Zanzibar na matamko ya viongozi wa Serikali ya Tanzania

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
10,518
19,883
Ni week ya tatu sasa tangu Waziri wa Afya atoe tamko la kupandisha kiwango cha kupima corona hapa inchini Tanzania.

Wakati huku bara tukiendelea kupima kwa 100$ kwa kila msafiri bila kujali urai au rangi ya mtu, Zanzibar wao bado kupima ni Tshs 30000 tu kwa raia wa Tanzania.

Je, hili lipoje wakuu au haya matamko yanayotolewa na wateule wa rais ni kwa ajili ya wanainchi wa bara peke yao?

Au wanainchi wa Zanzibar ndiyo wanyonge pekee katika inchi yetu ya Tanzania wanaostahili kuhurumiwa na kusaidiwa? Au Zanzibar sio sehemu ya Tanzania?

Tunaiomba serikali hii sikivu, serikali ya wanyonge iangalie upya suala la ongezeko la gharama za vipimo vya covid bara. Na kuzipunguza gharama.

Ili kuleta usawa katika jambo hili la kupima Covid 19.
 
Zanzibar wana maisha yao tofauti kabisa na bara hata suala la Corona kwamba haipo walikubali kishingo upande kwa maslahi ya nchi ila jamaa wana msimamo sana wale.
 
Back
Top Bottom