Zanzibar kuandikisha vitambulisho Oktoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kuandikisha vitambulisho Oktoba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bagwell, Sep 29, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zoezi la kuwawezesha wananchi kuwa na vitambulisho vya Uraia wa Tanzania litaanza kutekelezwa mwezi ujao kwa upande wa Zanzibar.

  Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa zoezi hilo imekamilika katika kanda kadhaa kwa upande wa Tanzania bara.

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambuolisho vya Tanzania (NIDA) Zanzibar, Vuai Mussa Suleiman, aliwaambia waandishi wa habari huko Rahaleo, zoezi hilo litaanza Oktoba 31, mwaka huu.

  Alisema wananchi wote wenye sifa za uraia wa Tanzania watasajiliwa na kupatiwa vitambulisho hivyo na kuwataka wananchi kujitokeza.

  Hata hivyo, alisema awamu ya kwanza ya kutoa vitambulisho ilifanyika kwa watumishi wa umma wa Serikali Zanzibar na Muungano.

  Alisema vitambulisho hivyo vina umuhimu mkubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo matibabu, mikopo ya elimu ya juu pamoja na ukataji wa lesseni za biashara na hati za kusafiria.

  Mkurugenzi huyo alisema vitambulisho hivyo vitasadia serikali kuwatambua raia wake katika utoaji wa huduma za jamii na katika kuipanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.

  Hata hivyo alisema kabla ya kusajiliwa kila mwanachi atatakiwa kuonyesha kielelezo cha kuthibitisha uraia wake kama cheti cha kuzaliwa, kadi ya mpiga kura au cheti cha elimu ya msingi.

  Alisema kwamba NIDA haitatumia nguvu kusajili watu ambao hawatakuwa tayari kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya Taifa.  Napenda kuwauliza viongozi wa serikali.....Inamana vile vitambulisho vya mkaazi wa Zanzibar ndio havitotumika tena au ndio tuseme kua nia ya kuifanya Zanzibar kma mkoa ndio inakaribia kwa hili sikubaliani nalo na sipo tayari kuandikisha katika hivyo vitambulisho...
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,595
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Umesema mwenyewe wanataka kuufanya mkoa? Ndiyo zanzibar ni mkoa ndani ya Tanzania! Kama hutaki basiii.
   
Loading...