Zanzibar: Kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere, watumishi 59,967 kupandishiwa mishahara na madaraja mwezi ujao

Habari wakuu,

Leo Rais Magufuli ni mgeni Rasmi kwenye kilele cha mbio za uhuru. Pia leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kinachoendelea sasa ni dua na sala kutoka kwenye Sheikh na Askofu, kuwa nami...



======

Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wote walishawasili na kuimbwa wimbo wa Taifa.

Hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki shughuli hii, mwaka jana nilimuomba Rais Shein aniwakilishe Simiyu.



MAGUFULI: Watanzania tunafaa kujiuliza kwanini tunamkumbuka Mwalimu Nyerere, nijuavyo siku hii iliamuliwa kuwa siku ya kitaifa ili kujikumbusha mchango mkubwa na usiosahaulika wa mwalimu Nyerere.

Nimuona ni jambo jema kumzungumzia kidogo Mwalimu Nyerere, historia ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndefu. Kwanza alikuwa mzalendo, TANU iliongoza harakati za kutafuta Uhuru nae alikuwa kiongozi.

Umbali wa kutoka Pugu mpaka ofisi za TAA, kwenda na kurudi ilikuwa kilomita 46 na alitumia fedha zake kusafiri na wakati mwingine kulazimika kutembea, tujiulize leo viongozi wangapi wanaweza kujitolea kiasi hiko.

Alipoambiwa kuchagua kati ya kazi na TANU, aliamua kuchagua TANU. Nna uhakika maisha yalikuwa magumu, wasomi wa kiwango chake wakati huo walikuwa wakihitajika sana, watanzania wangapi wangeweza kujitoa hivyo? Viongozi wangapi kwa kufanya kazi kwenye makampuni ya kigeni, wanatusaliti?

Yeye na familia yake waliishi maisha ya kawaida sana, hawakujilimbikizia mali. Kuna mifano mingi ya viongozi wa zama zake hata sasa.....

Mwalimu Nyerere hakukubaliana na wafanyakazi waliotaka kuongezewa mishahara, alifanya mfano kwa kujipunguzia mshahara wake. Je sisi tuko tayari kuacha mishahara hewa? Je! Mishahara tunayopata tuumeifanyia kazi? Je! Tuko tayari nasi kujipunguzia au kuacha kuishinikiza serikali kuongeza mishahara na marupurupu yetu ili kuwezesha kuboresha huduma za jamii kwa manufaa ya watanzania na hasa watanzania wote?

Ninasema hivyo, simaanishi kuwa mishahara isiongezwe, La Hasha! Ninachotaka kusema ni kwamba, kabla ya kudai nyongeza ya mishahara, ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa serikali. Lakini pia tutambua kwamba kuna watanzania wenzetu wengi wanaohitaji kuboreshewa huduma

Tuna mifano inayoishi kwa hapa Zanzibar, baada ya Shein kushika madaraka, mishahara ya kima cha chini imepandishwa 150,000 mpaka 300,000 lakini na sisi kule Bara, baada ya kuchukua hatua za kupunguza watumishi hewa pamoja na watumishi ambao hawakutakiwa serikalini na kuanza kujisafisha sisi wenyewe.

Tumeshafanya uchambuzi kwa watumishi 59,967 watarekebishiwa mishahara yao na promotion zao karibu bilioni 159 zitaanza kutolewa kuanzia mwezi unaokuja lakini tusingefanya uchambuzi, tungelipa bilioni 89 kwa watumishi hewa.

Baada ya miaka michache ya kupata Uhuru, Mwalimu Nyerere alitambua kuwa huwezi kupata maendeleo kama njia kuu za uzalishaji zimeshikiliwa na watu binafsi peke yake, ni lazima serikali ishiriki kikamilifu na huo ndio ukweli wenyewe.

Nchi zote zilizofanikiwa duniani, serikali zao zilishiriki moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi hivyo aliona upo umuhimu wa kujenga misingi itayowezesha seriakali kushiriki kikamilifu na ndipo azimio la Arusha lilipozaliwa mwaka 1967.

Mbali na azimio la Arusa kuweka miiko kuwabana viongozi kujilimbikizia mali, kulisaidia kuzuia mashirika na makampuni ambayo yalitumiwa na mabepari kutorosha rasilimali zetu kwenda nje ya nchi. Serikali ikajenga viwanda na mashirika, tulikuwa na viwanda vingi na kupunguza utegemezi kutoka nje, shirika la ndege pia lilikuwa na ndege 9. Lilianzishwa shirika la nyumba lililokuwa na nyumba zaidi ya 6,000

Pia namnukuu mwalimu, alisema 'Ni vyema madini yetu tukayaacha mpaka watanzania tutakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba' mwisho wa kunukuu.

Sambamba na hayo, serikali iliweka mkazo kwenye elimu ambapo serikali ilitoa elimu bure bila ubaguzi, kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuu. Mwalimu Nyerere aliamini, ukitaka kumkomboa mtu mnyonge, ni lazima uumpe elimu.

Vilevile alihimiza watu kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia kauli mbiu za uhuru na kazi, siasa ni kilimo na kadhalika. Pamoja na misingi hii iliyowekwa na mwalimu Nyerere, miaka michache baada ya yeye kung'atuka, tulilitupa azimio hilo, sasa sijui ilitokea kwa makusudi au kwa bahati mbaya, mimi sijui ila ni kweli kwamba tulilitupa na baada ya kulitupa tulianza kuuza mashirika na viwanda vyetu.

Hata vile vilivyojiendesha kwa faida kwa matarajio kuwa tunaowauzia, wangeviendesha kwa ufanisi zaidi haikuwa hivyo, mashirika mengi na viwanda tulivyobinafsisha, sasa vimekufa, vipo wapi viwanda vya nguo, ngozi, nyama matairi na kadhalka, jumla ya viwanda 197 vilikufa, kwa nini tuliamua kuuza viwanda vyetu? Kwa nini shirika letu lishindwe kujenga nyumba kwa wananchi wa kipato cha chini?

Jana nilikuwa naongea na Rais Museveni, yeye amesema bila mwalimu, asingekuwa Rais wa Uganda. Lakini tukumbuke Mwalimu alikuwa miongoni wa waanzilishi wa OAU na SADC.

Huyo sio mtu wa kumwamini wakuu! Hata kwenye may mosi alisema hivyo ikawaje?
 
"Sijapandisha mishahara ya watumishi, na sitapandisha sababu nina jukumu la kutoa huduma kwa wananchi."

Raisi John Pombe Magufuli.
Dar es salaam
Mkutano wa 33 ALAT
02.10.2017

Halafu leo 14.10.2017

Mtu yule yule.

"Tumeshafanya uchambuzi kwa watumishi 59,967 watarekebishiwa mishahara yao na promotion zao karibu bilioni 159 zitaanza kutolewa kuanzia mwezi unaokuja lakini tusingefanya uchambuzi, tungelipa bilioni 89 kwa watumishi hewa."

Magufuli kuna mtu anamuelewa anaenda au anarudi?
 
Wazanzibar na hotuba ya magu wapi na wapi?
Kwanza wazanzibari hawataki kusikia kitu kinaitwa Tanzania visiwani. Kule ni Zanzibar na wakazi wake wanaitwa wazanzibari sio watanzania. Sisi tunajiita watanzania badala ya waTanganyika. Ukisema ni mtanzania kwa mnyumbuliko ni kuwa Wew ni mtanganyika - mzanzibari
 
Hii inji..!

Kwahiyo Mkuchika alikua anaota au!?

Ngoja tuendelee subiri vimbwanga.
 
Leo kasoma hotuba anaenda vizuri..sema sasa akiachiwa kuhutubia bila kusoma hotuba..hua na majanga matupu..

Hata mimi nilishangaa kaenda mpaka dakika ya tano hakuna shombo, ikabidi niangalie vizuri, hapo ndio nikakuta anasoma. Ni bora tu abaki hapohapo kwenye hotuba za kuandikiwa kwani kipaji cha kuhutubia toka kichwani hana. Sana sana na kujenga chuki na kukwaza watu.

Naipongeza mitandao ya kijamii kumsema mpaka ikabidi akubali tu. Nakumbuka hapa jukwaani kulikuwa na uzi unaotabiri hotuba yake itazungumzia nini, na uzi mwingine ukisema hotuba zake hazina jipya. Hili la kuongeza mishahara nalo limefanyiwa kazi na ndio maana jana msemaji wa serekali alikuja kusafisha njia.
 
Hotuba zake zimeshakuwa kama hadithi kwa watoto, lazima kuwe na kiitikio"uongo njoo utamu na maisha magumu kolea"Namba tunaendelea kusoma!!!!!!!
 
Siku izi kuna msemaji wetu, atakuja kukanusha usijali. Ni ama hatujamuelewa magu, au mkuchika. Kuna mmoja yupo sahihi
 
Back
Top Bottom