao,” alisema Masoud ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole.

Alisema kwamba kambi ya upinzani haina nia ya kuvunja Muungano, bali inatetea maslahi ya Zanzibar kwa manufaa ya wananchi.
“Tabia ya wenzetu ya chao kuwa chao peke yao na cha Zanzibar kuwa cha pamoja, ni tabia iliyodumu kwa zaidi ya miaka 40,” alisema.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Tumbe, Ali Mohammed Bakar (CUF), alisema kwamba mafuta ya Zanzibar yaondoshwe na yasiwe katika orodha ya mambo ya Muungano kwa vile ni maliasili ya Zanzibar.

“Kama mafuta yataingizwa katika mambo ya Muungano, basi na madini yote yawe katika orodha hiyo ya mambo ya Muungano,” alisema mwakilishi huyo.

Alisema kwamba Wazanzibari wanayo mapenzi na watu wa Bara, hasa kwa kuzingatia hivi sasa ni ndugu wa damu, lakini si vizuri kuwa na Muungano unaohujumu upande mmoja kiuchumi.

Mwakilishi wa Jimbo la Mkanyageni, Haji Faki Shaali (CUF), alisema ni jambo la kushangaza Serikali ya Zanzibar na ya Muungano wameamua kutafuta mshauri katika suala la mafuta ya Zanzibar, wakati hatua kama hiyo haikuzingatiwa katika utafutaji wa gesi huko Tanzania Bara.

Kwa upande wake, Zakia Omar (Viti Maalum-CUF), alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapaswa kulipwa mgawo wa madini ya tanzanite, almasi na dhahabu kwa asilimia 50 tangu biashara hiyo ilipoanza kufanyika Tanzania Bara.

Alieleza kwamba kuingiza mafuta katika orodha ya mambo ya Muungano na kuacha madini kama vile tanzanite na almasi hakuleti sura nzuri katika matumizi ya maliasili baina ya pande mbili za Muungano.

Akiwasilisha bajeti yake, Waziri Mansour alisema suala la uchimbaji mafuta na gesi asilia ni suala la Muungano na linapaswa kutawaliwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kwamba suala la mafuta Zanzibar hadi sasa linajadiliwa katika vikao vya pamoja vinavyofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri Kiongozi na vikao hivyo vimeagiza Wizara ya Nishati na Madini Bara na Zanzibar kutafuta mshauri mwelekezi atakayezishauri serikali zote mbili juu ya namna sahihi ya kugawana mapato ya mafuta na gesi.
“Kwa misingi hiyo, inapaswa kuamuliwa na pande zote mbili za Muungano kwa kuzingatia kuwa suala la utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi linatawaliwa na Katiba ya Muungano,” alisema.
Zanzibar wadai mgawo wa madini
 
Kazi kweli kweli, ila nimeshangazwa na kitu kimoja hapo serikali ipi ya Mungano inayozungumziwa hapo ? kama kuna serikali ya zanzibar mbona ya Tanganyika hatuioni, unajua haya masuala ya Mungano yangekuwa yanaenda vizuri kama serikali ya Tanganyika ingekuwepo, sasa tutaongea habari ya masuala ya mgawanyo wa mapato na nchi huru "Zanzibar"
 
Sisi tuenda Zenji hawatutaki, sasa vipi tuwape mali zetu hawa wagunyaa
 
Mimi sielewi wa Zanzibar kwa sasa wanapata 4% ya kipato cha nchi na pesa ya madini yako kwenye kipato cha nchi sasa mgao wa madini wana maana gani???
 
Ama kweli humu tumo watu wa aina mbali mbali kuna wale wanaopeda kuleta habari za kuokoteza na wako wale wanaopenda kuchangia mambo ya kuokoteza huku hawajuwi chochote kwa wanaochangia.


Kamundu, Kinehe,jinuswe na wewe Error hivyo hamjuwi kuwa Zanzibar hakuna mawaziri vivuli? Hivyo hamjuwi kuwa kikao cha baraza la wawakilishi kinaanza tarehe 15/06/2011 na hamjuwi kuwa Mansouri ni waziri wa Kilimo si waziri wa Madini na huyo hamadi Masouid ni waziri kamili si waziri kivuli?
 
Back
Top Bottom