Kupongezwa si jambo la ajabu. Hata majambazi wakifanikiwa kwenye ujambazi wao huwa wanapongezana sana. Lililo la muhimu ni je, unapongezwa kwa jambo gani na kwa kufanya nini. Sielewi pongezi za mazingaombwe ya Zanzibar ni pongezi za nini. Kilichofanyika ni ufujaji wa pesa.
Hivi baada ya CUF kugomea kushiriki uchaguzi fake, kuna mpumbavu yeyote aliyekuwa akiamini kuwa Shein hatatangazwa Rais wa Zanzibar? Kwa nini kupoteza pesa kwa jambo lililokwishaamuliwa? Waafrika tutaendelea kudharaulika na wazungu kuwa hatujafikia sifa za kuwa binadamu kama tutaendelea kuwa na tawala hizi zisizoheshimu demokrasia, sheria na katiba.
Kila uovu huwa agent wake, na katika hili ni Jecha. Kama Wazanzibari wameshindwa kumwadhibu Jecha, Muumba ndiye ajuaye ni nini ujira wake hapa Dunia na baada ya maisha ya hapa Duniani. Nawaonea huruma wanawe maana hawataweza kujivunia Baba yao mbele ya macho ya wastaarabu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.