Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Natafakari kidogo hali ya Zanzibar!. Kujitangazia matokeo ni kosa la jinai!, kama ni kweli Maalim Seif, amejitangazia ushindi, kwa nini mpaka sasa hajashitakiwa?

Na kilichofanywa na M/Kiti wa ZEK kuufuta uchaguzi ni kinyume cha sheria! amepata wapi mamlaka hayo na kwa kutumia kifungu kipi? Zanzibar si kuna wanasheria, mbona Jecha hajashitakiwa?

Pasco
 
Tatizo halipo kwa Jecha wala Maalim.....tatizo ni kwamba ccm imeshindwa uchaguzi kule Visiwani Zanzibar na wamebana ila najua wataachia.
By Mhandisi jiwe linaloishi
 
kujitangaza ww mshindi isiwe sababu ya kufuta matokeo. Huku Lowassa alijitangaza mshindi lakini haikuzuia Tume kuendelea na taratibu zake.

Ina maana kama mgombea wa ADC angejitangaza mshindi uchanguzi ungefutwaa??
 
Maalim hakujitangazia kuwa yy ameshinda. Alitaja idadi ya kura alizopata na pia alitaja kura za mgombea mwenzake Shein, na aliitaka Tume ya Uchaguzi imtangaze Mshindi bila ya kuchelewa. Ccm wameshindwa sasa wanaleta Visingizio lukuki.
Ccm huwe kuitetea kwa hali yoyote hata uwe Mwanasheria uliebobea, mwisho wa siku itakutia aibu maana haina hadhi tena ya kutetewa.
Tume ifanye haraka itangaze Mshindi wa Urais ili wananchi waendelee na Shughuli zao.
 
Hivi kumtangaza mshindi wa uchaguzi si mpaka uwe na mamlaka kisheria?

Unapomtanga mshindi si kuna kifungu unatumia kumtangaza mshindi?

Maalimu alitumia kifungu gani kujitangaza?

Huku ni kuweweseka tu na hakuna kesi hapa!

Alichotamka Maalim kwa mujibu wa sheria sio rasimi na hivyo hakuna uwezekano wa kusema kajitangaza mshindi na hata kisheria sijui utathibitisha vipi kuwa kajitangaza mshindi wakati mamlaka hana.

Hii sheria imeacha loophole mtu kutamka kura alizopata na kusema mimi ndio mshindi pasipokuwa na kosa kisheria.
 
l
Tatizo halipo kwa Jecha wala Maalim.....tatizo ni kwamba ccm imeshindwa uchaguzi kule Visiwani Zanzibar na wamebana ila najua wataachia.
By Mhandisi jiwe linaloishi
Labda tujiulize ikiwa ccm ingekuwa imeshinda kwa mazingira aliyosema JEcha jE, angefuta uchaguzi? na je ccm wange react vipi?
 
Jecha alipofuta uchaguzi ni nani alikuwa amejaza fomu ya malalamiko?
Paschal jiongeze, kama kusoma hujui basi hata picha huoni?.
Paskali jibu hili swali

Unapigwa na pacha mmoja unaenda kumshtakia kwa pacha mwenzie?
Mkuu Gamba la Nyoka, msimamo wangu kuhusu kilichotokea Zanzibar uko wazi kabisa, Jecha hakuwa na mamlaka yale ya kujiugeuza ZEC, alichofanya Jecha ni kitendo haramu, lakini ili haramu iwe ni haramu kweli, lazima iharimishwe, haramu isipoharimishwa hugeuka halal!. Kwa vile ile haramu ya Jecha haikuharimishwa, hivyo ikahalalishwa na uchaguzi wa marudio.

Pia nikatolea mfano wa kubakwa. Kubaka ni kosa la jinai, lakini ili liwe kosa, lazima anayebakwa alalamike, mwanamke akibakwa asipolalamika, na akabakwa tena na tena, atahesabika ameridhia, hivyo Wazanzibari katika umoja wao, wameridhia unakaji huu wa demokrasia Zanzibar, kwa sababu hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, kulalamikia kwenye media sio utaratibu rasmi wa kuwasilisha , malalamiko.

Kuhusu hili la Zanzibar, mimi mwenyewe tuu nimepandisha nyuzi Zaidi ya 10 na hizi ni baadhi tuu.
  1. Zanzibar: Kama Maalim Kajitangazia Ushindi, kwa nini hajashitakiwa? Jecha Kapata Wapi Mamlaka ile?
  2. Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
  3. Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote
  4. Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?
  5. Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto, lakini ipo!, na hakuna aliyejiuzulu!
  6. CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake
  7. Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar!.
  8. Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!
  9. Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .
  10. Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!
  11. Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!
  12. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Paskali
 
Na kilichofanywa na M/Kiti wa ZEK kuufuta uchaguzi ni kinyume cha sheria! amepata wapi mamlaka hayo na kwa kutumia kifungu kipi? Zanzibar si kuna wanasheria, mbona Jecha hajashitakiwa?

Pasco
Ninafuatilia hii kesi ya Uchaguzi Kenya, kwa hoja zinavyotolewa, ni kama Tanzania hatuna Mawakili!. Kumbe alichokifanya Chebukat ni sawa na alichokifanya Jecha!.

Chebukat kajigeuza tume ya uchaguzi Kenya na kumtangaza Ruto kashinda. Jecha hakuwa na mamlaka ya kujigeuza ZEC na kufuta uchaguzi!.

Tofauti ya Kenya na Tanzania, sisi matokeo ya urais yakiisha tangazwa ni final and conclusive, hayawezi kupingwa mahakamani.

Kilichofanyika Zanzibar ile 2015 ndicho kilichofanyika Kenya. Mahakama Kuu inakwenda kufuta matokeo, zoezi la kuhesabu upya kurudiwa, kama Ruto ameshinda kweli, then atatangazwa baada ya kuhesabu upya kwenye majumlisho.

Kiukweli kabisa kwenye tasnia ya sheria, issues serious kama hizi ni kama hatuna kabisa mawakili!.

Tunapoelekea kwenye Mtangamano wa Africa Mashariki, ukifuka muda wa free movement of labor, kiukweli mawakili wa Kenya watakomba almost everything kutoka kwa mawakili lala wa Tanzania!.
P
 
Unamuongelea mwenyekiti wa ZEC ambaye miaka 5 baadaye alikuja kuchukua fomu ya urais kupitia CCM. Kweli CCM ni hovyo sana

Hadi hapo huoni Tanzania ni nchi ya maigizo .

Inakuaje referee anayetakiwa kuoversee mtanange dimbani anachagua upande.

I'm not boarding.
 
Ninafuatilia hii kesi ya Uchaguzi Kenya, kwa hoja zinavyotolewa, ni kama Tanzania hatuna Mawakili!. Kumbe alichokifanya Chebukat ni sawa na alichokifanya Jecha!.

Chebukat kajigeuza tume ya uchaguzi Kenya na kumtangaza Ruto kashinda. Jecha hakuwa na mamlaka ya kujigeuza ZEC na kufuta uchaguzi!.

Tofauti ya Kenya na Tanzania, sisi matokeo ya urais yakiisha tangazwa ni final and conclusive, hayawezi kupingwa mahakamani.

Kilichofanyika Zanzibar ile 2015 ndicho kilichofanyika Kenya. Mahakama Kuu inakwenda kufuta matokeo, zoezi la kuhesabu upya kurudiwa, kama Ruto ameshinda kweli, then atatangazwa baada ya kuhesabu upya kwenye majumlisho.

Kiukweli kabisa kwenye tasnia ya sheria, issues serious kama hizi ni kama hatuna kabisa mawakili!.

Tunapoelekea kwenye Mtangamano wa Africa Mashariki, ukifuka muda wa free movement of labor, kiukweli mawakili wa Kenya watakomba almost everything kutoka kwa mawakili lala wa Tanzania!.
P
Hivi na kenya wanajiita mawakili wasomi kama huku kwetu?
 
Back
Top Bottom