bilengeh
Senior Member
- Mar 31, 2017
- 135
- 86
HISTORIA ya Zanzibar kwa kiasi kikubwa imehusishwa na biashara ya utumwa. Bahati mbaya ni kwamba wengi wa waandishi wa historia hiyo wameunasibisha utumwa na Uislamu. Katika makala hii mwandishi wetu SAID MZEE anatuelezea juu ya historia ya utumwa katika Zanzibar.DUNIA imepata kupitiwa na mifumo mingi ya maisha katika mwanadamu kutaka kuishi maisha bora kwa lengo la kuzalisha mali. Moja kati ya njia hizo ni utumwa.
Utumwa ulikuwako katika nchi zote duniani kuanzia za Ulaya, Asia hadi Afrika. Kwa mujibu wa Tarekh wazungu ndio waliokuwa watu wa mwanzo kuwafanya wazungu wenzao kuwa watumwa baadaye wakafuatiwa na Wachina.
Chanzo cha utumwa katika jamii zote kilikuwa aidha kushindwa katika vita, kushindwa kulipa deni unalodaiwa, adhabu kufuatia uhalifu uliotenda n.k.
Wazungu ndio waliokuwa wahalifu wakubwa kabisa katika kuendeleza biashara hii ya utumwa kwa niaba ya msalaba. Kati ya makabila yote ya Kizungu waliotia fora walikuwa ni Waingereza na Wamarekani ambao ni Wakristo wa Kiprotestant na Katoliki ambao leo wanajigamba na kujidai ati ni wao walioondosha utumwa.
Kama tulivyotangulia kusema awali kwamba utumwa ulikuwa ni mfumo wa maisha pale Waingereza walipopendekeza kuondoshwa kwa utumwa ulikuwa ni kwa sababu utumwa haukutia faida tena za kiuchumi na ilibidi ubadilishwe na uzalishaji mali mpya wa kibwanyenye nasio kwa sababu kwamba Wazungu walikuwa na huruma sana na Waafrika.
Kwa njia ya kudau kuondosha utumwa Manuwari na Merikebu za Kiingereza zilidiriki kuchoma na kuteketeza kwa moto madai na majahazi ya wafanya biashara yakiwa na watumwa au la, na matendo yao hayo kubainika na watawala wao. Pengine ajenda ambayo imefichwa hadi leo na Waingereza hao juu ya ukatili wao huo ni kuwa lengo kubwa lilikuwa ni kukata mizizi ya biashara baina ya Afrika Mashariki na nchi za Mashariki ya Bahari ya Hindi.
Kwa kutumia njia hii Waingereza waliweza kuhodhi uchumi wa Afrika ya Mashariki na kuua kabisa biashara baina ya Afrika ya Mashariki na Mashariki ya Bahari ya Hindi biashara ambayo ilishadumu kwa karne nyingi. Wakati Muingereza alidai kupiga vita usafirishaji wa watumwa kutoka Afrika ya Mashariki, upande mwingine aliruhusu uuzaji na uzalishaji mali wa watumwa katika bara la Afrika ya Mashariki na kwa kutenda hivyo aliweza kujinufaisha kisiasa na kiuchumi kupitia biashara hiyo ya watumwa.
Kwa vile Zanzibar ilikuwa ndio kitovu cha biashara katika Afrika ya Mashariki na kati Muingereza aliweza kuuwa uchumi wa Zanzibar na hivyo kumuwiya rahisi kutawala sehemu yote ya Afrika ya Mashariki. Zanzibar iligeuzwa bandari na soko mojawapo maalumu la watumwa, vituo vingine vikiwa sehemu za jirani na visiwa hivi kama vile Bagamoyo na Kilwa.
Pamoja na kwamba Zanzibar ilikuwa ni bandari na soko muhimu la watumwa, hakuna Mzanzibari ambaye alifanywa mtumwa bali watumwa hawa walitoka mabara ama kutokana na kusakwa na wachuuzi wa watumwa wa Kiarabu na wa kienyeji au kutokana na kuwa mateka wa vita baina ya machifu, mapigano baina ya makabila mbalimbali kama vile Wamakonde, Wamakua, Wayao n.k. au ni kutokana na kushindwa nguvu na kutekwa na wenzao.
Kufikia mwaka 1873 Zanzibar ilipiga marufuku biashara ya utumwa lakini cha kushangaza ni kwamba Wareno na Wafaransa waliendelea na biashara hiyo na Muingereza hakunyanyua mkono wkae kuwakemea.
Ingawa sheria ya kukomesha utumwa ilipitishwa rasmi 1873 cha kustaajabisha ni kwamba hadi leo wanasiasa wetu wamekuwa wakiwadanganya wananchi na wageni wanaofika Zanzibar kwamba utumwa uliondoshwa na mapinduzi ya Januari 1964.
Kama neno lenyewe linavyoonyesha, utumwa ni njia mojawapo ya uzalishaji mali ambayo ni kashfa kubwa mtu kunasibishwa nayo na kwa mujibu wa sifa za ubinadamu anayekashifika zaidi ni yule muuzaji wa watumwa hao kuliko watumwa wenyewe, kwani yeye huwa ndio kaonyesha upungufu mkubwa wa kibinadamu kwa kukubali kumuuza binadamu mwenziwe.
Pengine kwa kutambua hili ndio maana Sultan hakutaka kuwaona raia wake wa Zanzibar wakifanywa watumwa. Nchi za Ulaya ambazo leo zinajipa au kupewa sifa za utu bora ndio zinazotumia uzalishaji mali kupitia njia za watumwa na kuyawezesha matabaka ya juu yaliyokuwa yakitawala kujinufaisha kwa kiasi kikubwa. Mfano mzuri wa Waafrika wa Kimarekani (Black American) waliojenga uchumi wa Marekani kwa jasho na damu yao wakati tabaka lao likisehelea katika umasikini.
Wakoloni wote wakiongozwa na Waingereza wamekuwa wakifanya njama za siri na dhahiri za kujifanya wao ni wazuri na kuja kwao Afrika kulikuwa na madhumuni ya kuleta kheri na mafanikio kwa Waafrika pasi na kuwa na lengo jingine lolote.
Njia moja kubwa waliyoitumia ni Makanisa na Mapadri. Wazungu hao walidai kwamba wamekuja kupiga vita ushenzi na kuleta staarabu.
Wakoloni wa Kiingereza mara tu baada ya kuwanyang’anya hatamu wazalia wa Zanzibar na kuuhifadhi utawala wa Kibuu Said walimpa jina ambalo lililokuwa na dhamira ya kuwapa faida zaidi wao.
Waingereza kwa sababu zao waliuita utawala huo kuwa ni wa Waarabu. Lengo la kuuita utawala huo kuwa ni wa Kiarabu lilikuwa ni kuufanya Uislamu uonekane ni mbaya na umekandamiza Waafrika na Wazungu na Ukristo ndio mzuri kwa vile unapiga vita biashara ya watumwa.
Bahati mbaya sana watu wengi hadi hii leo wamenasa katika mtego huo wa Waingereza na wengine pamoja na kusoma kwao kote basi wameshindwa kulielewa lengo na dhamira hii ya Muingereza. Ukweli ni kwamba utumwa ulikuwepo Afrika ya Mashariki hata kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (as) kwa hiyo hata kabla ya kuja Mtume Muhammad (saw) utumwa ulikuwa umeshaota mizizi ulimwenguni, lakini Waingereza na wakoloni wenzao wa Kizungu kwa kutumia Kanisa wakaufanya utumwa umeletwa na Waarabu kwa lengo lile lile la kuonyesha kwamba Uislamu ndio ulioleta utumwa.
Wakati ambao utumwa ulipigwa marufuku Zanzibar, Wareno na Wafaransa walishughulika na biashara ya utumwa katika nchi za Mashariki ya Afrika na kazi hiyo walifanya bila ya kuingiliwa kati na Manowari za Kiingereza zilizowekwa maalum kulinda usafirishaji wa watumwa.
Ukweli huu hausemwi na Muingereza wala vibaraka wake wa Kikristo ingawaje wanafahamu kwamba kulikuwa na Waingereza hapa hapa Zanzibar ambao walikuwa wakifaidika kutokana na jasho la watumwa hao na ndio maana utaona kwamba kilichopigwa marukufu na Wazungu ni usafirishaji wa watumwa na si kumiliki watumwa.
Jambo jingine ambalo Waingereza na vibaraka wao wamesahau kulisema ni kwamba huko kwao pia kulikuwa na utumwa ingawaje hakukuwa na Uislamu. Katika hili Waingereza wanajifanya hawatambui juu ya maafa ya Waafrika wa Afrika Magharibi (Nigeria, Ghana, Liberia) waliopelekwa Marekani ya Kaskazini, Kusini na Caribbean ambako nako hakukuwa na Uislamu. Wazungu walipokwenda Marekani waliwenda kwa niaba ya jina takatifu la Ukristo na kwa niaba ya jina la Msalaba, wakawateketeza wenyeji wa huko na kuwafanya watumwa, lakini hilo leo hawalisemi badala yake wanasingizia Uislamu ndio ulioleta biashara ya utumwa.
Njama za kuufanya Uislamu uonekane mbaya Afrika ilikuwa ni kuleta chuki za kugonganisha vichwa baina ya Wazanzibari kwa Wazanzibari, Watanganyika kwa Watanganyika ili kuweza kuwatawala kwa urahisi na kuweza kusambaza dini yao ya Kikristo.
Hilo ndilo lilikuwa na linaendelea kuwa lengo maalumu la kampeni hiyo, ingawa wengi wa Wazungu hao walikuwa na wanaendelea kuwa hata huyo Mungu mwenyewe hawamuamini bali hutumia Ukristo kuwatawala kimawazo na kiuchumi Waafriak tu. Waingereza hawa na vibaraka wao wamesahau kwamba Christopher Columus aliwateketeza Wahindi Wekundu kwa niaba ya Ukristo na kazi hiyo ovu ikaendelezwa na Waingereza mkoloni hadi leo hajatuambia ni kwa nini aliwateketeza wenyeji wa Australia na New Zealand kwa maradhi mbalimbali. Je, wakati wakifanya hayo nao walikuwa ni Waislamu?
Ni bahati mbaya sana kwamba Wazanzibari badala ya kuamka na kuzitamka mbinu za mkoloni za kutugonganisha vichwa Waislamu kwa Waislamu badala ya kukaa kitako na kujaribu kutatua tofauti zetu za kisiasa na nyingine za kijamii, tumezama katika kuendeleza mifarakano.
Jambo jingine ambalo Muingereza na Kanisa wamesahau kuwaambia Waafrika ni kwamba katika biashara ya utumwa Zanzibar Waislamu hawakufanywa watumwa na wale ambao walisimu walitolewa utumwani. Lakusikitisha ni kuona hata wale waandishi na wataalamu wanaodaiwa kuwa wameendelea wametekwa nyara na tafsiri potofu ya utumwa kama ilivyotolewa na Kanisa.
Uislamu hadi leo unapigwa vita sehemu zote ulimwenguni ingawaje leo hazitumiki sababu za utumwa lakini bado kwa kiasi kikubwa zinanasibishwa na matukio ya utumwa. Ni budi Wazanzibari tukumbuke kwamba kwa kutumia Uislamu badala ya tafsiri ya kitabaka aliyoiandaa yeye mwenyewe Muingereza alifanikiwa kuleta chuki na uhasama baina ya wakazi wa visiwa hivi, wakati mwenyewe akishirikiana na kuuhifadhi utawala huo aliouita wa Kiarabu.
Kwa njia hiyo Muingereza alifaulu kutufanya tukabane roho wenyewe kwa wenyewe na kusahau kumpiga vita adui yetu mkubwa ambaye ni yeye na Kanisa lake, kama alivyofanikiwa leo kutugonganisha vichwa kwa masuala ya kisiasa na kuwaacha maadui wetu wakubwa ukizidi kuiangamiza jamii yetu kwa kasi ya kutisha.