Zanzibar ikijitoa kwenye Muungano???

Zanzibar ikijitoa kwenye Muungano???

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,019
Reaction score
4,695
Wana jukukwaa
Kwa kile kinachoendelea zanzibar sasa nadhani kila mmoja anakielewa.
Wana ccm mko busy mnasherehekea ushindi huku mkisahau kuwa bila zanzibar ccm haipo...
Leo wako ktk sintofahamu lakini masikio yenu yameziba mnasahau kuwa hata magufuti ni rais wa muungano si wa tanganyika.. Mnazidi kumkorofisha maalim seif mnasahau kuwa wakati wowote anaweza kuwa rais wa zanzibar... Je leo hii akishinda urais kwa namna yoyote na akajitoa kwenye muungano ccm itakuwa wapi....??? Rais wenu wa muungano atakuwa wapi..??? Tafakirini hili na hakikisheni mnatafuta suruhu zanzibar maana mambo yakiharibika nyie ndio waathilika wakubwa.....!!!!
Yetu macho.......!!
 
Suala la Zanzibar kujitoa kwenye Muungano liko Karibu sana.
Jitihada za CCM za kupindisha Haki kule visiwani kutaleta Machafuko ambayo hayajawahi kutokea.
 
Kwa kinachoendelea sasa, ni dhahiri kwamba ccm bara wanadharau sana wenzao wa zanzibar. Vile vile imedhihirisha ni namna gani serikali ya ccm haioni kama zanzibar ina umuhimu wala thamani yoyote kwenye muungano.

Hii ni kutokana na kutangaza raisi bila kuajli kama wazanzibar wamepiga kura ama la. Kwa hiyo inatafsiriwa kwamba wazanzibar ni watu wa kuburuzwa na hawana mchango wowote wa muhimu kwenye maamuzi.

Ni sawa na kusema wazanzibar ni nyenzo tu ya matumizi ya ccm bara. Hiyo ndiyo taswira ambayo ccm kwa kiburi,ubabe na hila zak inaionyesha na iko dhahiri kwa mtu yeyote.

Kwa mantiki hiyo, sidhani kwamba Zanzibar inalengo la kujiondoa kwenye muungano. Ila kama ikitokea hivo, ni kwa sababu imefukuzwa na hivyo lazima itafute namna ya kuanza kusimama peke yake. Sioni nia nzuri ya ccm kwenye muungano wetu. Wazanzibar hawana tatizo katika hili ila shida iko ccm.
 
hamna kitu kama hicho ni fikira hewa na znz itaendelea kuwa tz visiwani kama kawaida! jeuri hiyo hawana
 
Wazanzibari wanauthamini Muungano isipokuwa CCM ndio hawauthamini.Wameziba masikio na wamejipofusha macho bila kufikiria kama itakuja kuwadhuru kwa namna moja ama nyengine.Wanajua kama ushindi upo kwa wapinzani kwahivo ikiwa itashindikana kukaa madarakani basi watahakikisha nchi wanaichafua ili iwe shughuli kwa wapinzani kuiweka sawa nchi.Na viongozi watajiondokea na kuwacha maumivu kwa wananchi ili ionekane kuwa wao CCM waliweza kulinda Amani na kumbe wao ndiowachafuzi wa amai.

AMAN KWENU WOTE
 
Enyi Watanzania Bara.. Msifawafanye Zanzibar colony letu tafadhali.. Mpeni Maalim kiti ameshinda
 
Wana jukukwaa
Kwa kile kinachoendelea zanzibar sasa nadhani kila mmoja anakielewa.
Wana ccm mko busy mnasherehekea ushindi huku mkisahau kuwa bila zanzibar ccm haipo...
Leo wako ktk sintofahamu lakini masikio yenu yameziba mnasahau kuwa hata magufuti ni rais wa muungano si wa tanganyika.. Mnazidi kumkorofisha maalim seif mnasahau kuwa wakati wowote anaweza kuwa rais wa zanzibar... Je leo hii akishinda urais kwa namna yoyote na akajitoa kwenye muungano ccm itakuwa wapi....??? Rais wenu wa muungano atakuwa wapi..??? Tafakirini hili na hakikisheni mnatafuta suruhu zanzibar maana mambo yakiharibika nyie ndio waathilika wakubwa.....!!!!
Yetu macho.......!!

mzikilizeni mtoto wa karume , Fatma Karume akieleza nani anahusika na kufuta uchaguzi..

https://soundcloud.com/m1m2-1/aud-2...soundcloud.com/m1m2-1/aud-20151029-wa0000-mp3
 
Back
Top Bottom