Zanzibar kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili kuwa Tanzania ambayo yatakuwepo Zanzibar

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye, Bungeni mjini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali ambazo Tanzania inachukua katika kukuza lugha ya kiswahili katika ngazi ya Kimataifa
d93e766c2f5f8dd27e6bb69747c04362.jpg


Nape amesema kuwa maamuzi hayo ya kuifanya Tanzania kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili yametokana na Tanzania kuzalisha walimu wengi wa kiswahili ambao wanatumika katika ngazi mbalimbali za elimu ndani na nje ya nchi

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema kuwa Wizara hiyo kwa sasa inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa mawakala wa kulinda lugha ya kiswahili

Aidha, amesema kuwa Waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuhakikisha lugha hiyo inaendelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya lugha hiyo katika majukumu yao ya kila siku

"Kutumia zana kama vile kamusi na vitabu vya miongozo ya uandishi pamoja na kuhudhuria makongamano ya kitaifa na kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inasaidia kuongeza ujuzi na weledi wa lugha ya kiswahili ", alisema Wambura

Hata hivyo Wizara hiyo iko katika maandalizi ya Sera ya Lugha ambayo itabainisha majukumu ya Vyombo vya habari katika matumizi na uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili.
 
Back
Top Bottom