Zanzibar na Tanganyika katika mezani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar na Tanganyika katika mezani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 12, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1]Zanzibar na Tanganyika katika mezani[/h]Posted on March 11, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Professa Abdul-Shareef akionesha mezani inayoninginia vidoo viwili kimoja cha Zanzibar na nyengine kikiwa na maandishi mawili ya Tanzania/ Tanganyika ambapo Prof alifundisha jinsi gani baada ya uhuru nchi hizi mbili zilikuwa sawa kimadaraka na maslahi, lakini ghalfa na pole pole Zanzibar ikaanza kunyanganywa baadhi ya mambo hatimae upande wa Zanzibar ukawa umezidiwa kwa uzito katika mezani, Professa alikuwa huko Wete Pemba wakati akitoa elimu ya uraia kwa niaba ya Baraza la Katiba Zanzibar.

  IMEELEZWA kwamba suala la mgawanyo wa madaraka baina ya pande mbili za Muungano katika katiba ya Tanzania iliyopo sasa hayana nguvu za kikatiba. Suala hilo limejitokeza jana katika mdahalo wa ujengaji wa uelewa wa utoaji wa maoni juu ya Katiba mpya ya Tanzania inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu za uundwaji wa kamati ya kuratibu na kukusanya maoni ya katiba mpya.
  Akitoa mada ya “Dondoo muhimu za msingi wa Katiba na maeneo ya migongano baina ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na ya Tanzania ya mwaka 1977” katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha zanzibar (SUZA) Mjumbe wa Baraza la Katiba Zanzibar, Ally saleh Abdallah alisema suala la mgawanyo wa madaraka baina ya pande mbili za Muungano, hasa nafasi ya Urais inapatikana kwa maamuzi ambayo hayana nguvu ya kikatiba na hivyo kuzorotesha haki.
  Alisema kutokana na hali hiyo hana imani kwamba kama Tanzania itapata tena rais kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa hakuna nguvu za kisheria wala kikatiba juu ya ya suala hilo.
  “Hakuna katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kipengele kinachoweka masharti juu ya mgawanyo wa madaraka, upungufu huo ni chanzo cha malalamiko juu ya namna madaraka yanavyotolewa kwa mtu, awe ni wa upande wa Tanganyika au Zanzibar, na hivyo basi siamini kwama ipo siku rais wa Tanzania atatokea Zanzibar nafasi imeshapoteza na sio rahisi kurudishwa tena” alisema Ally Saleh.
  Ally Saleh ambaye ni Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la Uongereza (BBC) alisema tatizo la mgawanyo wa madaraka ni kubwa zaidi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma ambapo baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar mwaka 1964, ambapo Baraza na Mawazi lilikuwa na mawaziri watano kutoka Zanzibar.
  “Hebu tutazameni hapa, hivi sasa orodha ya mambo ya muungano imeongezeka na kufikia 22, kutoka 11 mwaka 1964, baraza hilo lina watu wane tu, na kila siku tume zinaundwa kuondosha kero za muungano lakini matokeo yake kero zipo pale pale ” alisema katika kongamno hilo.
  Ally alisema baada ya rais Ali Hassan Mwinyi kupata urais huo hana imani tena kama ataweza kupata mtu mwengine kutoka Zanzibar kwani rais wa Zanzibar ndiye laiyekuwa makamo wa kwanza wa rais lakini kwa sasa nafasi hiyo haipo tena baada ya kufutwa kw awoga wa baadhi ya wabunge kwa kuhofia uchaguzi wa mwaka 1995 wapinzani wangeweza kushika madaraka huku Zanzibar hivyo makamu wa rais wa Tanzania angekuwa ni mpinzani.
  “Wakati ule wabunge waliiondosha nafasi ya rais wa zanzibar kuwa makamo wa kwanza wa rais, na walikuwa wanahofia pengine Maalim Seif angeshinda uchaguzi kuwa rais wa Zanzibar, sasa wakaona vipi makamo wa kwanza awe mpinzani? ….? wakaogopa…” alisema Ally.
  Mdahalo huo ulioandaliwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkao wa Mjini Magharibi (UWECSONET) umeanza kutoa elimu juu ya ushiriki wa wananchi katika zoezi la uelewa wa katiba mpya ambapo asasi mbali mbali zimeanza kutoa elimu.
  Ally alizishauri asasi za kiraia Zanzibar kuongeza nguvu katika umoja ili kuweza kutoa elimu za uraia kwa wananchi mbali mbali ili wakati mchakato huo utakapoanza wananchi wawe wameshapata ufahamu juu ya katiba mpya.
  Alisema mbali na kutoa elimu wadau wa taasisi za kiraia kwa kutumia jukwaa hilo pia wanaweza kuunda mfumo wa kufanyakazi za kufuatilia mwenendo wa hatua zote za utekelezaji wa mchakato wa kupata Katiba mpya.
  “Asasi zijiandae kuwa na mfumo wa kufuatilia maoni yote na kutunza kumbukumbu, hatuwezi kuiachia Tume kazi yote,” Ally Saleh. Na kuongeza kwamba ufuatiliaji na kumbukumbu zitakazotunzwa na wadau wa jukwaa litakaloundwa chini ya umoja ya ushirikiano wa taasisi zote za kiraia hapa Zanzibar.
  Ally alisema ushiriki wa wananchi katika zoezi hilo ndio utakaoamua upatikanaji wa Katiba inayozingatia nafasi ya Zanzibar katika mambo ya Muungano, yakiwemo ya mgawanyo wa madaraka na muungano wanaoutaka.
  Nao washiriki wa kongamano hilo walisema kabla ya kuanza kwa tume kukusanya maoni wanataka waulizwe kama wanautaka muungano au hawautaki kwani ni haki yao ya kikatiba na hivyo Zanzibar inayo sheria ya kuitishwa kura ya maoni.
   
 2. U

  Userne JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnakumbuka shukaa! Mbona kumekucha balahauu.
  TLissu aliliona hilo mapema! Wabunge wa zenj, Wakamzomea! sasa mti umeingia kwenye shoka acha msitu wishe ati!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo wanadhani kila anayezungumzia 'matatizo' yao anawahujumu
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hakika wanayarudia aliyosema Tundu Lissu.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wanakula matamshi yao!
   
 6. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wazanzibari nao kwa kiswahili cha Comoro!
  kidoo = kindoo
  mwengine = mwingine
  mezani = mizani

  Muungano utawafundisha kiswahili fasaha, msiukatae!
   
 7. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafiliki prof kachemka maana ni obvious
  Assuming all tanzania,Tanganyika and Zanzibar are positive
  IF Tanzania=tanganyika +Zanzibar
  then
  Zanzibar must be subset of Tanzania
  Therefore
  Tanzania must be heavier than Zanzibar
  End If

  Non sense comparison
   
 8. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  Hii program lazima i run wapende wasipende wasipo elewa na hapa achana nao
   
Loading...