Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Tokea vilipoumbwa visiwa hivi vilivyo jaaliwa kuwa na rasilimali ya kutosha, Zanzibar iliweza kustawisha uchumi wake bila ya kutetereka. Mbali na rasilmali ardhi, kilimo kilichukuwa nafasi yake kwa mazao kama vile, karafuu, mbata, pilipili( chillies) pamoja na viungo ( spices) na kwa pamoja vilijenga ngome imara ya uchumi,
Kuangushwa kwa rasilmali hii kuli tokana na siasa chafu na uongozi dhaifu, lakini bado mungu bado hajaisahau Zanzibar. Zanzibar imepata rasilmali nyengine ya mafuta, mbali ya kutoitumia " Zanziba Channel" kama kitega uchumi tuliiwacha kunufaisha watu wengine na kulitumia tokea 1964 na Zanzibar kuambulia patupu
"Latham Island kinachojuulikana kama Fungu baraka au fungu Kizimkazi ni kisiwa cha Zanzibar chenye utajiri mkubwa wa gesi na kinachokodolewa macho na Tanganyika"
Leo katika gazeti la serikali la "Zanzibar leo" limesema eti " utafiti" kuhusu uwepo wa mafuta Zanzibar unatia tamaa( una muelekeo mzuri)
Hii ni taarifa ya upotoshaji kwa lengo tu la kutumika kisiasa propaganda ya kuhadaa umma kuwa mafuta yetu karibu yataanza kuchimbwa. Utafiti wa mafuta Zanzibar ulifanywa na kampuni ya mafuta Shell kataika miaka ya '50 na hata kuwekwa kwenye Atlas za kufundushia za madarasa ya msingi kwenye '60 kwa kuonesha alama kwenye maeneo yenye mafuta " oil reserves"
Kama hiyo haitoshi kwenye December 2010 Antrim Energy ya Canada iliingia makubaliano na Zanzibar kufanya utafiti sio kuwepo kwa mafuta lakini kujua kiasi kama kilichokuwepo kinatosha kwa biashara?
Lakini taarifa ya " Zanzibar Leo" inaonesha tu na kutanabahisha kuwa usimamizi bora ya rasilmali zetu hauko kwenye mikono mizuri na tunakesha kumtafuta "mtu" wa kusimamia mirathi ya rasilmali zetu kwani wenye mali wanaonekana kuwa ni taabani na mahtuti. Tumebakishwa na kubambakizwa nyimbo za kutiana moyo tu,- CCM mbele kwa mbele.