Zanzibar: Kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere, watumishi 59,967 kupandishiwa mishahara na madaraja mwezi ujao

tambueni kupanda madaraja ni jambo linalowahusu baadhi ya watumishi kwa wakati fulani na halitawagusa watumishi wote.tunachohitaji ni ile nyongeza iwagusao wote pamoja na hao wanaopanda madaraja ! watumishi wapo zaidi ya laki tano yeye anazungumzia watumishi elfu hamsini na tisa.!!!
 
ile karatasi ya hotuba i
Keshampiga dongo Seif.

Ahahaha.

Eti wale waliokuwa wanataka kuapishwa wameshaapishwa?

Wanatuwezaaa...!

Ahahaha
ILE KARATASI YA HOTUBA IKIPEPERUSHWA NA UPEPO TU! TUTAZIBA MASIKIO.ILA AKIENDELEA NA HIZI HOTUBA ZA KUANDIKIWA MAMBO YATAKUWA SAFI.ANGEKUWA HATUMII KARATASI JASHO LINGEKUWA LIMEMTOKA BALAA
 
Mlivyo watu wa ajabu...AMETAAMKA kuwatimizia KE3LELE ZENU...
MLIVYO NA LAANA mnaanza kuropoka pumba...SASA MSEME MNATAKA NINI???
WOTE MLIOCOMMENT HAPO JUU nyie sio watanzania....wivu unawasumbua mno
MNATAKA KUSIKIA MABAYA TU muda wote
 
So Dkt. Abbas jana alikua akitoa Utangulizi ili huyu aje atoe habari kamili,
Means hili tamko la leo lingekuja kabla ya Dkt Abbas jana kungekua na ukakasi kidogo
 
Mlivyo watu wa ajabu...AMETAAMKA kuwatimizia KE3LELE ZENU...
MLIVYO NA LAANA mnaanza kuropoka pumba...SASA MSEME MNATAKA NINI???
WOTE MLIOCOMMENT HAPO JUU nyie sio watanzania....wivu unawasumbua mno
MNATAKA KUSIKIA MABAYA TU muda wote



01/05/2017 alisema hivyo hivyo
 
Huyu jamaa wimbi kweli! Yaani anaona kuhamia Dodoma ndiyo jambo la maana katika yote ambayo Nyerere alipanga? Yaani kuhamia Dodoma ndiyo anaona anamuenzi 'Baba wa Taifa'? Rais tunaye.

Naamini, Nyerere angekuwa hai leo, angekuwa wa kwanza kupinga wazo la kuhamia Dodoma. Kwa taifa ambalo bado watoto wa shule wanasomea chini ya miembe; ambalo hata panadol inaweza kukosekana kwenye zahanati za serikali; ambalo bado watu wanakunywa maji yanayonywewa na wanyama n.k., kutumia mabilioni ya shilingi ati kwa kuhamia Dodoma, ni ujinga wa kiwango kisicho na upinzani.

Hilo la kuhamia Dodoma siyo kipaumbele cha wananchi anaowaita wanyonge kila siku. Kama anamuenzi kweli Nyerere asimuenzi selectively, amuenzi kwa mambo yote ambayo Nyerere aliyapigania. Kama Azimio la Arusha, ambalo yeye kama mwanaCCM alishiriki kulifutilia mbali. Lakini ati kuhamia Dodoma ndiyo anaona ni jambo la msingi. Hakika nakubaliana na watu wanaosema bila Katiba mpya, Tanzania isahau kupata maendeleo ya watu wake. Yaani mkurupuko wa mtu mmoja tu, unaligharimu taifa!
 
Habari wakuu,

Leo Rais Magufuli ni mgeni Rasmi kwenye kilele cha mbio za uhuru. Pia leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kinachoendelea sasa ni dua na sala kutoka kwenye Sheikh na Askofu, kuwa nami...



======

Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wote walishawasili na kuimbwa wimbo wa Taifa.

Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki shughuli hii, mwaka jana nilimuomba Rais Shein aniwakilishe Simiyu.



Watanzania tunafaa kujiuliza kwanini tunamkumbuka Mwalimu Nyerere, nijuavyo siku hii iliamuliwa kuwa siku ya kitaifa ili kujikumbusha mchango mkubwa na usiosahaulika wa mwalimu Nyerere.

Nimuona ni jambo jema kumzungumzia kidogo Mwalimu Nyerere, historia ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndefu. Kwanza alikuwa mzalendo, TANU iliongoza harakati za kutafuta Uhuru nae alikuwa kiongozi.

Umbali wa kutoka Pugu mpaka ofisi za TAA, kwenda na kurudi ilikuwa kilomita 46 na alitumia fedha zake kusafiri na wakati mwingine kulazimika kutembea, tujiulize leo viongozi wangapi wanaweza kujitolea kiasi hiko.

Alipoambiwa kuchagua kati ya kazi na TANU, aliamua kuchagua TANU. Nna uhakika maisha yalikuwa magumu, wasomi wa kiwango chake wakati huo walikuwa wakihitajika sana, watanzania wangapi wangeweza kujitoa hivyo? Viongozi wangapi kwa kufanya kazi kwenye makampuni ya kigeni, wanatusaliti?

Yeye na familia yake waliishi maisha ya kawaida sana, hawakujilimbikizia mali. Kuna mifano mingi ya viongozi wa zama zake hata sasa.....

Mwalimu Nyerere hakukubaliana na wafanyakazi waliotaka kuongezewa mishahara, alifanya mfano kwa kujipunguzia mshahara wake. Je sisi tuko tayari kuacha mishahara hewa? Je! Mishahara tunayopata tuumeifanyia kazi? Je! Tuko tayari nasi kujipunguzia au kuacha kuishinikiza serikali kuongeza mishahara na marupurupu yetu ili kuwezesha kuboresha huduma za jamii kwa manufaa ya watanzania na hasa watanzania wote?

Ninasema hivyo, simaanishi kuwa mishahara isiongezwe, La Hasha! Ninachotaka kusema ni kwamba, kabla ya kudai nyongeza ya mishahara, ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa serikali. Lakini pia tutambua kwamba kuna watanzania wenzetu wengi wanaohitaji kuboreshewa huduma

Tuna mifano inayoishi kwa hapa Zanzibar, baada ya Shein kushika madaraka, mishahara ya kima cha chini imepandishwa 150,000 mpaka 300,000 lakini na sisi kule Bara, baada ya kuchukua hatua za kupunguza watumishi hewa pamoja na watumishi ambao hawakutakiwa serikalini na kuanza kujisafisha sisi wenyewe.

Tumeshafanya uchambuzi kwa watumishi 59,967 watarekebishiwa mishahara yao na promotion zao karibu bilioni 159 zitaanza kutolewa kuanzia mwezi unaokuja lakini tusingefanya uchambuzi, tungelipa bilioni 89 kwa watumishi hewa.

Neno mwezi ujao tumelizoea. Taarifa ya Abasi ilijichanganya tu. Leo anataka kupooza machungu. Mkuchika tumemsikia hadi suala la kufoji umri liishe. Leo anasema mwezi ujao watarekebisha mishahara. Ngonjera hatutaki
 
Kusema ukweli kama Raisi wetu anavyotuasa kusema ukweli ili kuwa mpenzi wa mungu Sijawahi kuona jipya katika hotuba za Mheshimiwa zaidi ya "Tumeondoa watumishi hewa ambao walikuwa wanalipwa mabilioni ya hela, tunajenga reli ya kisasa ya standard gauge, tutajenga flying overs na zimeshaanza kujengwa...............Jamaa nahisi bado anahisi ni waziri wa ujenzi au mwandaji wake wa hotuba ni yule aliekuwa naye kule wizara ya ujenzi. Tunahitaji kusikia mikakati ya kukuza uchumi wa kundi kubwa ambalo ni maskini Tanzania, tunahitaji kusikia mipango ya muda mfupi na mrefu kuhusu kuinasua sekta ya afya ambayo iko ICU, tunahitaji kusikia mikakati iliyoko kukuza na kutoa elimu bora kwa watoto wetu, tunahitaji kusikia mikakati ya kustawisha demokrasia yetu, tunataka kusikia mipango ya kuwapatia watu maji safi na salama nchi nzima na mwisho kabisa tunahitaji kusikia mipango kabambe ya kudumisha umoja wetu na mshikamano kwa kudumisha na kuimarisha ulinzi ambao unaonekana kuruhusu watu wasiojulikana kutuchafua kama taifa.
Nani nyie mnayotaka hayo?
 
Back
Top Bottom